Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

[emoji28][emoji28][emoji28] 842 kj mlale

Sitasahau siku nimekula doso mlangoni kisa nilitaka kwenda pasi huku nimevaa pensi. Siku hiyo nilipigwa doso toka saa 2 asubuhi mpaka saa nane wengine walivyorudi pasi

Op uadilifu 2008
 
Wapi mangi kibiro, gama, mzee zengo na moyo. embakasi, 842kj dah ipo siku nitaelezea life ya jkt humu.
[emoji28][emoji28][emoji28] 842 kj mlale

Sitasahau siku nimekula doso mlangoni kisa nilitaka kwenda pasi huku nimevaa pensi. Siku hiyo nilipigwa doso toka saa 2 asubuhi mpaka saa nane wengine walivyorudi pasi

Op uadilifu 2008
 
Sitasahau siku dawiri wa kombania yetu alipokamatwa pori akiliwa uroda na afande.. Yan tulikula doso si la kitoto hatukulala usiku wote na asubuhi mbio kama kawaida... Tulikunja ngumi... Mapenzi ya nyoka.. Kutembea kibatabata nk yaani usiku kucha na kadada kenyewe kapo kamelala maana kalikuwa kagonjwa ka pumu..
 
Nilikua chalii wa C coy alafu nilikua doja laana
Siku moja nilidoji nikakimbizwa na fande alafu kama jini vile nikapotelea chooni, yani namaanisha niliingia chooni alaf sijatoka afande nae akaingia kanitafuta bila kuniona

Jiulize nilijificha wapi? Nikiingia kwenye pipa la maji ya chooni alaf pipa lenyewe limejaaa maji full nilikua naibuka kidogo juu navuta hewa sekunde mbili alaf narud nazama ndani ya pipa dakika 4

Madoja wenzangu huko nje walipigwa tifu laana walikwepa ndege masaa 8
 
Jkt kanembwa 824 kj Afande CO bwegoge,
Chief instructor alikua Captain sebastian Tesha saivi ni major.
Kulikua na Luteni Mwakyobwe akahamishiwa mtabila afande mpenda kuruti ni major sasa uyu jamaa.
Private Marwa asee pt instructor
Marehemu magesa mboje mzee wa doso jamaa alikua anajipiga doso mweyewe anaruka uchura kilometer nne kutoka nduta hadi maini gate.😂😂😂
 
Jkt kanembwa madawili walikunya pembeni wote wakaambiwa wachukue mavi kwa kidole na kuyapaka kwenye ndoo.watoto wa mujibu wakishua sijui st kunani walilia hao😂😂
 
Nashauri Jeshi lifikirie umuhimu wa kutoa beji "Nishani" za JKT kwa kila "Operation" zilizopo na zilizopita ziuzwe au zitolewe bure kwa askari wote wa akiba,.... mujibu wa sheria na wa kujitolea waliohudhuria na kufuzu kwenye makambi yote ya JKT, Ili kwenye sherehe za kitaifa wale waliopo Duniani bado waweze kuning'iniza nishani zao. Nawasilisha!
Wazi Soja.
 
Sitasahau siku dawiri wa kombania yetu alipokamatwa pori akiliwa uroda na afande.. Yan tulikula doso si la kitoto hatukulala usiku wote na asubuhi mbio kama kawaida... Tulikunja ngumi... Mapenzi ya nyoka.. Kutembea kibatabata nk yaani usiku kucha na kadada kenyewe kapo kamelala maana kalikuwa kagonjwa ka pumu..
Mgonjwa wa kudumu aliwaponza
 
Wazalendo;

Moja ya sehemu ya maisha yangu ambayo kamwe sitasahu ni kupitia JKT.

Nilijiunga na JKT Ruvu na baadaye nikaenda Service Buhemba Lwamkoma.

Sitosahau kamwe mafunzo ya ukakamavu, kwata, mchaka mchaka, disko na vitimbi mbalimbali kati ya Makuruta na Maafande. Nilikuwa Combania E.

Moja ya vituko vya kukumbuka ni simulizi kutoka- Operation OKOA, kulikuwa na huyu jamaa alikuwa ni mweusi sana anaitwa afande Lucas, badala ya kuwaaamsha kuruta kwa filimbi, alikuwa anaingia na kuvuta Sigara. Kuruta inatakiwa ukisikia harufu ya Sigara uamke na kufoleni nje. Usipotoka in time unakula mijeledi.

