Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimepandakiza miche 5000 ya nyanya aina ya eden ,je ikiota vizuri na kuhudumiwa vizuri naweza kupata kilo ngapi za nyanya mpaka mwisho wa mavuno.
nina imani
- dawa za ukungu zinapigwa wakati wa unyevu ukiona ni msimu wa mvua kama sasa angalau kila baada ya siku 14 upige hizo dawa, ni vizuri ukaanza na hizo protective fungicides zenye copper kwa wingi kama tan copper, blue copper, etc hizi ni vizuri zikapigwa pale mvua zinapoanza tu kunyesha utazirudia tena kila baada ya siku 14, badae mvua zikiendelea kuchanganya unaendelea na hizo protective na curatives fungicides kama ridomil gold, au amistar xtra, au funguran, ebony 72 wp, ivory 72 etc etc. booster-hii inapigwa ndani ya siku 14 za kwanza tangu miche kupandikizwa, lengo ni kuchangamsha miche, pia huwa zinapigwa miche inapoanza kutengeneza vitumba vya maua
NEW, NEW, NEW, NEW.. TAREHE; 14 DISEMBA 2015.
SOMO LA NNE (4) . Denguwe/Kanitangaze/Tuta Absoluta
LEO TUTAJIFUNZA KWA KIFUPI KUHUSU MDUDU AITWAYE DENGUWE/KANITANGAZE/TUTA ABSOLUTA
KIASILI/KIHISTORIA
-Mdudu huyu alianzia peru miaka ya 1917
-Nchi za Bara la Amerika ya Kusini zimeathirika na mdudu huyu kwa miaka mingi
-Mwaka 2006 aligundulika hispania (Valencia)
-Mwaka 2007 aliingia Morocco
-Mwaka 2009 Alingia Uholanzi, Ureno, na Uingereza
Mwaka 2012 Aliingia Sudan. Ethiopia, Kenya, na Senegal
-Mwaka 2014 Aliingia nchini Tanzania
HUSHAMBAULIA
Mimea (Majani, na matunda) ya familia ya Solanaceae-Kama vile pilipili hoho, Nyanya, Viazi mviringo, Bilinganyi etc. MARA NYINGI HUPENDELEA ZAIDI NYANYA
? Solanum lycopersicum (tomato)
? Solanum tuberosum (potato)
? Solanum melongena (eggplant)
? Capsium annuum (pepper)
? Nicotiana tabacum (tobacco)
? Solanum nigrum
? Datura stramonium
? Solanum eleagnifolium
? Physalis peruviana
SIFA ZA MDUDU (Adult-Tuta Absoluta) /MZUNGUKO WA MAISHA.
-Mzunguko mzima wa maisha ya mdudu (yai -mdudu)ni siku 20 hadi 70
-Hutaga mayai juu ya mmea katika sehemu tofauti tofauti za mmea (katika majani, maua, na katika matunda), hutumia siku 3 hadi 9 kutaga mayai
-Baada ya hizo siku mayai hugeuka na kuwa Larvae
-Maisha ya larvae ni siku 11 hadi 37 siku
-Badae lavae hudondoka ardhini na kugeuka na kuwa pupa
-Pupa huishi kwa siku 6 hadi 24 na badae huwa mdudu kamili
-Mdudu mkuu (Adult) yuko na antena mbili
-Ana magamba ya rangi ya kaki, kijivu, au udongo
-Size ya ukubwa wa mwili ni urefu wa mm 10-12
-Ana mabawa
-Mazingira ya joto husaidia sana utagaji wa mayai
-Jike ni nene (umbo), kuliko dume
-Jike mmoja anaweza kutaga mayai 200 hadi 250 katika umri wote wa maisha yake
-Tuta Absoluta Jike huishi siku 10-15
-Tuta Absoluta Dume huishi siku 6-hadi 8
HASARA
-Usipochukua tahadhari mdudu huyu husababisha hasara kuanzia 80%-100% ya mavuno uliyotarajia.
-Mdudu huyu
ameshasabaisha hasara kubwa sana kwa wakulima wengi wa nchi hii
KUENEZA KWAKE NCHINI-TANZANIA
Mdudu huyu ameshaenea Zanzibar yote na kwa Tanzania bara zaidi ya mikoa 10 tayari imeshaingia katika hasara za mdudu huyu.
