Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Allien,

Allien:

Wanaozaliwa na vipaji vya kufanya biashara au vitu vyovyote bila mafunzo are so rare. Lakini wengi wanazaliwa na instincts ambazo kwa namna fulani zinaboreshwa au kutoboreshwa na mazingira wanayokulia. Hivyo ngazi zote za elimu na maisha ni muhimu zilea na kuzikuza instincts za watu.

Kitu ambacho napinga matumizi ya JKT kutumika kama sehemu ya ujasiamali ni kuwa chombo chenyewe kiliundwa kama chombo cha ujasiamali lakini kilishindwa kufikia malengo yake.

kwa sisi tuliopitia JKT kwa ulazima wa shule zetu. JKT ilikuwa na maana nyingine.

Lakini kwa vijana waliojiunga kwa kujitolea JKT ilikuwa sehemu ya kujifunza ujasiamali. Walijifunza kazi nyingi tu na mategemeo yalikuwa wakimaliza mafunzo yao wanaweza kuanzisha shughuli zao wenyewe.

Wengi waliomaliza walitafuta kazi za kuajiriwa kama vijana wengine. Kwa mtaji huu marekebisho makubwa yanatakiwa hili JKT itoe wajasiliamali. Na kama marekebisho hayo yakifanyika basi JKT itapoteza muundo wake wa kijeshi.

Mtatumia juhudi nyingi kunishawishi kuwa mtu ambaye maisha yake yote ameishi kama mwanajeshi anayeishi kwenye nyumba ya bure na kutegemea pororo kumfundisha mtu kuwa mjasiliamali
icon10.gif


Ujasiliamali 101 na afande Kibuyu.
 
Mtu wa Kawaida,
Nyundo alikuwa na sura mbaya si kawaida.. masikini wa watu Nyundo aliugua akatutoka akawaacha kina Basekana, Sanga, Merdad, na of course Meja Omari mtaalamu bingwa wa magonjwa ya kuruta wa Kike!
 
Sikonge,

Huyu jamaa bwana fedha alikuwa aivinjari Ruvu na pikipiki akaopoa mtoto mmoja wa Kichaga ambaye walipata naye ajali, nafikiri yule binti alikuwa anaitwa Rose Lema, sijui kama alipona hiyo ajali!
 
kama sikosehi Cadanian vilikuwa ni vichwa vya Train vyenye speed nzuri. Hivyo mnaokimbia mchakachaka kwenye makundi inakuwa kama train inayovutwa na Canadian.


Canadian Spirit ilikuwa jina la nafikiri meli za speed boat kwenda Zanzibar. Yule alikuwa Afande Karubi aliyekuwa Oljoro, Mgulani kisha akahamia Mlalakua.
 
DawaKali,
Na weye kumbe ndio ulikuwa ukikaa kwenye hanga maalumu la Special coy wagonjwa, watoro na wanono 🙁?
 
Wakulu;

Je; kuna baaadhi ambao wako interested kuandika kitabu cha kumbukumbu za matukio haya?
 
Sanctus Mtsimbe,
Nami wanikumbusha mbali sana. Mimi nilikuwa makutupora operation miaka 30 ya uhuru. kulikuwa na afande Mwashamba ambaye sasa ni marehemu-R.I.P kipindi cha kwata alikuwa analala chini kuangalia miguu endapo yenda sawa wakati wa kwata na coment yake nikikumbuka huwa nacheka peke yangu ie, 'wewe unayepeleka mguu pande mguu sawa kama mbwa anayekojolea kisiki my friend nimekuona'.

Nilikuwa A coy na sir major wetu aliitwa afande Singira alikuwa hatoi adhabu bali maneno yake ya kukusimanga yalikuwa yanaliza mhusika na yanatoa burudani kwa wanaosikiliza. mfano kuna siku bogi la buhemba lilipita na tukasikia kuna mtu kafia safarini. yeye alisindikiza bogi aliporudi tuliuliza kwa masikitiko taarifa hiyo akatujibu 'ninyi ndo makabasii my friendi' akagundua hatukuelewa maana yake akaongeza 'kabasii ni mtu akaae mtunduruni kusema habari za watu kutwa nzima akija taharuki jioni anajikuta yanapigwa upepo pitshot ishaliwa na mchwa'.

