Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Tunaweza kupata mawasiliano tafadhali?#kilimomaarifa.utajiri
 
kilimomaarifa.tajiri sikupiga dawa ya kinga ya kantangaze miche ilipokuwa kwenye kitalu, sasa naweza kupiga dawa gani baada ya kupanda. Nimesoma option ulizotoa lakini nahisi zinanichanganya. Pia ni mbolea gani nzuri kwa migomba zaidi ya samadi? Asante
 
Last edited by a moderator:
je kuna ukweli kuwa ukikata maua au ukipunguza majani kwenye viazi mviringo vinavyokuwa eti unaongeza mavuno ,yaani kiazi kitakuwa na viazi vikubwa tofauti na ungeacha hivi bila kukata maua au kupunguza majani?
 
nilipandikiza nyanya na kuweka mashine iwe inamwagili , sasa kuna jirani kasema ukimwagilia nyanya kwa saa 24 au zaidi sehemu moja bila kuhamisha mashine unasababisha ziungue, mimi nilijua kuwa ndio zitaota vizuri,ulisema yara miller winner unaweza kupandia na kukuzia ,je mbolea ya dap nayo naweza kupandia viazi na nikakuzia? kwani nimeona mtu anakuzia dap kachanganya na can. Eti kuna parachichi zinazozaa mara mbili kwa mwaka? Asante sana.
 
Nimepandakiza miche 5000 ya nyanya aina ya eden ,je ikiota vizuri na kuhudumiwa vizuri naweza kupata kilo ngapi za nyanya mpaka mwisho wa mavuno.
 
NINA IMANI
WASTANI WA MAVUNO KWA EKA MOJA UNAPASWA USIKOSE KRETI (@40 KG) 400 NA KUENDELEA ILI UWEZE KURECOVER GHARAMA ZAKO, AMBAPO HATA BEI IKIFIKA TSH 10,000 KWA KRETI MOJA (BEI YA CHINI KABISAAA) BADO UTAPATA JUMLA YA MAVUNO YA TSH 4,00,000, NA GHARAMA ZAKO HATA ZIKIWA KUBWA VIPI HAZITAZIDI 3 MILIONI KWA EKA MOJA, HIVYO UTAPATA FAIDA YA TSH 1,000,000 KWA EKA . KILA LAKHERI
Nimepandakiza miche 5000 ya nyanya aina ya eden ,je ikiota vizuri na kuhudumiwa vizuri naweza kupata kilo ngapi za nyanya mpaka mwisho wa mavuno.
 
Asante sana, je dawa za ukungu na booster starter natakiwa kupiga kuanzia siku ya ngapi tangu kuipandikiza shambani
 
nina imani
- dawa za ukungu zinapigwa wakati wa unyevu ukiona ni msimu wa mvua kama sasa angalau kila baada ya siku 14 upige hizo dawa, ni vizuri ukaanza na hizo protective fungicides zenye copper kwa wingi kama tan copper, blue copper, etc hizi ni vizuri zikapigwa pale mvua zinapoanza tu kunyesha utazirudia tena kila baada ya siku 14, badae mvua zikiendelea kuchanganya unaendelea na hizo protective na curatives fungicides kama ridomil gold, au amistar xtra, au funguran, ebony 72 wp, ivory 72 etc etc. booster-hii inapigwa ndani ya siku 14 za kwanza tangu miche kupandikizwa, lengo ni kuchangamsha miche, pia huwa zinapigwa miche inapoanza kutengeneza vitumba vya maua

nashukuru sana
 
kilimomaarifa.tajiri hivi naweza kupiga dawa ya kinga ya kantangaze na kinga ya wadudu zote kwa wakati mmoja?
 
Last edited by a moderator:
Pia kwa ajili ya majani kusinyaa na kuwa njano kama picha ya jani uliyoweka nilipiga Grino 70WP na Dimethoate kwa ajili ya wadudu ni wiki sasa toka nipige lkn sioni badiliko lolote na nyanya nyingi zikiiva ndani zimeoza! Nirudie dawa au maoni yako ni yepi? Huu ugonjwa naona umesogea mpaka kny bustani ya spinach na chinese!
 