-Aliingia nchini mwaka 2014 akitokea Kenya, aliingilia 1.Arusha, badae akaingia 2.Kilimanjaro, 3.Tanga, 4.Morogoro akafika mwezi wa 6 mwaka 2014,yupo 5. Iringa tangu mwezi wa pili 2015, 6.Mbeya, 7.Mtwara, 8. Katavi, 9. Simiyu, 10.Mwanza
NJIA ZAKUENEA KWA MDUDU
Mdudu huyu mara nyingi sana huenezwa kutoka eneo moja kuja lingine kutokanana na vifaa vya shambani (Kama havikusafishwa vizuri)-hasa ile atua ya Kiwavi (Larva). Vifaa vya kusafirishia kama magari au makreti ya kubebea mazao, yakiwemo mazao yenyewe husika. Pia huenea kwa haraka zaidi kwa njia ya upepo (yule adult Tuta-Nondo), hutegemea upepo ili aweze kusafiri kutoka sehemu Moja hadi nyingine.
-KRETI za nyanya zinabebwa kutoka arusha zinaenda kwa gari hadi dar, badae gari hilohilo kreti zilezile zinaenda iringa etc kubeba nyanya pia, mzunguko ni mkubwa sana wa mdudu huyu..lazima Intervetion yake ihusishe wadau wote katika mnyororo wa thamani
JAMBO LA KUSIKITISHA
-Mdudu huyu yupo nchini sasa zaidi ya mwaka, na tayari wakulima maelfu wameshapata hasara 60-100% kwa sababu ya ugeni wao wa kutokujua nini cha kufanya dhidi ya mdudu huyu. WENGI WA WAKULIMA WAMEPATA HASARA WAMEPOTEZA MITAJI NA WENGINE WAMEKIMBIA MASHAMBA YAO.
-Mpaka sasa hakuna sera yoyote iliyotungwa na serikali zote (BARA/VISIWANI), HATA KUITISHA PRESS CONFERENCE TU YA KITAIFA NA KUMTANGAZA MDUDU HUYU KAMA NI JANGA LA KITAIFA IMESHINDIKANA.WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI NYINGI WANAJUA UWEPO WA MDUDU HUYU LAKINI HAKUNA HATUA STAHIKI ZILIZOCHUKULIWA ZINAZOLENGA KUMTHIBITI MDUDU HUYU.
-KUSEMA UKWELI, BILA NGUVU YA PAMOJA SERIKALI, NA WADAU WOOOTE WALIOPO KATIKA MNYORORO WA THAMANI WA NYANYA HAKUNA MAFANIKIO DHIDI YA MDUDU HUYU
-SHIDA KUBWA NI KWAMBA UELEWA WA WATU DHIDI YA MDUDU HUYU UKO CHINI SANA
MFANO WAPO WAKULIMA AMBAO WAKIKUTA NYANYA ZIMEHARIBIKA NA TUTA HUISHIA KUZITUPA TU, MASOKONI NI HIVYO HIVYO, MAHOTELINI NA MAJUMBANI NI HIVYO HIVYO PIA, WATU WANATUPA NYANYA HIZO AMBAZO TAYARI ZIKO NA VIWAZI (LARVA) VIWAVI HAO BADAE HUGEUKA KUWA BUU (PUPAE) NA BADAE NONDO (TUTA ABSOLUTA) TENA MAISHA YAKE YANAENDELEA ANATAGA MAYAI ETC
-MPAKA SASA KAMA TAIFA HATUNA HATA SERA (POLICY) /MKAKATI WA PAMOJA WA KITAIFA DHIDI YA MDUDU HUYU
-MZUNGUKO WA MDUDU HUYU NI MKUBWA SANA (NAAMINI HADI MWISHONI MWA MWAKA 2016 MDUDU HUYU ATAKUWA AMEMALIZA NCHI NZIMA)
Dawa kukinga Denguwe/Kanitangaze/Tuta Absoluta-HIZI NI BAADHI TU. DAWA HIZI NI VIZURI ZIKATUMIKA KUJIAHAMI (KUKINGA) MICHE IKIWA KITALUNI, AU MARA TU UNAPOKUWA UMEHAMISHIA MICHE SHAMBANI.
1. Match 500EC (Kiambata-Lufenuron)
2. Rimon 10EC (Novaluron)
3. Actra 25WG (Thiamethoxam)
4. Duduall etc
5. Buffalo 100EC
Dawa za kutibu Denguwe/Kanitangaze/Tuta Absoluta-HIZI NI BAADHI TU YA ZILIZOTHIBITISHWA TPRI
1.Evisect 50SP (Kimbata-Thiocyclam)
2. Ascotin 0.15EC/Nimbecidine (Kiambata-Azadirachtin-Mwarobaini)
3. Coragen SC (Kiambata-Chlorantraniliprole)
4. Avaunt 150 EC/ Mavuno 25EC (Kiambata-Indoxacarb)
5. Belt 480 SC (Kiambata-Flubendiamide)
Dawa no 3 (Coragen) na Dawa no 5 (Belt) Ili zifanye kazi vizuri ni vyema ukawa unazipiga kwa mzunguko, wiki hii unapiga belt, wiki ijayo unapiga coragen (ALTERNATION), Lengo kuu ni kupunguza uwezo wa mdudu kujenga usugu dhidi ya hizi dawa.
