Je, unakumbuka "Scaba-Scuba, Scaba Line", basi dogo lililokuwa ikifanya safari zake Dar es Salaam - Morogoro?

Shkuba hayo majina mbona yana element za utapeli? Si ndio huyo aliyekuwa anauza Ngada? Scuba na magari wapi na wapi? Scuba si Hardware na Fremu tu?
Walianza siku nyingi hawa watu.
 
Nyingine zilikuwa Pop Juice, Master Top nk. Hizi zilikuwa zinapaki Magomeni Mapipa opposite CRDB Morogoro Road.

Nyingi zilikuwa ni Coaster za 3B engine ndo zikafuata Coaster Box Body.
El Sakaran ilipata ajali mbaya mno maeneo ya Mwidu 1991 au 2
The big mayai
 
Yeah, kituo kilikuwa Mapipa hiyo CRDB hata siifahamu. Mimi ni mmoja wa tuliomiliki hizo gari. 3B ni engine tu bro, gari model kwa coaster ni BB 10 na 11(waliita dungu), BB20, 21, 30, 31(double coaster)
 
Nyingine zilikuwa Pop Juice, Master Top nk. Hizi zilikuwa zinapaki Magomeni Mapipa opposite CRDB Morogoro Road.

Nyingi zilikuwa ni Coaster za 3B engine ndo zikafuata Coaster Box Body.
El Sakaran ilipata ajali mbaya mno maeneo ya Mwidu 1991 au 2
Ndio ni 1991 uso kwa uso na Scania ya Wade Adams. Siku kabla ya ajali tumezungusha trip za kutosha mimi nikiwa napiga ya tatu kurudi moro usiku nikagonga maeneo ya Pingo, kesho yake niko Chalinze natengeneza gari ndio habari za ajali ya Sakran.
 
Ilihuzunisha sana.

Nikumbushe vizuri, hivi ni ile ajali waliogongana nje ya barabara kwa kuwa maamuzi ya madereva yalifanana ya kupita nje (kushoto / kulia) ya gari (kicheche)!?
 
Hapana, Sakran alilala Moro na alopakia gari ya 2. Gari yake ilikuwa imeshachoka alikuwa hampi dereva anasukuma mwenyewe. Eneo la ajali wao wamepanda tokea Bwawani na Scania inashuka kwenye vilima vya mwidu huku ikiyumba (inasemekana dereva alipiga bia sana Mdaula ). Hivyo Sakran alipojaribu kumkwepa kwa kuhamia upande mwingine naye akarudi, gari iliburuzwa kaka kama mita 50
 
Hizi coaster zilikuwa zinatumika kama mpokezi wa abiria wa Treini mara nyingi tulikuwa tunashukia moro tunapanda hizo bus mpaka Dar. Stand ilikuwa Manzese msufuni. Humu ndani hawa watoto waliojazana humu hata hawajui.
 
Enzi hizo Morogoro ilikuwa hot kinoma,weekend vijana walikuwa wanaenda Mdebeni Moro,
 
Hizi coaster zilikuwa zinatumika kama mpokezi wa abiria wa Treini mara nyingi tulikuwa tunashukia moro tunapanda hizo bus mpaka Dar. Stand ilikuwa Manzese msufuni. Humu ndani hawa watoto waliojazana humu hata hawajui.
Kweli mkuu. Ila Manzese ilikuwa stendi ndogo. Zilikuwa zinatoka gari 2 zaidi 3 kwa siku.
 
Nimeikumbuka WAGALA! Pia kulikuwa na JACK CITY (Isuzu Journey)
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Enzo tamu

Tulikua na scholastica, yellow bus mwenge stesheni, jadide ubungo stesheni/posta, Tim mtoto,
 
Kulikuwa na easy come easy go
Dereva salum ujiko zilikuwa mbili hizi ingine dereva watanga konda marehemu tembo mtoto Isuzu journey za mzee bihonyi
 
Kulikuwa na easy come easy go
Dereva salum ujiko zilikuwa mbili hizi ingine dereva watanga konda marehemu tembo mtoto Isuzu journey za mzee bihonyi
Yaani mengi tu. Kriss Kross pia nimeikumbuka GoGuGu Line, journey L ya shule ya viziwi pale Kariakoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…