Dah nimepitia siku tatu huu UZI toka mwanzo mpaka mwisho hapa page ya 14 kwa umakini kabisa.

Aisee sijawahi kutana na UZI mtamu, wenye akili na unaokuelekeza direct hata kwa mkulima mdogo kabisa wa kule kijijini anaelewa.

Mkuu kilimomaarifautajiri salute kuu kwa mkono juu mwingine umenyooka chini. Nimechukua notes nyingi sana kwa ajili ya msaada.

Nikiwa na swali naliandika pembeni kwani nikiuliza itanipoteza ajabu nilivyozidi kusoma nikawa napata majibu na kujikuta nakata maswali.

Nililima nyanya riogrande mkulima tena kwa kuanza kwa mbwembwe sana pale kahe ekari 3. Shamba zilikuwa 2 moja ekari na robo nyingine mbili kasoro. Nililima kipindi cha January nikavuna March mwishoni.

Dah jamaa walikuwa wanakuja shamba kuchuma kreti moja la 40Kg lile niliuza kwa mara ya kwanza 45,000. Mwishoni niliuza 20,000.

Nilitumia milioni tano kasoro ikiwa ni jumla ya kila kitu, shamba, mashine mbili, mbegu, mbolea, Dawa, vitendea kazi na wafanyakazi.

Pamoja nakupata bei nzuri nilivuna kama kreti 60 tu mfano jumla zilinipa 2.1m pekee. Nyanya zilitafunwa na mdudu ambaye Sasa nimemjua ni kanitangaze kwani namtangaza Sasa.

Nimepitia kwa nguvu sana na kwa akili kwani narudi tena kahe msimu huu. Nafreka shamba Sasa na nataka kuandaa kitalu. Aisee nataka nilime kisasa zaidi. Huwa nanunua mbegu pale Moshi, nimepita maduka kadhaa nimeona wana kipato. Japo natafuta Eden.

Sasa swali langu tu hapa ni unanishauri pale kahe nipande ipi? Kipato inafanya vizuri au eden? Je Moshi duka gani linauza pembejeo za kilimo zilizo bora kama madawa, mbegu na kadhalika? Nakuuliza hivi kwani nimeona mahala umegusia kahe nikahisi unapaelewa vizuri.

Kwasasa napanda lile shamba la ekari mbili kasoro pekee baada ya kulipumzisha kwa Mwaka na miezi je kanitangaze bado atakuwa around?

Kuna sehemu umegusia kulima kwa kupandisha matuta kilimo kilicho bora kwa drip lines Sasa sikuelewa vizuri kwa umwagiliaji wa furrow niwekeje matuta? Nitamwagiliaje?

Kipindi kilichopita nilitumia majaluba kama ya mpunga ila sikupenda kwani hata shamba halipendezi.

Asante sana mkuu kwani kiukweli nililima nikiwa sina ujuzi. La mwisho mkuu tupatie namba tukupe walau kifurushi kwa roho nyeupe kabisa.

Umefanya kitu kikubwa hakina mfano wake.mtu anavyouliza unavyojibu Safi sana kaka, wala hujali kwamba ulishalijibu kabla.

Pamoja mkuu.
 
NEW, NEW, NEW, NEW.. TAREHE; 14 DISEMBA 2015.

