Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

841 kj - Operation Oljoro,
.Mkuu wa kikos Calonel Mlay,
.Charlie Coy
.OC Shayo
.Idetero tulipalilia miraba ya kutosha.
.lindo kipindi cha nyahenge asikuambie mtu,una freez
.kurudi na furushi la kuni ukitoka kwenye mraba na jembe juu,
.adhabu detach ya lungemba

Siwezi sahau kabisa zile pilika maishani.
 
Nawatafuta ndugu zangu wa op miaka 50,832kj danger coy intake ya tatu mujibu(2013) platoon number moja,section number moja
 
Nimecheka mpaka kilio
 
Habari wanaungwana,

Moja kwa moja niende kwenye maada. Kama wewe ni miongoni mwa watu umepitia JKT lazima kuna kituko umefanya au ulishuhudia ukikikumbuka kinakufanya ufurahi mpaka leo.

Mimi huwa nakumbuka tulikuwa na jamaa yangu anaitwa Charles wakati wa msosi tulikuwa tunaenda kukaa meza yenye wasichana wengi sababu walikuwa hawamalizi msosi halaf wakiondoka tunausogeza tunamalizia😂😂!

Hii tabia nlioona tena chuoni rafiki alimnunulia demu chakula akala kidogo tu akaachia, alilalamika sana akaamua kuumalizia mwenyewe mbele yake. Salute kwa mwanangu nimuhifadhi jina.
 
Kulikuwa na Operesheni Oljoro? Ilikuwaje hapo Mafinga? Mwaka gani?
 
Nimecheka mpaka kilio
siku moja mkuu wa kikosi lt col Meena wa Ruvu 832kj mwaka 1986 alikamata makuruta walikuwa wanatoroka.Akawapakia kwenye gari lake nyuma magari wakati huo yaliitwa Dube.Akawa anawaendesha kuwapeleka kikosini wakapewe adhabu cha ajabu alivofika kati ya waliokamatwa wa5 wanne hawakuwepo waliruka kwenye gari wakakimbia akabakia mmoja tu.
Akasema hawa ndio askari hata vitani wakikamatwa ni raisi kumkimbia adui.
Yule aliyebaki akaambiwa sasa wewe utabeba adhabu za wenzako wote maana ni askari rahisi sana kukamatwa na adui kisha ukaenda kutoa siri wewe ni askari legelege.
 
Heshima yako mkuu[emoji23][emoji23][emoji23]
Unatisha, op gani hiyo? Kifupi ambae hakupita jkt(ya enzi zile) hawezi jua utamu wake. Ni sehemu ambayo akili ilitumika sana kufanikisha kila jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…