X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aaaah,pole mi nilifanya palizi msimu mmoja ilofata ni mwendo wa kukaba vitengo yaani nilikuwa mbabaishaji sana yaani mi nimelivuna sana jeshi wakati wengine likiwavunaKuna la kukumbuka zaidi ya palizi?
Tupe utundu mkuuAaaah,pole mi nilifanya palizi msimu mmoja ilofata ni mwendo wa kukaba vitengo yaani nilikuwa mbabaishaji sana yaani mi nimelivuna sana jeshi wakati wengine likiwavuna
Jeshini ukijitia mtiifu utajuta yaani unajiraa we and no appreciation baada ya kujua hilo sikuwahi kujichosha zaidi ya kula utawalaTupe utundu mkuu
Afande bafeni anapenda kuongea matusi kinoma,tulikuwa nae eagle coy op flani hivi ya karibuniMajirani zetu nyie, sisi tulikua Eagle coy
Op gani kaka,832kjAfande bafeni anapenda kuongea matusi kinoma,tulikuwa nae eagle coy op flani hivi ya karibuni
Makao kaka hii ya 2019 tu hapaOp gani kaka,832kj
🤣🤣🤣We jamaa umenifurahisha kwel aiseeKatika vitu Mungu amenibariki ni kutokuwa na wasiwasi ninapojua nipo katika jambo au kitu sahihi.
Story iko hivi.
Miaka ya zamani nipo zangu JKT ndio nimefika hata intro. Hatujapitia tunasubiri mkuu wa kikosi arudi kutoka Dar es Salaam sina hili wala lile nimetoka zangu canteen naenda kwa mwendo wa kuruti (kukimbia kwa ukakamavu) nimepiga zangu green vest na kikaptula changu chini nina converse kali za kijani mpauko sina habari.
Naona hali si ya kawaida njia ya kuelekea uwanjani(master parade ground) hakuna watu kabisa na ilikuwa ni njia rahisi ukipita hapo unaingia kombania.
Nikajusemea moyoni labda watu wameenda kwenye fatiki acha nikaze mwendo nirudi zangu kulinda Hanga (sijui nimepatia ili neno) ,
Njiani nakutana na msoja amenuna mbaya begani yuko na bibi na bwana nikajiongeza kuwa huyu atakuwa afisa mkubwa mathalani Meja nikapunguza mwendo bana mikono nikatoa salamu kwa mbwembwe zote “Jambo Afande “.
Chuma kikageuka macho makavu hakikutoa mlio hata kidogo nilipoona amegeuka na kurudisha shingo nikasema Aaah kashaipokea hiyo nikachanganya miguu kama hakijatokea kitu mbio zikaendelea kuelekea kombania.
Nafika tu Sir meja wa kombania ananiambia kuruti umepita wapi? Bila ajizi nikamwambia maeneo ya uwanjani jamaa akashtuka akaniambia haukumwona mkuu wa kikosi! Kaubaridi kidogo kalinipitia nikasema eeeh nilimwona ila sikuwa nimemfahamu.
Ebwana kumbe siku ile alikuwa na kibarua na Level 3 walitinyanga sijui madudu gani jamaa walikula kazi pale uwanjani mpaka kombat zikawa za brown kesho yake wakawa Mbogo aliyejeruhiwa walitupiga tifu zito sana kwenye intro kama sikufa pale maisha yangu ni marefu sana .
Wakati mwengine nitawaletea jinsi nilivyokimbia mkesha wa six weeks na kutokomea porini nisijue naenda wapi [emoji23] .
Kuna wakati pia niliongoza kundi la majanga wazee wa kazi za hovyo hovyo nililipamba mpaka watu wakawa wanakimbia parade ya mwisho kuja kujiunga maana lilikuwa na watoto wakali pamoja na vibe za kutosha.
Mwisho wa siku nilipewa zangu B nadhani zoezi la shabaha lilinibeba nilipiga zangu range vizuri kwa kufuata maelekezo ya kukata pumzi na composure nikaosha jina mbele ya vigogo wa kambi.
Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna la kukumbuka zaidi ya palizi?
Bafen bado yupo pale kumbe nilimuacha 2013Makao kaka hii ya 2019 tu hapa
Bado yupo mkuuBafen bado yupo pale kumbe nilimuacha 2013
Marwa ni coproral sa Hiv daah ana vituko saana Yule Afande,Magesa huyu ndo yule alipata ajali??
Daah Aisee private Kibutu ni hatr Sana Yule mwamba katupigisha doso kinoma,ctosahau Ilikuw kweny mazoezi ya kwata bwana si nikaingia mtelo nikakosea alinirusha mtama kimo cha ng'ombe,Kanembwa pale kwa mzee mbiji,, Afande kibutu,,Teddi mtu m-bad kabsa serengeti wanachura sema mda wa kusimamisha jogoo ndo aupo[emoji34]
Sir major ktundu the RSM e bnaa ana sauti ile kinomaaYule sir meja na sauti lake noma, nakumbuka tulienda nae range acha kbs.
Aisee yule ni mtu hatari sana kule kwenye palizi ndo hatari kuna serengeti alipigwa mpka kutapika dam nafkr atamchukia kibutu milele daima AminaDaah Aisee private Kibutu ni hatr Sana Yule mwamba katupigisha doso kinoma,ctosahau Ilikuw kweny mazoezi ya kwata bwana si nikaingia mtelo nikakosea alinirusha mtama kimo cha ng'ombe,
Hii ni ya kipekeeSaluti kwa masoldier wote wanaozijua hizi sehemu
Mlima nguruwe
Idetero
Kwa Balali (yule gavana wa BOT)
Airport
Kawawa
Njia ya kwenda mgororo
Kitundu hall
Mwamunyange recreation
Bila kumsahau
Afande pilato (Mhenga)
Captain nkya
From kambi ya ubaridini....yaani ilikuwa ikifika night unavaa nguo zote zilizopo kwenye tranka na asubuhi maafande wanawakomoa hamrudi bwenin (angani) so mnakimbia kuifuata chai na manguo yote mwilini.
Kunakipindi kama snow inashuka maafande wanaiita "nyahenge" kwa kihehe.
Kuna siku baridi kali alfajiri kuna kuruti akajificha jalalani akalala usingizi wa pono. Kimbembe muda wa usafi watu kuchoma jalala alitoka mtu kama mzimu akazua kataharuki.
Vile vyoo vya mabanzi ambavyo hakuna kitu kinachozuia wa shimo moja asimuone mwingine. Aliwahi kuja demu akanikuta nimechutama pale akashusha kombati akashusha mzigo hakujisafisha akavaa kombati akaondoka alinifunza kuivua aibu pale kambini.
Kuna siku tunaenda kumwagilia miparachichi. Wakati tunashuka mteremko wa kutoka kambini kuingia mafinga mjini gari IVECCO ilikimbia hadi tukaacha kuimba kwa morali cha ajabu dereva afande akatoa kichwa akawa anasema kumamayo nimesema imbeni kwa morali na hapo one week before kuna ajali ilitokea ikaaua maafande.
I mic good moment una bust wali unaficha kwenye kofia ya komboti.
Kuvaa kama afande kisha mnacheki pamoja game ya EPL pale kitundu hall.
Shall out kwa maafande wangu wote mtakaopita hapa.
[emoji28][emoji28][emoji28]dah hii imenifurahisha sana yaaniJamaa mmoja alikuwa mwoga sana, anaogopa sana adhabu. Kama kawaida ya jeshi. ilikuwa ni lazima utandike kitanda vizuri kwa style ya jeshi, kila kitu, shuka, blanketi, kitanda mess tin, kwa dressing. Haya yote unatakiwa ufanye kabla hujapurukushwa kwa wito wa 'FOLEN'! Basi huyu jamaa alikuwa anatandika kitanda chake vizuri usiku tukitoka disco, halafu alikuwa analala chini! Tulikuwa tunamcheka sana, lakini baadae tukawa tunamuonea huruma.