SOMO LA NNE (4) . Denguwe/Kanitangaze/Tuta Absoluta

LEO TUTAJIFUNZA KWA KIFUPI KUHUSU MDUDU AITWAYE DENGUWE/KANITANGAZE/TUTA ABSOLUTA


KIASILI/KIHISTORIA
-Mdudu huyu alianzia peru miaka ya 1917
-Nchi za Bara la Amerika ya Kusini zimeathirika na mdudu huyu kwa miaka mingi
-Mwaka 2006 aligundulika hispania (Valencia)
-Mwaka 2007 aliingia Morocco
-Mwaka 2009 Alingia Uholanzi, Ureno, na Uingereza
Mwaka 2012 Aliingia Sudan. Ethiopia, Kenya, na Senegal
-Mwaka 2014 Aliingia nchini Tanzania


HUSHAMBAULIA
Mimea (Majani, na matunda) ya familia ya Solanaceae-Kama vile pilipili hoho, Nyanya, Viazi mviringo, Bilinganyi etc. MARA NYINGI HUPENDELEA ZAIDI NYANYA

? Solanum lycopersicum (tomato)
? Solanum tuberosum (potato)
? Solanum melongena (eggplant)
? Capsium annuum (pepper)
? Nicotiana tabacum (tobacco)
? Solanum nigrum
? Datura stramonium
? Solanum eleagnifolium
? Physalis peruviana


SIFA ZA MDUDU (Adult-Tuta Absoluta) /MZUNGUKO WA MAISHA.

-Mzunguko mzima wa maisha ya mdudu (yai -mdudu)ni siku 20 hadi 70
-Hutaga mayai juu ya mmea katika sehemu tofauti tofauti za mmea (katika majani, maua, na katika matunda), hutumia siku 3 hadi 9 kutaga mayai
-Baada ya hizo siku mayai hugeuka na kuwa Larvae
-Maisha ya larvae ni siku 11 hadi 37 siku
-Badae lavae hudondoka ardhini na kugeuka na kuwa pupa
-Pupa huishi kwa siku 6 hadi 24 na badae huwa mdudu kamili
-Mdudu mkuu (Adult) yuko na antena mbili
-Ana magamba ya rangi ya kaki, kijivu, au udongo
-Size ya ukubwa wa mwili ni urefu wa mm 10-12
-Ana mabawa
-Mazingira ya joto husaidia sana utagaji wa mayai
-Jike ni nene (umbo), kuliko dume
-Jike mmoja anaweza kutaga mayai 200 hadi 250 katika umri wote wa maisha yake
-Tuta Absoluta Jike huishi siku 10-15
-Tuta Absoluta Dume huishi siku 6-hadi 8

HASARA

-Usipochukua tahadhari mdudu huyu husababisha hasara kuanzia 80%-100% ya mavuno uliyotarajia.
-Mdudu huyu
ameshasabaisha hasara kubwa sana kwa wakulima wengi wa nchi hii


KUENEZA KWAKE NCHINI-TANZANIA

Mdudu huyu ameshaenea Zanzibar yote na kwa Tanzania bara zaidi ya mikoa 10 tayari imeshaingia katika hasara za mdudu huyu.

-Aliingia nchini mwaka 2014 akitokea Kenya, aliingilia 1.Arusha, badae akaingia 2.Kilimanjaro, 3.Tanga, 4.Morogoro akafika mwezi wa 6 mwaka 2014,yupo 5. Iringa tangu mwezi wa pili 2015, 6.Mbeya, 7.Mtwara, 8. Katavi, 9. Simiyu, 10.Mwanza

NJIA ZAKUENEA KWA MDUDU

Mdudu huyu mara nyingi sana huenezwa kutoka eneo moja kuja lingine kutokanana na vifaa vya shambani (Kama havikusafishwa vizuri)-hasa ile atua ya Kiwavi (Larva). Vifaa vya kusafirishia kama magari au makreti ya kubebea mazao, yakiwemo mazao yenyewe husika. Pia huenea kwa haraka zaidi kwa njia ya upepo (yule adult Tuta-Nondo), hutegemea upepo ili aweze kusafiri kutoka sehemu Moja hadi nyingine.