JAMBO LA MSINGI JITAHIDI KUJUA VAMBATA VILIVYOMO KATIKA HIZO DAWA, MAANA HAYO MAJINA YA DAWA (Ie Belt/ Evisect et al.. ) NI MAJINA YA KIBIASHARA TU HUBADILIKA MUDA WOWOTE
XXXXXXX NOTE, NOTE, NOTE, NOTE, NOTE.................XXXXXXXXXXXXXXXX
-Baadhi ya dawa 1. zenye kiambata cha Profenofos, dawa kama Wilcrom, Selecron, Agrocom, Supercron, Duducron, Bonaphos et al... ni dawa nzuri sana kumuangamiza mdudu Kanitangaze, LAKINI CHANGAMOTO YA DAWA HIZI ZENYE KIAMBATA CHA Profenofos BAADHI YA TAFITI, ZIMEONYESHA KUWA , Ziko na side effects kwa wadudu marafiki wa shamba na kwa wadudu wale wanaoweza kumla Tuta Absoluta
2. Dawa zenye kiambata cha Chorpyrifos , dawa kama vile Dursban, Twigaphos, Subachio, Propyrifos et al, Ni dawa nzuri sana dhidi ya Tuta Absoluta lakini pia ziko na athari kwa wadudu marafiki.
3. Dawa zingine zenye athari kwa wadudu rafiki ni zile zenye kiambata cha Dimethoate kama vile Dume, DDimate,Dimefarm,Digoz, Sume,Dud-ethoate
4. Zingine ni dawa zenye kiambata cha Deltamethrin, dawa kma vile Decis, Decis Forte, Atom, Keshet, Modeci, nk
ATHARI ZA DENGUWE/KANITANGAZE/Tuta Absoluta katika zao la Nyanya
![]()
![]()
![]()
adult Tuta Absoluta
![]()
Larvae Tuta Abosluta
![]()
effects of Tuta on Leaves
![]()
![]()
Fruit affected with Tuta Absoluta
![]()
Tuta Absoluta Life Cycle
![]()
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Kwa jambo lolote niandikie E-mail: kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
AMANI YA BWANA IWE NANYI
Tarehe; 18/10/2015 Saa 12.00 JIONI
Leo tutajifunza Faida na Agronomy ya matunda yaitwayo Parachichi (Avocado)
SOMO LA TATU; ZAO LA PARACHICHI (AVOCADO)
![]()
Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili
1. Faida za Parachichi upande wa Lishe
-Tunda lina vitamini zifuatazo
1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri
2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve
3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa
4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili
5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi
6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu
Madini- (Mineral Elements)
Ni tunda lenye
1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi
2. Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili
3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili
2. Agronomy ya Parachichi
Hali ya hewa
-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa
Joto
Nyuzi 15-25 Sentigrade
Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi
Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji
Aina za Parachichi
1. Zipo aina za kiasili
Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache
2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania
i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi
![]()
-Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi
ii. Aina ya pili ni Fuerte
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
![]()
-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo
iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana
UPandaji wa Parachichi
Nafasi kati ya shimo na shimo
-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7
Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati
-Hivyo nafasi yaweza kuwa
8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1
Ukubwa wa shimo
-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)
-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90
Mbolea
-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP
Kipimo cha mbolea,
-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche
-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa
KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
-Parachichi hasa hizi za kisasa, huanza kuzaa baada ya miaka 3 na matunda yake hukomaa baada ya miezi 6 hadi 12. Tunda la aina ya HASS ndilo huchelewa zaidi kukomaa huchukua kati ya mizei 7 hadi 12 tangu lilipo jitengeneza katika mti.
MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '
FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)
Magonjwa ya parachichi
Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda
1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni
Jani lililoshambuliwa na Alga![]()
![]()
![]()
Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri
2.Magonjwa ya matunda
Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia
-Tatizo la Athracnose husababishwa na Ukungu/Fangasi![]()
-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi![]()
![]()
![]()
Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips
DAWA
-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi
-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu
-Lishe ya mmea
Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.
-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.
BEI
KUANZIA MWEZI WA 8 PARACHICI HUWA ADIMU SANA, NA KWA MAENEO YENYE MUINUKO WA MITA 1700, NDIO MUDA WA PARACHICHI AINA YA HAAS HUKOMAA, AMBAPO
KILO MOJA YA HAAS HUWA MATUNDA 3 HADI MATUNDA 5. DEBE MOJA LA KILO 20 HUWA NA MATUNDA 40 HADI 70 KUTEGEMEA NA UKUBWA.
