Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nakumbuka mwaka 1972 tulitoka Bulombora jkt Hadi Nguruka Kijiji Cha Mtego kujenga Zahanati kufika huku tukaanza ujenzi Kama kawaida ya majkt wakaanza kuwahonga mabinti wa Kijiji mchele Hadi wake za watu Bwana weee, habari zikavuma kuwa Kati yetu Kuna wakware kumbe wanakijiji wakakaa vikao vya Siri na kuazimia kuwa hawatutaki tuondoka na Kama ni Zahanati hawaitaki kwa hiyo tuondoke.


kijiji wakaenda porini na kukata mafimbo na marungu tayari kutuadhibu maana tumeacha kilicho tupeleka .Mimi nilikuwa na dogodogo moja matata sana.sasa siku akafika ya kutupiga nadhani ilikuwa jumapili,jirani kambi kulikuwa kilabu Cha pombe ya kienyeji miminilikuwa hapo ,saa 10 jioni Mungu wangu nilishangaa karibu nusu ya Kijiji wanna marungu na wanapiga kila JKT huku wanauliza kwa Nini mnatongoza wake zetu.ile nataka kutimua mbio wapi nikadakwa e bwana e kill si kipigo usiombe.

Jamaa yangu anaitwa Kalikubwa nikamuona yupo chini anakoroma nikaanza kushushiwa kipigo,nikabebwa na kutumbukizwa katika pipa la pombe Sasa Mimi naomba msaada wapi,kumbe kwa kunitumbukiza katika pipa la pombe kukanisaidia wengine wakidai ule ni uharibifu wa pombe kwa hiyo wakanichomoa humo ,wakati wanarumbana Mimi nikatoka nduki,huyo huyo huyohuyo nikatokomea msituni

Cha ajabu huko porini nikamkuta mwenzangu Mr Mika,mwenzangu angalau alikuwa vizuri tukaondoka Hadi Nguruka station nikamuomba mwenzangu anpe nguo akanipa.usiku tukapanda treni Hadi Tabora,mwaka 1982 niliamua kwenda Tena Hadi Nguruka na kwenda Kijiji Cha Mtego wakati huo nimesha jiunga na jeshi la polisi,kweli Jkt sintosahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ya maji niliiacha kama ilivyo, yaani ukienda station kuchota maji mchana unarudi usiku, pale ni jeshi ndogo, kuna lile roli linaitwa Samson linaleta maji wanafunzi full kugombaniana, napakumbuka kwasakwasa kule sokoni, old is gold
Haya mkuu hongera. Kuna mabadiliko yoyote? Shida ya maji bado iko? Mnaenda “stesheni” kugombea maji na wafungwa? Mlima wa kwa koko ushaenda? Kuchanja kuni porini?[emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo saa hivi ni sgt nani mkubwa[emoji3]
 
Sisi tulihamishiwa 822kj ramkoma kuna mwenzetu akawa anamendea mtoto wa kota kule kumbe kaka zake wanaona na wanajua asee siku jamaa yuko gurd kisimani ( kule kuna kisima kile cha chini cha kutoboa ardhi kumefunga pump)basi pale huwa inalindwa huwezi amini jamaa (kaka wa bint)waenda na kisu wakamchoma cha tumboni kama sio bugando hospital jamaa kidogo tumkose
 
Umenikumbusha mbali sana, gendagenda na kwamsanga tumehamia tumbili na nyani hatari, pia umenikumbusha afande kibakuli, ni kijeda fulani ivi kinajiamini, namkumbuka afande dick tulikuwa na bifu la demu alitokea kunizimikia afu hamtaki msela, nilikula doso za ajabu pale combani F hiyo ilikuwa 2013, wapi afande kariata
Kibakuri komando saiv ahaha mgambo jkt

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu unakufahamu AMAZON,long live kanembwa
 
Wale wa Mlale jkt wapo wapi 842KJ OP KIKWETE 2015
wapi RSM William
Wapi sir meja mwarabu
Wapi afande Nyingo
Wapi afande pilato

Wapi afande wa kikosi Lyimo mchaga aliyekosa mwili hahaaaa


A-COY YA DEMO ndio mana molari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa OperesheniTIMIZA nikiwa na maafande wachache ninaowafahamu pale Ruvu, Marehemu Makame Mkuu wa Kambi, Urio nakumbuka alikuwa Luteni, Londo, Agnes, Afande machibya aliyewahi kuwa Mkuu wa Mikoa kadhaa etc. Nakumbuka sana kuchoma nyama porini hasa tukiwa zamu ya kupika, pili kula mayai mabichi hasa ukipangwa kwenda kufanya kazi kwenye mabanda, tatu siku Bendi ya muziki inapotumbuiza siku hiyo kwenye kambi la Ruvu. Mwisho hakuna ya Mwanamke au Mwanaume wote siku ya kwanza mnatupiwa bukta/pitishot ya kuvaa na ndiyo sare ya kila siku. Kweli ilipendeza na pale mara chache kuugua sababu ya mikiki mikiki ya pale.
 
Nimeishi jirani na afande machibya ame staafu akiwa Lt Col alikuwa mtu poa yeye hata mkewe pia sikujua Kama alikuwa Ruvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afande Machibya ni mtu mwenye utaratibu sana. Yeye kazi ni kazi hataki masihara.
 
Ni mengi sana siwezi hata kuyaandika hapa..ila comment za wadau wengi zimeniwakilisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…