-KRETI za nyanya zinabebwa kutoka arusha zinaenda kwa gari hadi dar, badae gari hilohilo kreti zilezile zinaenda iringa etc kubeba nyanya pia, mzunguko ni mkubwa sana wa mdudu huyu..lazima Intervetion yake ihusishe wadau wote katika mnyororo wa thamani

JAMBO LA KUSIKITISHA

-Mdudu huyu yupo nchini sasa zaidi ya mwaka, na tayari wakulima maelfu wameshapata hasara 60-100% kwa sababu ya ugeni wao wa kutokujua nini cha kufanya dhidi ya mdudu huyu. WENGI WA WAKULIMA WAMEPATA HASARA WAMEPOTEZA MITAJI NA WENGINE WAMEKIMBIA MASHAMBA YAO.

-Mpaka sasa hakuna sera yoyote iliyotungwa na serikali zote (BARA/VISIWANI), HATA KUITISHA PRESS CONFERENCE TU YA KITAIFA NA KUMTANGAZA MDUDU HUYU KAMA NI JANGA LA KITAIFA IMESHINDIKANA.WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI NYINGI WANAJUA UWEPO WA MDUDU HUYU LAKINI HAKUNA HATUA STAHIKI ZILIZOCHUKULIWA ZINAZOLENGA KUMTHIBITI MDUDU HUYU.

-KUSEMA UKWELI, BILA NGUVU YA PAMOJA SERIKALI, NA WADAU WOOOTE WALIOPO KATIKA MNYORORO WA THAMANI WA NYANYA HAKUNA MAFANIKIO DHIDI YA MDUDU HUYU

-SHIDA KUBWA NI KWAMBA UELEWA WA WATU DHIDI YA MDUDU HUYU UKO CHINI SANA

MFANO WAPO WAKULIMA AMBAO WAKIKUTA NYANYA ZIMEHARIBIKA NA TUTA HUISHIA KUZITUPA TU, MASOKONI NI HIVYO HIVYO, MAHOTELINI NA MAJUMBANI NI HIVYO HIVYO PIA, WATU WANATUPA NYANYA HIZO AMBAZO TAYARI ZIKO NA VIWAZI (LARVA) VIWAVI HAO BADAE HUGEUKA KUWA BUU (PUPAE) NA BADAE NONDO (TUTA ABSOLUTA) TENA MAISHA YAKE YANAENDELEA ANATAGA MAYAI ETC

-MPAKA SASA KAMA TAIFA HATUNA HATA SERA (POLICY) /MKAKATI WA PAMOJA WA KITAIFA DHIDI YA MDUDU HUYU
-MZUNGUKO WA MDUDU HUYU NI MKUBWA SANA (NAAMINI HADI MWISHONI MWA MWAKA 2016 MDUDU HUYU ATAKUWA AMEMALIZA NCHI NZIMA)


Dawa kukinga Denguwe/Kanitangaze/Tuta Absoluta-HIZI NI BAADHI TU. DAWA HIZI NI VIZURI ZIKATUMIKA KUJIAHAMI (KUKINGA) MICHE IKIWA KITALUNI, AU MARA TU UNAPOKUWA UMEHAMISHIA MICHE SHAMBANI.

1. Match 500EC (Kiambata-Lufenuron)
2. Rimon 10EC (Novaluron)
3. Actra 25WG (Thiamethoxam)
4. Duduall etc
5. Buffalo 100EC

Dawa za kutibu Denguwe/Kanitangaze/Tuta Absoluta-HIZI NI BAADHI TU YA ZILIZOTHIBITISHWA TPRI

1.Evisect 50SP (Kimbata-Thiocyclam)

2. Ascotin 0.15EC/Nimbecidine (Kiambata-Azadirachtin-Mwarobaini)
3. Coragen SC (Kiambata-Chlorantraniliprole)
4. Avaunt 150 EC/ Mavuno 25EC (Kiambata-Indoxacarb)
5. Belt 480 SC (Kiambata-Flubendiamide)

Dawa no 3 (Coragen) na Dawa no 5 (Belt) Ili zifanye kazi vizuri ni vyema ukawa unazipiga kwa mzunguko, wiki hii unapiga belt, wiki ijayo unapiga coragen (ALTERNATION), Lengo kuu ni kupunguza uwezo wa mdudu kujenga usugu dhidi ya hizi dawa.

