Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
View attachment 342896
PICHA: Mnyama Nyegere
View attachment 342897
PICHA: Mtu aliyedhuriwa na mnyama NyegereView attachment 342899
PICHA: Nyegere akipambana na Simba
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea
Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike
Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism" yake.
Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.
Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi.
Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...
Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
ZAIDI TAZAMA HAPA
===
MICHANGO YA WADAU KUHUSU MNYAMA HUYU
---
---
---
---
---
Aisee nimelazimika kutafuta maelezo jf baada ya Jamaa kutusimulia.kikiweni kwamba alibamiwa na huyu mnyama akiwa porini shamba kwake walikuwa wawili wakaja wakawa wanataka kumshambulia nyama za miguuni.
Njia gani unaweza tumia kumuua au kupambana nae? May be uwe na kitu kinachoweza kuwasha moto Kwa harakaHahahahaa naangaliaga sana video za huyu jamaa, ni mtata balaa na unaambiwa ana kumbu kumbu kwa hali ya juu sana! Huna cha kumdanganya! Anaitwa Honey Barger kwa Kidhungu ni habari nyingine kabisa huyo.
HujaelewekaMsiombe kukutana na Nyegele hafai hafai hata kidogo, Kuna Jamaa uliumizwa na huyo mdudu, alipona baada ya kukutana sisi akauwawa, nakumbuka alikufa kwa fimbo ya mti mbaazi, coz alipigwa sana lakni kufa ikawa ngumu, kuna mzee akaja akasema itafutwe fimbo ya mti wa mbaaz iliyokauka ndo apigiwe, na baada ya kumtindika na iyo fimbo akafa kilain sana
Maelezo Yako yamenifanya nigundue kitu na nikubaliane na Jamaa aliyetusimulia jinsi vilimvamia nhakujaua ni mnyama gani navyo vilikuwa vinafuata Kujaribu kumh'ata miguuni.Ni kweli kabisa mimi kuna siku aliwahi kuingia nyumbani usiku kufuata kuku mimi sikujua huyo ni nyegere nilichukua mpini mfupi na kupambana naye kila alipokuja miguuni kunifuata nilikuwa nampiga kichwani nilicheza naye kama dakika 20 nikafanikiwa kumuua nikamfunga kamba shingoni na kumtupa nje ya nyumba wala sikujua nimeua mnyama gani mpaka kesho yake asubuhi walipopita wapita njia ndiyo wakasema ni nyegere hapo ndipo nikapata uonga kumbe nilipambana na mnyama hatari hivyo lakini nikagundua uonga saa nyingine hufanya mtu asiwe na ujasiri kwani pengine ningekuwa nimejua tangu awali kuwa nyegere kaingia ndani pengine ningeshikwa na woga hivyo mnyama huyo angenidhuru
Kwa staili yake hii ya kushambulia au kulenga sehemu Moja unaweza pambana nae kama una kimti kikubwa au rungu na hiyo tabia ya ubishi ,kujiamini na kiburi nako katafika mahala kanachoka Kwa kipigo Cha mti.Daaah mkuu maalon basi ulikaotea sana haka kajamaa,haka huwa akakubali kushindwa,ni king'ang'anizi sana huyu mdudu...Ama hakika ulikuwa shujaa,vinginevyo kangekuondolea serikali yako yoooote bila huruma,maana kenyewe huwa kanavizia hukohuko "ikulu" kubwa
Hii ni kiboko ya kitu chochote ila Sasa kifaa gani potable kinakuwa na moto mda wote kuweza kuutumia kirahisi au kutembea nao unapokuwa porini kikazi au shambani?dawa yake moto,hataweza kujidefence kwakukakamaa
🤣🤣 Hii Sasa balaa kwamba anafungua kitasaPia ni mmoja kati ya wanyama wenye akili sana kiasi kwamba ana uwezo wa kujifunza maarifa mapya kwa muda mfupi sana na akayatumia kutatua tatizo lililojitokeza ghafla. Mfano mzuri ni kuwa,anao uwezo wa kupanda ukuta mrefu kwa kuegemeza ubao au gogo, mawe n.k Ana uwezo wa kusogeza kitasa cha geti na kulifungua. Na mambo mengi tu
Piga kichwa au mdomo sema Sasa ndio sio rahisi anakwepa ila huko kwingine utapig Hadi ukeshe yupo tuu 😆😆Huyu mdudu tuliwahi kutoboa nae usiku kucha porini.
Ilikuwa saa sita usiku akahamia nyumbani kwenye banda la kuku mbwa walishughulika nae walachoka bila kumuua.
Tukaamua kumshughulikia kwa fimbo na mikuki hatukufua dafu.
Kukimbia hawezi na akiamua vita harudi nyuma.
Tulimpiga sana mpaka sisi wenyewe tukachoka akawa hawezi kukimbia na sisi tumechoka kupiga tunamfuata tu akirudi kupambana anakutana na kipigo, anaendelea na safari.
Ilipofika saa 11 alfajiri kuna mwenzetu mmoja akawa amemsogelea sana na kajisahau mdudu akageuka ghafla jirani na miguu ya msela katika kugeuka kukimbia rungu lake alilirusha kinyume nyume likambahatisha puani akadondoka hapo hapo .
