Hayo yote waliyoongea wakubwa hapo juu yamenifurahisha na kunikumbusha mbaali sana,,,,nakumbuka mwaka 1993(operation miezi sita) mie na rafiki yangu aitwae gwakisa tulianza safari tokea mbeya kwenda arusha kambi ya oljoro,,,tulifika njia panda ya oljoro hiyosehemu inaitwa mbauda, mie na jamaa yangu tukashauriana ngoja tupate bia hata moja moja pale,,eneo hilo lilikuwa linauzwa bia pamoja na mbege,, tukaagiza bia moja moja na kikopo cha lita moja ya mbege,,,,,,,kwenye kona kabisa kulikuwa na bwana mmoja amekaa anakunywa mbege huku akituangalia sana,,,,,na kwa kuwa stori zetu yule mhudumu dada alitusikia kwamba tunaelekea kambini oljoro,,,akamstua yule bwana aliekaa pale pembeni akatumaki sura zetu vizuri,,,,,kesho yake yule bwana alizunguka kombania zote akitutafuta kumbe ni corporal alikuwa anaitwa HEKAHEKA akatudaka wote tuko kombania moja E(eagle coy) saa meja alikuwa anaitwa maduma ,,,huyu bwana alisema kuruta unakunywa bia wakati hekeheka anakunywa mbege leo mtakoma,,,, tulipewa adhabu sitosahau.