JAMBO LA MSINGI JITAHIDI KUJUA VAMBATA VILIVYOMO KATIKA HIZO DAWA, MAANA HAYO MAJINA YA DAWA (Ie Belt/ Evisect et al.. ) NI MAJINA YA KIBIASHARA TU HUBADILIKA MUDA WOWOTE


XXXXXXX NOTE, NOTE, NOTE, NOTE, NOTE.................XXXXXXXXXXXXXXXX

-Baadhi ya dawa 1. zenye kiambata cha Profenofos, dawa kama Wilcrom, Selecron, Agrocom, Supercron, Duducron, Bonaphos et al... ni dawa nzuri sana kumuangamiza mdudu Kanitangaze, LAKINI CHANGAMOTO YA DAWA HIZI ZENYE KIAMBATA CHA Profenofos BAADHI YA TAFITI, ZIMEONYESHA KUWA , Ziko na side effects kwa wadudu marafiki wa shamba na kwa wadudu wale wanaoweza kumla Tuta Absoluta

2. Dawa zenye kiambata cha
Chorpyrifos , dawa kama vile Dursban, Twigaphos, Subachio, Propyrifos et al, Ni dawa nzuri sana dhidi ya Tuta Absoluta lakini pia ziko na athari kwa wadudu marafiki.

3. Dawa zingine zenye athari kwa wadudu rafiki ni zile zenye kiambata cha
Dimethoate kama vile Dume, DDimate,Dimefarm,Digoz, Sume,Dud-ethoate

4. Zingine ni dawa zenye kiambata cha
Deltamethrin, dawa kma vile Decis, Decis Forte, Atom, Keshet, Modeci, nk


ATHARI ZA DENGUWE/KANITANGAZE/Tuta Absoluta katika zao la Nyanya

attachment.php

attachment.php


attachment.php





adult Tuta Absoluta

attachment.php


Larvae Tuta Abosluta
attachment.php


effects of Tuta on Leaves


attachment.php

attachment.php


Fruit affected with Tuta Absoluta

attachment.php




Tuta Absoluta Life Cycle
attachment.php

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Kwa jambo lolote niandikie
E-mail: kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx





AMANI YA BWANA IWE NANYI



Tarehe; 18/10/2015 Saa 12.00 JIONI

Leo tutajifunza Faida na Agronomy ya matunda yaitwayo Parachichi (Avocado)

SOMO LA TATU; ZAO LA PARACHICHI (AVOCADO)

avocado-sliced-in-half.jpg

Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili

1. Faida za Parachichi upande wa Lishe

-Tunda lina vitamini zifuatazo

1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri

2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve

3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa

4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili

5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi

6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu

Madini- (Mineral Elements)

Ni tunda lenye

1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi

2. Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili

3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili


2. Agronomy ya Parachichi

Hali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto

Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko

Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi

1. Zipo aina za kiasili
Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

images



-Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu


images




-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

UPandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo
-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,

-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO

-Parachichi hasa hizi za kisasa, huanza kuzaa baada ya miaka 3 na matunda yake hukomaa baada ya miezi 6 hadi 12. Tunda la aina ya HASS ndilo huchelewa zaidi kukomaa huchukua kati ya mizei 7 hadi 12 tangu lilipo jitengeneza katika mti.

MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi

Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda

1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni

5824734299_4940d330eb_o.jpg
2372468252_ea77e64362_z.jpg
Jani lililoshambuliwa na Alga

14991342145_8fb7f1fe14_z.jpg
5684201507_a9cb170821_z.jpg

Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda
Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia
15085900645_f4932bf337_z.jpg
-Tatizo la Athracnose husababishwa na Ukungu/Fangasi

Scab.jpg
-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

1390031-SMPT.jpg
1390032-SMPT.jpg

Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips


DAWA

-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

BEI

KUANZIA MWEZI WA 8 PARACHICI HUWA ADIMU SANA, NA KWA MAENEO YENYE MUINUKO WA MITA 1700, NDIO MUDA WA PARACHICHI AINA YA HAAS HUKOMAA, AMBAPO


KILO MOJA YA HAAS HUWA MATUNDA 3 HADI MATUNDA 5. DEBE MOJA LA KILO 20 HUWA NA MATUNDA 40 HADI 70 KUTEGEMEA NA UKUBWA.