Basi siku moja Kuruta wakapanga wamfanyizie na wakatoka mapema nje na kujificha huku ndani kwenye Bweni wakiyaviringisha mablanketi mithili ya mtu amelala. Afande alipomaliza sigara hakuna aliyetoka akajua siku hiyo kuruta wamegoma kuamka na kuanza kuchapa viboko yale mablanketi yaliyovingirishwa. Alishtukia kaanza kushambuliwa yeye na kuruta toka nje ambao walikuwa na fimbo kibao mpaka akakoma.

Kisha kuruta wakafoleni nje. Nakumbuka Mkuu wa Kombania alipata habari na kulikuwa na drill si kawaida na mpaka push ups za kunusa mkojo katika nyasi walizokuwa wanakojoa kuruta usiku. Hata hivyo yule afande naye alikoma kwani hakurudia mchezo wa kuwaamsha watu kwa sigara.

Kwa waliokuwa Ruvu Operation Okoa:

Na miss

  • Ugali na korosho mnapojongo kambini
  • Mihogo ya Vibwende kwa Babu
  • Wali na Maembe
  • Uji wa Mestin ya Jeshi
  • Bukta na Green Vest
  • Kuokota kuni
  • Bustani
  • Michezo
  • Disco
... Ama Johnnnnn ambaaaa ambaaa John, amba Johnnn wa Tanzania. Arusha Mbali, Arusha Mbali, tukumbukane kwa Barua nk...

Nakumbuka pia siku moja sikuimbisha disco vizuri na kipindi kile 1985 bado kulikuwa kuna ubaguzi wa rangi Africa Kusini, basi afande akanipiga mkwala na kuniambia.

"Kuruta nitakutemea mate yenye sumu usoni upofuke macho, na sijui utatibiwa wapi kwani mipaka yote Afrika Kusini imefungwa. . . (Kana kwamba hakukuwa na hospitali ya kutibu mate ya sumu hapa bongo"

Jamani mliokosa JKT, mlikosa mengi, japo tulipata tabu lakini tulijifunza mengi katika maisha.

Je, wewe unakumbuka nini?
Nimekumbuka msange Tabora OP Kikwete 2015, E coy chini ya OC Jomo, na Sir major Mudo, kuna siku tulikuwa tunapanga tanuru ile tunamaliza akapita luteni mmoja hivi jina limenitoka akatwambia hilo eneo tulilo panga Tanuri hapatakiwi kuchomea hapo tofari kwahiyo tupangue tuhamishe tofari na tupange upya, alafu hapo jua limewaka balaa niliishiwa nguvu nakujilaani, ila nilivyozoea mazingira nikaanza kudoji, maisha ya Msange vyoo hakuna tunajisaidia kwenye shamba la mahindi, nilivyoona shida zinazidi nikajiunga ngoma COY huko nikuimba tu na kukata mauno na wagonjwa wa kudumu nimemic sana Mesi kwa afande Mafleta, maisha ya JKT yalinijenga naweza kuishi sehemu yoyote iwe mjini au kijijini
 
Umenikumbusha mbali sana mie niliudhuria ile miaka ya mwishoni ya themanini (1989/90) Pale kambi ya Ruvu kombania ya B kuna afande alikuwa anaitwa Nyundo. Huyu afande hatukubahatika kumuona akiwa amefurahi kila siku sura yake ili kuwa ya kazi kazi.