Tunduruni ni aina ya bushes za Dom. Pia aweza kukupa kazi ukakosea sehemu basi atakusema 'lione roho mbaya tu utadhani abiria walokuwa wamepewa lifti ktk mashua wakati wote wanaomba eti Ee Mungu Pindua mashua tugawane Mbao' Jamaa adhabu zake watu wa pembeni walizipenda sana kwa kuwa ilikuwa ni burudani bali mwiba kwa anayesemwa.
 
@Laligeni,
E bwana Singira alikuwa kiboko ya njia hakunyung'unyi lakini habari ya maneno yake tu. Nakumbuka kuna siku tumeenda kugeuza tofari ili zikauke na upande wa pili, tukawa tumechoka, tumeswet na tunaonekana tusio na furaha jamaa akaanza maneno yake, 'Yaone, eti yanawaza tunateswa tunateswa, my friend ni njaa zenu tu ndo zilizowaleta hapa. mnajua bila kupita hapa hakuna post utakayopata, so kamlaumuni Mungu aliyeleta njaa kisha akajificha na kesi yake iko mahakamani angeonekana watu wangemrarua vipande.


Yaone yalivyoswetiana utafikiri yamejifukiza ubani wa kienyeji. tena yamenuniana utafikiri boga la kiangazi' ilikuwa ni burudani ya aina yake hata kama ulikuwa umenuna unajikuta jioni mkikutana na wenzenu mnacheka na kusahau matatizo yote. nawakumbuka sana Nancy morenje, Jacq bundala, Ev. Komba, Ngadu, Judith mlaki, na wengine wengi
 
Jamaa yaani umenikumbusha mbali sana, nilikuwa operation miaka 25 ya JKT, kambi ya Mafinga, sitmsahau CO Col. Mlay kwa makeke na mbwemwe zake kwani jeshi lilikuwa ndani ya damu yake, lakini kiboko kuliko wote alikuwa afande Nusu Mungu ! yeye alikuwa na mkwara sijapata kuona. Pembeni yake alikuwepo afande Mlay vituko vyao we acha tu.
 
Lole Gwakisa,

Gwakisa,

Umenikumbusha mbali kwa kutaja jina la Mwiba. Huyu alikuwa mpiga kwata mzuri na hasa akiwa na NCOs pale makutopora. Nilikuwa katika operation miaka ishirini ya Azimio la Arusha. Nilikuwa C coy na ninawakumbuka sana Afande Baineti, Gidamas, Pima, Mwiba na Afande Omary.

Nina kumbukumbu ya mambo mengi lakini nilifurahia sana jinsi na namna Afande Mwiba alivyokuwa na busara wakati mwingine. Yeye siku yuko zamu kesho yake, anakuja jioni anawataarifu kwamba atakuwa zamu kesho na kazi inayotakiwa kufanya labda ni kupalilia miraba ya zabibu. Kwa sauti yake ya zege anawaambia yeye hawezi kuja kumwamsha kruta ila anataka saa 11 alfajiri kila mtu awe kule tayari na kwamba tutakuta anatusubiri.

Basi mnaamshana saa 10 halafu mbio kwenda kwenye mizabibu na kuanza kupapalia. Mwiba anafika saa nne wakati tayari mmemaliza, halafu anawaambia, makamanda, safi sana hii!!! Mkwara wake ulikuwa mzito na wakutisha.

Nawakumbuka wanakombania wenzetu waliopata ajali mbaya ya gari wakati wanatoka kubeba magogo kule mayamaya akiwemo waziri mdogo wa Biashara na viwanda Mh. Cyril Chami, Andrew Kyabashasa (sijui huyu jamaa yuko wapi kwa sasa alikuwa ni section Trainee - ST), Kivuyo, Kabanda, Tryphone, Moshi na Bazil amabaye baadae alikuwa mpiga kinanda mzuri pale kwenye kanisa katoliki kawe (kwa sasa sijui yuko). Ajali ilikuwa mbaya lakini wote walipona.

Kama wengine walivyopendekeza, kuna haja ya kudocument hizi comments ili wale ambao hawakupita JKT wajue ni kitu gani wanakikosa.

Tiba
 
Jamaa yaani umenikumbusha mbali sana, nilikuwa operation miaka 25 ya JKT, kambi ya Mafinga, sitmsahau CO Col. Mlay kwa makeke na mbwemwe zake kwani jeshi lilikuwa ndani ya damu yake, lakini kiboko kuliko wote alikuwa afande Nusu Mungu ! yeye alikuwa na mkwara sijapata kuona. Pembeni yake alikuwepo afande Mlay vituko vyao we acha tu.