KUANZIA HUO MWEZI WA SABA NA KUENDELEA DEBE MOJA LA PARACHICHI AINA YA HAAS HUANZIA TSH 15000 NA KUENDELEA

JUST IMAGINE

UNA EKA MOJA (1 ) TU YA PARACHICHI YA MITI 100 TU (MITI MICHACHE KABISA), NA KILA MTI UKUPE JAPO KILO HIZO 40 (DEBE 2), NA KILA DEBE 1 UUZE KWA TSH 15000 TU


MAHESABU

MICHE 100 X DEBE 2@ MCHE X 15,000TSH@DEBE 1= 3,000,000 TSH-MAPATO HASA HUPATIKANA BAADA YA MIAKA 3 NA KILA MWAKA MAVUNO HUONGEZEKA PARACHICHI ZENYE UMRI WA MIAKA 5, HUFIKIA KUTOA MAVUNO HADI YA DEBE 8 (KILO 160) KWA MMCHE MMOJA. JE KWA MICHE 100??

MAHESABU

MICHE 100 X DEBE 8 KWA KILA MMCHE MMOJA X TSH 15,000 KWA KILA DEBE 1=TSH 12,000,000

UMRI WA MAVUNO BORA KWA MMEA WA PARACHICHI NI MIAKA 40 HADI 50

Hitimisho

Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini


Masomo mengi zaidi kuhusu kilimo yatakuwa yanakujia kupitia hapa Jf na blog yetu ya
http://kilimomaarifatajiri.blogspot.com/ punde itakapo kamilika kuandaliwa



attachment.php


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx




AMANI YA BWANA IWE NANYI

9/10/2015; 10.45 jioni

kilimomaarifa.tajirinawakaribisheni katika ukurasa huu KADRI NITAKAVYOKUWA NIKIPATA WASAA (MUDA) ntakuwa nikitoa mada mbalimbali katika ukurasa huu ZIHUSUZO KILIMO CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo kilimo cha mboga mboga na matunda; (Ukipata wasaa waweza jifunza mengi zaidi kupitia blog hii http://kilimomaarifatajiri.blogspot.com/

SOMO LA PILI ;
KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.

Karibuni sanaa

Kwa leo ntajikita kueleza kwa kifupi sana na kwa lugha rahisi , KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.

1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI

-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k

Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.

BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).

Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi

-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE

i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-

Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.

Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida

ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.


2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)

Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.

Wasalaamu. mawasiliano. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

SOMO LA KWANZA; KILIMO CHA NYANYA

TAREHE; 20/09/2015 SAA 12. 49 JIONI



KARIBU


NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanaimuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..

WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA


DAWA ZA KUTUMIA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yle moth kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)


2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Arysta Life Science inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana


AGRONOMY YA NYANYA


AINA
Ziko nyingi kama fupi kiasi (Semi Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA

A; Semi-determinent


1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-


B; Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU


AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA


C; AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima


MAZINGIRA
i. Joto la kadri 20-35 degree sentigrade

ii. UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo


iii. NAFASI YA KUPANDA


-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapnada double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE


-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA


Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)


Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)


KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 30-50 kwa hybrid (F1) . Ghrama za kutosha eka moja kwa OPV variety ni tsh 100,000-180,000, na kwa Hybrid (F1) Gharama ni kati ya tsh 200,000-400,000 kutegemea na aina yenyewe ya mbegu.


UPANDAJI


Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowte utakao, na kisha chora vimefereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dodondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia mwaji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.


Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)


MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.


ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.


