Je, unamfahamu ngekewa?

Je, unamfahamu ngekewa?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Uliwahi kusikia kuhusiana na ngekewa? Basi leo nataka nikufumbue ufahamu vizuri. Ngekewa ni mnyama aishie porini moja ya tabia zake kuu ni kupendwa na wanyama wenzie. Anapokaa ngekewa hukaa na kila aina ya wanyama na ndege na hawamdhuru. Kwa maana hiyo ngekewa ni mnyama ambaye anapendwa na kila mnyama alie mbugani.

Hali hii inasababisha vitu vyake kutumika kutengenezea dawa za mivuto na waganga. Mnyama huyu hupatikana kwa msimu na kumuona kwake ujue una bahati sana anaishi kwenye majani marefu kandokando mwa mito au maziwa makubwa.

Mara nyingi mnyama huyu anapotembea hufuatwa na wanyama wengine nyuma. Mkia wake hutumika kutengeneza dawa kwa watu wanaohitaji wafuasi mfano wasanii, wanasiasa wanaofanya kazi za kutembea na kuongea mbele za watu.

Kiufupi mnyama huyu hutengenezewa dawa nyingi za kuvuta wapenzi kuvuta mali nk Anapokanyaga mnyama huyu na wewe ukakanyaga kama kazi zako ni za kusafiri utapata safari mpaka utazichoka Ukichukua majani aliyelalia mnyama huyu ukayaanika ukamuwekea mtu sehemu anapolala au kwenye maji ya kuoga kitakachotokea huyo mtu atakuwa hana kauli kwako iwe bosi mpenzi nk.

Nimejitahidi kuelezea navyoelezeka

FB_IMG_1666273637538.jpg
 
Capybara analiwa vizuri tu na Puma, Jaguar, na ile mijoka mikubwa.

Capybara wanapatikana South America tu, Mganga wa Sumbawanga au Handeni akikwambia ana ngozi ya ngekewa possibly anakudanganya tu, hakuna mnyama Ngekewa Africa.
 
Na wataalam wanadai huwa anatoa harufu nzuri inayowavutia wanyama wengine..ila habari ya mganga na NGEKEWA!!!! Labda mganga na KIPUKULA
 
Back
Top Bottom