KUANZIA HUO MWEZI WA SABA NA KUENDELEA DEBE MOJA LA PARACHICHI AINA YA HAAS HUANZIA TSH 15000 NA KUENDELEA
JUST IMAGINE
UNA EKA MOJA (1 ) TU YA PARACHICHI YA MITI 100 TU (MITI MICHACHE KABISA), NA KILA MTI UKUPE JAPO KILO HIZO 40 (DEBE 2), NA KILA DEBE 1 UUZE KWA TSH 15000 TU
MAHESABU
MICHE 100 X DEBE 2@ MCHE X 15,000TSH@DEBE 1= 3,000,000 TSH-MAPATO HASA HUPATIKANA BAADA YA MIAKA 3 NA KILA MWAKA MAVUNO HUONGEZEKA PARACHICHI ZENYE UMRI WA MIAKA 5, HUFIKIA KUTOA MAVUNO HADI YA DEBE 8 (KILO 160) KWA MMCHE MMOJA. JE KWA MICHE 100??
MAHESABU
MICHE 100 X DEBE 8 KWA KILA MMCHE MMOJA X TSH 15,000 KWA KILA DEBE 1=TSH 12,000,000
UMRI WA MAVUNO BORA KWA MMEA WA PARACHICHI NI MIAKA 40 HADI 50
Hitimisho
Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini
Masomo mengi zaidi kuhusu kilimo yatakuwa yanakujia kupitia hapa Jf na blog yetu ya http://kilimomaarifatajiri.blogspot.com/ punde itakapo kamilika kuandaliwa
![]()
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
AMANI YA BWANA IWE NANYI
9/10/2015; 10.45 jioni
kilimomaarifa.tajirinawakaribisheni katika ukurasa huu KADRI NITAKAVYOKUWA NIKIPATA WASAA (MUDA) ntakuwa nikitoa mada mbalimbali katika ukurasa huu ZIHUSUZO KILIMO CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo kilimo cha mboga mboga na matunda; (Ukipata wasaa waweza jifunza mengi zaidi kupitia blog hii http://kilimomaarifatajiri.blogspot.com/
SOMO LA PILI ; KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.
Karibuni sanaa
Kwa leo ntajikita kueleza kwa kifupi sana na kwa lugha rahisi , KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.
1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI
-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k
Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.
BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).
Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi
-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE
i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-
Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.
Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida
ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.
2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)
Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.
Wasalaamu. mawasiliano. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
SOMO LA KWANZA; KILIMO CHA NYANYA
TAREHE; 20/09/2015 SAA 12. 49 JIONI
KARIBU
NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanaimuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..
WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA
DAWA ZA KUTUMIA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yle moth kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)
2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Arysta Life Science inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana
AGRONOMY YA NYANYA
AINA
Ziko nyingi kama fupi kiasi (Semi Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA
A; Semi-determinent
1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-
B; Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU
AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA
C; AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima
MAZINGIRA
i. Joto la kadri 20-35 degree sentigrade
ii. UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo
iii. NAFASI YA KUPANDA
-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapnada double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE
-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA
Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)
Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)
KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 30-50 kwa hybrid (F1) . Ghrama za kutosha eka moja kwa OPV variety ni tsh 100,000-180,000, na kwa Hybrid (F1) Gharama ni kati ya tsh 200,000-400,000 kutegemea na aina yenyewe ya mbegu.
UPANDAJI
Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowte utakao, na kisha chora vimefereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dodondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia mwaji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.
Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)
MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.
ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.
MAMBO YA KUFANYA SHAMBANI
Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung'oa miche, na sahamba mama pia liwe limemwagiwa vya kutosha
-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)
Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo paada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji
BAADA YA KUPANDIKIZA
Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani
Dawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao
Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, UREA, Yarra miller winner, au Hata NPK,
Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitumba vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) kama vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix
WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU
Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipingwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana sa 6 hadi sa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shape less
MATUNDA YAKIJA
Ni muhimu kuzungusha chini katika mizii mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking
WADUDU
Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)
Magonjwa
Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)
MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 120 HADI 150 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA
MAVUNO
Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 65
SOKO
Nyanya yenye bei nzuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000
Gharama za kuhudumu shamba la Nyanya kwa eka 1 ni takribani 2.5 hadi 3.5 Milioni ( Gharama kubwa ipo, katika mbegu hasa kama ni hybrid (F1), mbolea, maji (Pump), Vibarua (wakati wa kupanda na kupalilia) na madawa ya kuzuia wadudu na kutibu magonjwa.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
minimum
mls 500 kwa mche 1 kwa siku 1 (mls 250-asubuhi, mls 250-jioni)
maximum
mls 1000= 1 litr kwa mche 1 kwa siku 1 (mls 500 -asubuhi, mls 500-jioni)
idadi ya mara ngapi uirrigate itategemea sana na aina ya udongo ulio nao, na hali ya hewa ya eneo lako.
chayowa
Kiongozi asante kwa kushukuru, Shukrani sana