Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Kuna la kukumbuka zaidi ya palizi?
Aaaah,pole mi nilifanya palizi msimu mmoja ilofata ni mwendo wa kukaba vitengo yaani nilikuwa mbabaishaji sana yaani mi nimelivuna sana jeshi wakati wengine likiwavuna
 
🤣🤣🤣We jamaa umenifurahisha kwel aisee
 
Kanembwa pale kwa mzee mbiji,, Afande kibutu,,Teddi mtu m-bad kabsa serengeti wanachura sema mda wa kusimamisha jogoo ndo aupo[emoji34]
Daah Aisee private Kibutu ni hatr Sana Yule mwamba katupigisha doso kinoma,ctosahau Ilikuw kweny mazoezi ya kwata bwana si nikaingia mtelo nikakosea alinirusha mtama kimo cha ng'ombe,
 
Daah Aisee private Kibutu ni hatr Sana Yule mwamba katupigisha doso kinoma,ctosahau Ilikuw kweny mazoezi ya kwata bwana si nikaingia mtelo nikakosea alinirusha mtama kimo cha ng'ombe,
Aisee yule ni mtu hatari sana kule kwenye palizi ndo hatari kuna serengeti alipigwa mpka kutapika dam nafkr atamchukia kibutu milele daima Amina
 
Sitosahau kwa wale tulioanzia Mafinga JKT enzi za kanali MLAY, then baadhi ya vijana tuliosoma masomo ya sayansi tukachaguliwa kwenda JWTZ, pale Twalipo camp Dar, kwenye interview ya u pilot. Kwa wale ambao hatukutaka kujiunga na JWTZ si wakaamua kuturudisha makutupora JKT ili kumalizia mafunzo ya JKT. Bwanaaa wee pale Makutupora si wakaanza kutupiga drill na mazoezi ya kutukomoa?? Tuliotoka Mafinga tukaamua kutoroka pale Makutupora na kurudi zetu Mafinga, aisee siwezi sahau ile mission impossible. Tulitoroka kwa kutoka mmoja mmoja from kwenye hanga to the meeting point vichakani, then baada ya kuona tumetimia robo tatu (wengine walibadili mawazo hawakuja) tukaanza safari (hiyo ni saa 8 usiku!!) ya kwenda Dodoma mjini kwa mguu, kupitia porini kwenye mitunduru. All in all mwishowe tuliingia Mafinga JKT baada ya siku 2 au 3 kama sijakosea, na bahati nzuri tukapokewa vizuri tuu, daaah.
 
Hii ni ya kipekee
 
[emoji28][emoji28][emoji28]dah hii imenifurahisha sana yaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…