Mwenyewe alikuwa anajiita ndio handsome wa kwao. Nakumbuka moja ya wimbo ambao alitufundisha muda wa disco ulikuwa wa Malela.... na mwingine ulikuwa nadhani wa kishona kama sijakosea unaitwa Kule kule kwa chinoma....
Kitu kingine nakumbuka ni ufugaji wa kuku kule phase 2 pamoja na kusimamisha minazi serengeti muda wa jioni.
Operation orjolo?au
 
Duuh aseeh inabidi tuheshimiane humu mtu mwaka 70 kamaliza form six [emoji23] [emoji23]. Mimi nimeshajitoa kuwa na heshima ya hali ya JUU humu tupo na baba zetu.
Dah asee... Nimekoma kujiita babu. ***** zangu sana mimi
 
[emoji743]🆄🅻[emoji745]🅼[emoji743][emoji743][emoji745]🅻[emoji742] 🆈[emoji742] 🅳🅴🅼[emoji745]
 
Nilikua chalii wa C coy alafu nilikua doja laana
Siku moja nilidoji nikakimbizwa na fande alafu kama jini vile nikapotelea chooni, yani namaanisha niliingia chooni alaf sijatoka afande nae akaingia kanitafuta bila kuniona

Jiulize nilijificha wapi? Nikiingia kwenye pipa la maji ya chooni alaf pipa lenyewe limejaaa maji full nilikua naibuka kidogo juu navuta hewa sekunde mbili alaf narud nazama ndani ya pipa dakika 4

Madoja wenzangu huko nje walipigwa tifu laana walikwepa ndege masaa 8
Kukwepa ndege huku umebeba gogo ndo balaaa[emoji2][emoji2][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
OP Kikwete MGAMBO Jk 832 daah dada wili si akamchoma private kuwa anamtaka alafu alikuwa mtoto wa Mkubwa balaa yani yule Private alipiga magoti mbele ya Kurutu 2000 anamuomba yule binti msamaha alafu demu mwenyewe Mbovuu kinomaa Maafande walitukana balaa yani achaa tuu.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Jamani baada ya lile tukio Tulikulaaa kazi yanii mateso yale hapanaa ikawa kama Course ya Kadet mamaee week 6 zilikuwa Chungu mnoo kuna siku tulilazwa kwenye Mvua inanyeshaa dadekii kesho yake nikasema wakirudia tena natorokaa yanii napiga mguu kwa mguu mpaka niipate lami...[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ilaa baadae nikaja kuwa doja balaa wakagawa vitengo picha linaanza nikakimbilia Upishiii...baadae nikawa nadoji msituni tu sieleweki nipo wapi then nikajiunga Ngoma Coy kwa wazalendo nilikuwa nalala kuanzia asubuhi mpaka jionii naamka kulaa tuu. Nilirudi jeshi shavu hilooo mpaka nikatamani kubaki yani wakanipa na 150k ya nauli enzi hizo za JK mambo safii.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
mafinga JKT 1988/89 (program ya chama) Mkuu wa kikosi aliitwa kanali Mlay, we! hatareee ya danger weka mbali na watoto!
Alikuwa akiogopewa na kila mtu hadi askari wenzake, bora ukutane na kifutu kule idetero au dubliganga kuliko ukutanae nae.🙄
D-Coy alikuwepo mtu anaitwa nusu mungu, aliwahi kumpa adhabu binti mmoja kuruta ya kumwangalia usoni, alilia hadi alijikojolea😀
 
OP Kikwete MGAMBO Jk 832 daah dada wili si akamchoma private kuwa anamtaka alafu alikuwa mtoto wa Mkubwa balaa yani yule Private alipiga magoti mbele ya Kurutu 2000 anamuomba yule binti msamaha alafu demu mwenyewe Mbovuu kinomaa Maafande walitukana balaa yani achaa tuu.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Jamani baada ya lile tukio Tulikulaaa kazi yanii mateso yale hapanaa ikawa kama Course ya Kadet mamaee week 6 zilikuwa Chungu mnoo kuna siku tulilazwa kwenye Mvua inanyeshaa dadekii kesho yake nikasema wakirudia tena natorokaa yanii napiga mguu kwa mguu mpaka niipate lami...[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ilaa baadae nikaja kuwa doja balaa wakagawa vitengo picha linaanza nikakimbilia Upishiii...baadae nikawa nadoji msituni tu sieleweki nipo wapi then nikajiunga Ngoma Coy kwa wazalendo nilikuwa nalala kuanzia asubuhi mpaka jionii naamka kulaa tuu. Nilirudi jeshi shavu hilooo mpaka nikatamani kubaki yani wakanipa na 150k ya nauli enzi hizo za JK mambo safii.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji16][emoji16][emoji16]huyu afande alipata aibu!
 
Back
Top Bottom