Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Kazi yangu hapa shamba.. Dah sijui nimepatia hii kazi ila ndio kukomaa kiakili ya kilimo. Mkuu kilimo nipe maoni mkuu. Leo namalizia kazi hapa. Nimejaribu kuweka mistari miwili katika tuta moja.
 
Attachments

  • IMG-20160202-WA0006.jpg
    114 KB · Views: 102
  • IMG-20160202-WA0005.jpg
    141.8 KB · Views: 96
  • IMG-20160202-WA0003.jpg
    98.1 KB · Views: 95
Dah Asante kwa kunipa moyo. Zig zag bwana zikuinote kwenye uzi.. Nadhani nilipitiwa.. Ila nikaja kuikuta kwenye pdf.. Kiukweli sijaweka ya kuplan zipo zilizokaa ila zilijipatia tu. Dah so effect yake itakuwa nini mkuu
 
Noted mkuu. Nimeshazinunua nilitaka nizitumie baadae ila ngoja zifanye hiyo kazi. Nashukuru kwa moyo usiochoka kunipatia elimu hii ambayo vyuo vichache vinaitoa.. Thanx sana bro
 
Effect yake ni kuwa Canopy ikiwa kubwa sana zitakutana katikatika na ufanyaji usafi au upigaji dawa utakuwa mgumu kidogo kuna zingine zitakatika wakati mtu atakapokuwa anapita aiza kupiga dawa, au kuweka mbolea etc
Dah.. Hapo kazi itakuwepo. Anyway ngoja tuone tutapambanaje. Nashukuru kaka
 
mkuu kuna tatizo nimekutana nalo kwenye matikiti, mmea unakua njano, ila ni kuanzia kwenye ncha, majani yaliyoathirika hayafi, yanaonekana mazuri tu ila yanakosa kijani, majani yanayoathirika sana ni yale ya kwenye ncha, na tatizo limeenea kwa kasi sana sio shamba moja, mashamba mengine yapo umbali wa km7 kutoka nilipo ila nayo yameatirika..
 
Kazi yangu hapa shamba.. Dah sijui nimepatia hii kazi ila ndio kukomaa kiakili ya kilimo. Mkuu kilimo nipe maoni mkuu. Leo namalizia kazi hapa. Nimejaribu kuweka mistari miwili katika tuta moja.
hii ndio spirit chayowa, umepata elimu ukaingia shamba fasta
 
mbona kwenye vitunguu bei inakua na variation kubwa hivyo, tanga ni 90,000 halafu kariakoo ni 240,000? na umbali kutoka tanga na dar wala sio mbali kiasi hicho, au ndio wa tz tumeshindwa kuleta ufanisi kwenye uchumi?
 
Usimamizi wa mazao masokoni si mzuri, Madalali wanapanga bei wanavyotaka (Wao ndio huamua bei leo iweje) ndio maana wakulima wa chini wanabaki chini kila siku, dalali anapata faida mara 2 ya aliyelima.

mbona kwenye vitunguu bei inakua na variation kubwa hivyo, tanga ni 90,000 halafu kariakoo ni 240,000? na umbali kutoka tanga na dar wala sio mbali kiasi hicho, au ndio wa tz tumeshindwa kuleta ufanisi kwenye uchumi?
 
Habari ndugu. Hapa kahe kuna vipepeo wengi wameibuka. Vipepeo wa kawaida tu. Bado sijaona effect kwenye miche shambani. Je wanaweza leta matatizo shambani.
Mkuu Yara miller winner 15-9-20 inafaa kukuzia?
Leo nimefanya mahesabu ya makadirio.. Shamba lina matuta 136 ambayo yameingia mashimo 163 hivi kila tuta. Kwa maana hiyo kwa hesabu za haraka nimefanikiwa kutoa takribani miche 22,168 kutoka kwenye zile gram 60 za eden. Na bado kuna miche midogo midogo kadhaa iliyobaki kitaluni ambayo naitunza kuzima magap yatakayojitokeza.

Wasalaam
 
Mkuu maarifa habari za siku nyingi. Nahitaj kujua aina gani ya nyanya inayofaa kwa kilimo cha greenhouse kwa hali ya hewa ya Dar es salaam.
 
Kwa Green House best mbegu (kwa maoni yangu) List ni hii 1. Anna F1 2. Colazon 3. Eva 3. Gallilea 4.Eden 5. Monica 6. Shanty
etc..
....
Shukrani mkuu swali la nyongeza nahitaj kupuliza dawa kwenye greenhouse ili kuondoa aina yoyote ya contamination nitumie aina ipi ya dawa? ingekuwa vyema kama utanitajia jina la dawa na mahala inapopatikana.
 
Endela kuobserve hiyo effect ya hao vipepeo maana inaweza kuwa source ya Leaf Miner (Chora chora wa majani)

All the best Mkuu,Na kuwa makini kwa kila hatua maana umeinvest pesa zako
Nashukuru mkuu. Mbolea ya Yara miller winner 15-9-20 itafaa kukuzia kabla ya nitrable? Na je nikitaka kupuliza booster ni lazma niwe nimemwagilia maji kwanza
 
CHECK UREA KWANZA KWA UKUAJI WA HARAKA, UKIKOSA TUMIA HIYO YARA MILLER AU NPK YOYOTE YENYE N-KUBWA (NAMBA KUBWA YA KWANZA IWE KUBWA KULIKO ZOTE). WAKATI WA KUWEKA DAWA AU MBOLEA AU CHOCHOTE CHA KUPULIZA DHIDI YA MMEA NI MUHIMU UDONGO UKAWA UMELOWA.

Nashukuru mkuu. Mbolea ya Yara miller winner 15-9-20 itafaa kukuzia kabla ya nitrable? Na je nikitaka kupuliza booster ni lazma niwe nimemwagilia maji kwanza
 
TAFUTA DAWA INAITWA NIMBECIDINE INATENGENZWA NA KAMPUNI YA OSHO-SIJUI OFIS ZAO . INASAIDIA KUONDOA NEMATODES ETC. TAFUTA PIA AGRICULTURE LIME KUSAIDIA KUONDOA MATATIZO YA MNYAUKO (WILT).
Agricultural lime Ina content gani na ninaweza kuipata wapi?

Better stand alone and remain firm
 
CHECK UREA KWANZA KWA UKUAJI WA HARAKA, UKIKOSA TUMIA HIYO YARA MILLER AU NPK YOYOTE YENYE N-KUBWA (NAMBA KUBWA YA KWANZA IWE KUBWA KULIKO ZOTE). WAKATI WA KUWEKA DAWA AU MBOLEA AU CHOCHOTE CHA KUPULIZA DHIDI YA MMEA NI MUHIMU UDONGO UKAWA UMELOWA.
Sawa sawa mkuu
 
Mkuu kuna mbolea wanaitangaza sana wafanya biashara wa mitandao sijawahi pata ushuhuda was ufanyaji kazi wake. Inaitwa super agro. Je ni sawa na Busta za kawaida wakina polyfeed au nayo ina mambo yake?
 
Nashukuru mkuu
 
naomba kuuliza,nimepita kwenye duka la dawa za kilimo kununua dawa ya ukungu, nimezoea kununug ridomil gold kg 1 kwa sh 44,000 elfu nikaambiwa ipo na ivory kg 1 inauzwa sh 28,000 je utofauti huu wa bei unatokana na ubora wa dawa au nini? asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…