MAMBO YA KUFANYA SHAMBANI


Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung'oa miche, na sahamba mama pia liwe limemwagiwa vya kutosha


-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)


Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo paada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji


BAADA YA KUPANDIKIZA


Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani


Dawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao


Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, UREA, Yarra miller winner, au Hata NPK,


Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitumba vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) kama vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix


WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU


Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipingwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana sa 6 hadi sa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shape less


MATUNDA YAKIJA

Ni muhimu kuzungusha chini katika mizii mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking

WADUDU

Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)


Magonjwa


Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)


MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 120 HADI 150 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA


MAVUNO


Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 65


SOKO


Nyanya yenye bei nzuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000


Gharama za kuhudumu shamba la Nyanya kwa eka 1 ni takribani 2.5 hadi 3.5 Milioni ( Gharama kubwa ipo, katika mbegu hasa kama ni hybrid (F1), mbolea, maji (Pump), Vibarua (wakati wa kupanda na kupalilia) na madawa ya kuzuia wadudu na kutibu magonjwa.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

mkuu hivi nyanya kitaalamu inahitaji lita ngapi za maji kwa mche
 
minimum
mls 500 kwa mche 1 kwa siku 1 (mls 250-asubuhi, mls 250-jioni)

maximum
mls 1000= 1 litr kwa mche 1 kwa siku 1 (mls 500 -asubuhi, mls 500-jioni)

idadi ya mara ngapi uirrigate itategemea sana na aina ya udongo ulio nao, na hali ya hewa ya eneo lako.

mkuu nashukuru ,tatizo maji ni shida kwa hiyo nilitaka nijue kiasi cha maji mche mmoja unatumia kiasi gani ili ninue maji kwahiyo nikiwa na mche 2000 kila mmoja unatumia 500ml itakuwa ni : 2000x500=1000000ml sawa na lita 1000,lita 20 wanauza sh. 50 kwahiyo 50 x 59
= sh 2500 kwa siku x siku 100 =250000 si tupo pamoja mkuu ,Sasa kwa miche 2000 ntapata tani ngapi? je itanilipa?
 
chayowa


Kiongozi asante kwa kushukuru, Shukrani sana

Mkuu baraka ZIWE nyingi kwako na kwa kikazi chako hata milele. Kaswali kengine kameclic kichwani.

Nimepata elimu ya starter solution ambayo unachukua mbolea ya kupandia kiganja kimoja kikiwa kimenyooka na kuweka kwenye Lita 20 za maji zikiyeyuka tunaweka shimoni 250mls then ndio tunaotesha mmea.

Kwenye kuweka mbolea ya kukuzia kama urea au wakati wa matunda ile yenye calcium je naweza pia ichanganya na maji nikamwagia kama solution badala ya kupima na kuzungushia kwenye SHINA? Na je kama ni sawa nahapa napima 250mls pia?

Je unashaurije mkulima wa kawaida katika umwagiliaji pump zile za mafuta au moneymaker pumps hasa katika umwagiliaji wa matuta hayo? Nimeuliza kwani nahisi mmea utabaki bila udongo hapo kwani maji yakipita yatapita nao.

Na pia dizaini hii ya matuta nikitaka kufungia nyanya ile dizaini ya nguzo mbili imara halafu nyingine baada ya mita 2 nitazichomekaje kwa tuta mbili au nguzo moja moja na kushuka hivyo? Au wewe unashaurije mkuu?

Nakushukuru
 
Naomba kuuliza,je naweza panda parachichi kwa mbolea ya chumvi tu na baada ya mwaka nikaweka samadi? Nina taka kupanda mwezi wa kwanza ila nimekosa samadi.asante.
 
Asante sana mkuu ubarikiwe, dawa nimeshapiga naamini itasaidia.
 
nataka kulima sijui pakuanzia au zao gan litanilipa
 
Viazi mviringo kwa wastani vinatakiwa vipigwe booster mara ngapi mpaka kukomaa? Watu wanasema ukizidisha booster unasababisha viazi kuoza kuna ukweli. Asante.
 
Back
Top Bottom