Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa


mkuu tatizo mitaji na pembejeo na vyanzo vya maji ya umwagiliaji mbogamboga
 
kirusoo


MKUU MITAJI INABIDI KUJIPANGA KWA KWELI, MAANA KILIMO KINAHITAJI PESA. BILA HIVYO UTAFANYA KILIMO CHA KUBAHATISHA KIONGOZI... NA MABENKI HAYA SI RAFIKI SANA HASA KWA SISI WATU WA CHINI.


mkuu tatizo mitaji na pembejeo na vyanzo vya maji ya umwagiliaji mbogamboga
 
kirusoo


MKUU MITAJI INABIDI KUJIPANGA KWA KWELI, MAANA KILIMO KINAHITAJI PESA. BILA HIVYO UTAFANYA KILIMO CHA KUBAHATISHA KIONGOZI... NA MABENKI HAYA SI RAFIKI SANA HASA KWA SISI WATU WA CHINI.
inamaana wengi wanaofanya kilimo cha kisasa wanakazi nyingine
 

mkuu mimtaji wangu hauzidi milioni ntaweza wapi zaidi ya kuanza na kilimo cha mvua
 
Uzi mzuri sana , Asante sana nitaufanyia kazi
 
Asante sana kwa msaada wako mkubwa na moyo wa kuwasaidia wengine kupata elimu ambayo tukiifanyia kazi inaweza kutusogeza mbele kimaendeleo. Asante sana na jumapili njema.
 
JEMEDARI .H.

POLYFEED FINISHER (NI AINA YA KUNDI LA FINISHER BOOSTER-BOOSTER YA KUMALIZIA HUPIGWA WAKATI WA MATUNDA)

NI BOOSTER YENYE POTASSIUM KWA WINGI (K) PAMOJA NA MICRO ELEMENTS, AMBAZO HUSAIDI TUNDA KUKOMAA KWA WAKATI, KUZUIA TUNDA KUNYAUKA LIKIWA MTINI, KUZUA TUNDA LISINDONDOKE ( FRUIT ABORTION), NA PIA HUSAIDIA TUNDA KUWA NA AROMA (TEST/RADHA) NZURI ZAIDI.


Mkuu Nini Kazi Ya Polyfeed Finisher?
 

Nimepanda tikiti black diamond water melon, mmea una mwezi na siku kadhaa inshalah naendelea vema.
 
Mungu akupe uhai mrefu tuzid kupata maarifa zaid ongera kwa kipaji ulichonacho na elimu yako

Tutafika kule tunapopataka kupitia hii elimu yako
 
Naomba msaada,nimegundua miche yangu ya nyanya kitaluni inakatwa na nimefukua chini ya ardhi nimeona wale wadudu ambao huwa wanakata mashina ya viazi au mboga zikiwa bado changa, je huyo mdudu anaweza kuwa kanitangaze?

Kwa sababu miche mingi imekatwa nataka ninunue mbegu ili kusia mingine ili iweze kutosheleza eka 1 kwani mara ya kwanza nilinunua gram 30,naomba kuuliza je hiyo miche nitakayosia sasa nyanya yake itatoka bei ikiwa bado nzuri?

Bei ya nyanya hushuka soko lake hasa mwezi wa ngapi? Je nikipiga polyfeed starter miche ikiwa bado kitaluni itaathiri chochote nitakapoihamishia shambani? Asante.
 
Mkuu Naomba Kufahamu Hizi Nyanya Za Hybrid Kipato F1 Zinavunwa Kwa Muda Gani Kwenye Open Space Na Je Nikishaanza Kuchuma Kwa Mara Ya Kwanza Nizifanyaje Ili Zidumu Kwa Muda Mrefu Na Nichume Mara Nyingi Zaidi?
 
Wanaouza Na Kusambaza Mbegu Za Kipato F1 East West International Wameniambia Inavunwa Miezi 6 Sijui Ukweli Wake.
 
Mkuu kwema....nimewatika vitunguu ni wk ya nane sasa aina ya red creole lakin havinenep na kurefuka kufikia kuingizwa shamban.....eneo ni igawa na nilipandia DAP.....NA MAJANI YALIONYESHA DALILI YA KUNYAUKA KWENYE TIP NIKAPIGA TANKOPA.....NAOMBA USHAURI NIFANYEJE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…