Njemba moja alikuwa akizurura kutwa na sururu. Akiulizwa, askari unakwenda wapi, anasema ametumwa kazi na afande fulani. Tulikuwa tunamuonea huruma maana alikuwa anazurura kutwa na sururu baada ya kulala porini kama sie wengine wajongomeaji.
Tulijifunza kutomaliza kazi mapema, maana ukiripoti umemaliza kazi uliyopewa, unabambikiziwa nyingine. Tulikuwa na midomo yenye fridge, maana kama jamaa yako alikuwa zamu jikoni, akikuchotea nyama au wali kwenye mess tin, unatakiwa umeze haraka, hata kama ni vya moto kiasi gani. Ulitakiwa uwe mwizi sana, hasa wa kofia, maana kama umeibiwa kofia na hukuvaa, unapewa adhabu. Mimi nilizoea kuwaibia maafande kofia zao, maana ilikuwa ni rahisi kwao kupata nyingine.
Katika kombania yetu tulikuwa na wahindi wawili. Siku moja kwenye disco, baada ya wiki kadhaa za kukaa jeshini, mhindi mmoja akawa anatufundisha wimbo wa kihindi. Tulijifunza, lakini yule mwingine akawa anacheka sana,. Sisi tukadhani kuwa maneno ya wimbo ule yanachekesha. Kesho yake ilibainika kuwa yule Mhindi aliyetufundisha ule wimbo ametoroka. Yule mhindi aliyebaki akatuambia alikuwa anacheka sana maana maneno ya wimbo ni: Kwaherini, mimi kesho natoroka!
Siku moja kombania yetu ilikuwa zamu. Platoon yetu ikapelekwa kwa kuku. Kama kawaida, ukishafika huko unakazana kubugia kwa wingi mayai mabichi kiasi utakachoweza. Baada ya kumaliza kazi, tukachukua mengine, tukajaza kwenye mifuko ya combat. Rafiki yetu mmoja akachukua mengine akayaweka kwenye jungle hat yake, halafu akaivaa.
Tukawa tunaondoka kutoka kwa kuku, tukiwa na dhamira ya kwenda kwenye jongomeo letu msituni. Mara tukakutana na ma MP. Kitu kilichotuponza siku hiyo ni kutokuvaa vizuri. Hatukufunga kamba boot, mashati hayakufungwa vifungo nk. MP mmoja akasema, 'Askari, simama. Mbona mmevaa kama askari wa kukodiwa?' Akamuita yule jamaa aliyevaa jungle hat yenye mayai. 'We, kuja hapa, mbona umening'iniza kofia?
Njoo hapa nikuonyeshe namna ya kuvaa'!! Akashika kofia, akaishusha kwa nguvu ili aizingushe zungushe kwa nguvu kichwani. Lo, si mayai yakavunjika! Yakaanza kumwagika usoni mwa jamaa. Basi tukazingirwa tusikimbie. Tukasachiwa likapatikana karai zima la mayai. Tukapigishwa fang fang usawa wa Quarter Guard, tayari kwa kufungwa na kuwa court marshalled.
Muda huo ulikuwa mchana na chakula cha ma MP kilikuwa kimeletwa. Basi ma MPwote, isipokuwa mmoja, wakaenda kula. Ikatokea kuwa kitabu cha kuandikisha mahabusu kimejaa, MP akaenda kuchukua kingine. Wakati huo tupo kwenye baraza la Quarter Guard, bado hatujawekwa ndani. Kuona upenyo huo, tukaamua tutoroke. Mmoja wetu akakumbuka kuwa tumesahau karai letu la mayai, akalirudia, tukatokomea nalo msituni. Mchana ule tulikula vizuri sana mayai ya kuchemsha .
Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio. Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!