Mafinga JKT we acha tu, kulikuwa na RSM Mungure anatisha kama nini, MP Kamanda jina nimemsahau huwezi kumuangalia usoni mara mbili, Captain Frank( huyu alikuwa mzee wa Totos kwa kwenda mbele),.. F Coy SGT kawau Tesha ,Mikwala kama nini,anakwambia amesoma mpaka Tabora girls.Sameja Enock.
 
Mazee,
Duh! Na mimi nakumbuka mengi. Me nilikuwa Makutupora Operation "WAJIBU" mwaka 1984 na kumalizia Mpwapwa. Kulikuwa na afande mmoja mdogo mdogo kimwili. Alituacha hoi pale alipomuuliza kuruta mmoja WAKATI WA MLO WA MCHANA:
AFANDE[/B][/B]: We KURUTA mbona huli?
KURUTA: Afande...mi sina epitaiti (Appetite).
AFANDE: Mbona wengine wanazo mbili-mbili...We kuruta mpe mwenzako moja (Ilikuwa ni Mess-pan).
Makuruta waliokuwa kwenye foleni kwenye USAWA WA KUDULIA walicheka sana.
 
Ndio phase 2 mayai mabichii yanapigwa kwenye uji!
siku nilijogo kurudi nimekatisha kwa CO Meena, giza, nikakuta kuruta 2 nao wanavizia tuingie uwanjani, ghafla gari ya CO ikatokea na kutumulika taa usoni kila mtu alikimbia njia yake sijawahi ona nikatokea dipsensary nimesave ohh. Ila nilijifunza kufuga kuku hado leo huniwezi
 
Mlifaidi sana some experience lasts for a life time, natamani na mimi ningepata hio nafasi story zote zimenifanya nihisi na mimi nilishiriki, wengine tulikuwa ndio tunazaliwa lakini story hizi bado zipo ila kwa waliopitia huko wana decipline sana ya maisha kwa wengi wao sio wote kbs. Na ukakamavu wa hali ya juu ingerudi hivi sasa magonjwa kama kisukari yasingekuwepo vile baada ya jsehi mtu unakuwa na discipline ya mazoezi kujituma mara kwa mara na uchangamfu.
 
Nilikuwa Makutupora operation miaka 30 ya uhuru.Nilienjoy sana. kutoroka kwa sana ukichukulia kuwa nilikuwa bustanini, hadi aje kunoti kuwa hukuwepo ni too late.Kujipikilisha kama kawa maana makocho kocho ya kupika yote yapo bustani. Nakumbuka niliwahi kuugua kitu ambacho ilikuja bainika kuwa nilikuwa na damu nyingi kutokana na kula sana fruits na mboga mboga.

Nawakumbuka vijana machachari kama akina Mkumbo Mitula, Jackson Mwandiki, Rwegasira tulokuwa naye A coy na wengine wengi na sijui wapo wapi.Singira alikuwa kiboko ya njia hakupi adhabu bali vijembe vyake hutapenda uingie ktk anga zake. hakika jeshini kulikuwa na mambo na huwa naenjoy sana nikikutana na jeshi mates wangu maana hukumbuka mengi kuliko ma mates wa mashuleni.

Jeshini hakukuwa na kusoma na kipindi cha siasa PEO ambaye kwa sasa ni mwalimu jitegemee alikuwa anafundisha hakuna anayemsikiliza ndo kwanza watu wanakuwa wanajipa wasaa wa kusinzia zao hadi siku moja jamaa kajisahau ktk usingizi mzito na kujikuta anatoa mlio mmkubwa wa hewa chafu iliyochafua mazingira.Ukweli kuna haja ya kuandika kitabu
 
Kwa wale waliopitia Mgulani enzi za Mambolaghe, kujongo kupitia tobo usawa wa Salvation unasubiri wakati bendera inashushwa halafu unapita kwenye tobo . MPs wanasubiri mpaka bendera ishuke. Kwa upande mwingine , askari wa JKT wakati huo walikuwa integrity ya hali ya juu. Walikuwa na imani kubwa na system na ndiyo maana UWT walikuwa wana ajiri wengi kutoka huko. Apsom (ex DGI) naye aliwahi kuwa CO wa Mgulani.
 
Back
Top Bottom