Tukachuna ngozi yake tukaondoka wakati tunamchuna ngozi kuna kipindi alikuwa akitikisika kama mzima vile tunatawayika.
Hata mzoga wake uliendelea kushtuka shtuka hivyo mpaka ulipooza.
Huyu mdudu ukikutana nae njiani hapishi njia kama ni umande lazima utaupiga tu labda uwe na gari.
Sent using Jamii Forums mobile app
Duu haka kadudu hakafai kabisa yaani bila kukaua hakamalizi timbwili full mapepo.Zamani umewahi kukutana na kibwana mdogo flani uwezo wa kukipiga unacho ila unaogopa timbwili lake?
Vipo vi bwana mdogo flani yaani unaweza piga halafu wewe ukachoka.kanakufuata tu kanakupiga na mawe,gogo,mchanga na kila kitu....yaani inabidi wewe ukimbie sasa.. basi ndo Nyegere.
Yaani Nyegere usije ukapumbazwa na jina lao maana hapo utawaza Nyege... Achana na hbr hizo. Hivi vinyama ni vibishi....acha. huwa vina mapepo flani hivi...ukikitibua hakikuangalii usoni. Ndo wale watu wanakwambia "nguse kama sijakuchana chana na viwembe"
Wanyama wana vifahamu hivi viumbe....we imajini vinakunywa sumu ya nyoka ndo kilevi chao...eeeehhh....usibishe.hata nyoka akikagonga...kanaanguka kama kamekufa ...halafu ghafla kanainuka kuliendeleza chezo.kakimuua kanamnyonya mate....kanalewa.kanaalala kakikoroma.
Sasa jichanganye kukaamsha... Utajuta.Ukikosana na Nyegere atakufuata popote uendapo.... Yaani kama utapanda gari ukamwacha atakuja tu akifuata barabara na kuulizia njian... Washkaji mliona gari flani imepita hapa.... Mpaka katafika kwako.
Yaani Nyegere anaweza kukuma mguu halafu asiuachie. Ukapiga mpaka wewe ukakaribia kufa kwa kuchoka. Unaweza ukakachoma choma na kisu kakang'ang'ania tu mguu huku kanavuja damu kinoma.yaani ni vibishi.
Ukikuta kimemgomea simba kupisha njia ndo utacheka.kanagoma kabisa na wala hakakwepeshi macho...sasa simba huwa wanaelewa kuwa hiki kibwana mdogo ikatokea tu kimeshika sehemu ndo basi.hakiachii. mwishowe simba huwa anasema ....dogo we jifanye kukomaa kuna siku ntakiwasha hapa tuonane wabaya" basi utasikia "usintishe wala nini...hayo manyama tu hata kwenye sambusa yapo" simba hapo anajifanya hajasikia anaondoka.
Sasa shida kubwa ya hivi vimnyama. Wewe huwa unasema xxxxx ana wivu sana....siwezi ishi naye nmechoka.huyo hana wivu. Nyegere ana wivu bwana. Ana wivu balaaa. Hafai.
Akiwa anatembea na mkewe yeye anakuwa nyuma analinda uchi wa mkewe. Ikatokea hata jani likagusa tu. ..asalaleeee....balaa lake.katalichana chana jani kinyama na kulifakilia mbali.kakiamini jani limefaidi utamu wake. Yaani kana wivu haka kamnyama acha. Hapo mkewe atasema 'baba ukwaju...yaani jani kugusa tu inakuwa issue..?twende bwana" kanajibu huku kametuna kanahema.
" Na wewe usinchanganye saahizi ntakuchenjia..." Hapo wife anajua itakuwa issue basi ili wafike salama anakikisha sehemu zake za siri haziguswi na jani lolote njiani.
Hawa wanyama wanapenda asali kinyama.... Unajua vinakula wanyama na wadudu wa ajabu halafu vinashushia na juice ya sumu ya nyoka. Sasa usiombe vikajamba ..unaweza kukufa hapo hapo kama afya yako haina amani...yaani ina mgogoro.
Basi huwa vinaenda ilipo asali...vinatoa gesi kwa nyuma (ashakum si matusi, vinajamba) hapo nyuki ule ukali wao huwa si kitu.. wanalewa wanalala. Kanaenda kuchukua asali.kanakula mpaka kabavimbiwa.
Na wakati mwingine vinaweza kutoa harufu flani kali sana ya kukwaza matakoni kukera tu wapita njia...ni tukorofi sana hutu tumnyama. Yaani bora uende ukawachokoze fisi walioketi wanapiga stories kuliko kuanzisha beef na haka kamnyama.
Huwa hakasamehi. Unaweza ukatibuana nako leo ila baada ya miaka miwli ukikutana nako hakakuulizi kuwa why siku ile ulinifanyia hivi?kanalianzisha upyaaaa.
Wanyama wengi hupenda kutengeneza amani nako sababu wanajua.kabishi kinyama.katukutu,kakorofi na hakaambiliki.
Huyo ndo Nyegere. Kaa mbali naye ukienda porini...anaweza kukufuata hadi kwako.na kama upo ndani kanakusubiria mlangoni....ni kama kanakuwa kanakudai hivi ....