Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Mkuu tafadhali usinichoke, nyanya ya Rio grande na Eden ipi ina mavuno mengi?.
 
Ukipata wasaa naomba utupe A to Z ya kitunguu maji mkuu. Usituchoke tukipata changamoto huko mashambani, tutakukumbuka kwa kutuvusha hatua moja kwenda nyingine kielimu na hatimaye kikipato. Na Mungu aendelee kukubariki katika ufanyalo na kizazi chako mkuu. Amen
 
kuna miche ya nyanya ilikauka shambani,je inawezekana kuchukua mbegu moja kwa moja na kuweka shimoni moja kwa moja bila kupitia kitaluni kwanza?
 
nilimwagiza mtu akaninunulie multi k booster, kanunua yenye namba (N)13%(P)O%(K) 46% Je hii inafaa kwa viazi na nyanya
 
Mkuu ipi itafanya vizuri zaidi kwenye eden yangu kati polyfeed starter na finisher yake au yara miller tracer biz?
Nimekuta polyfeed inauzwa 7000 kwa 1kg je ni kama kiasi gani makadirio ya juu itatosha kwa ekari moja zote starter na finisher?
Je kuna tofauti ya vipimo kati ya Yara miller winner na Mono Ammonium Phosphate? Yara miller winner 50kg iko kwenye 73,000 wakati MAP 25kg ni 70,000. Naisakanya coragen inaonekana ni shida belt ndio iko sana, nishauri mkuu naplan kupiga duduall toka kitaluni kumdhibiti kanitangaze pamoja na wadudu wakorofi then shambani nitwange evisect, je nitakuwa salama?
 
Mkuu naomba msaada, nimepanda nyanya zina mwezi mmoja na mahitaji yote nilitimiza, niliacha kijana shambani nilipopata safar, mvua zilizoanza wiki iliyopita kijana naye alijichimbia kwani aliona hakukuwa na mahitaji ya kumwagilia, sasa leo nimefika pale nimepatwa na mstuko nimekuta majani yamefunika nyanya, nimechukua hatua kuingiza watu wafanye palizi mpaka kesho kutwa watamalizia, je mkuu baada ya hapo nifanye nini kuokoa shamba, kama ni mbolea niweke ipi na dawa nipige ipi? nimepatwa na kiwewe kwa majani nilikuta leo.
 
da,ahsante sana kwa elimu yako bt naomba msaada kuhusu kilimo cha matango,kuanzia hatua zote mpaka kuvuna,dawa za kudhibit magonjwa,na inachukua muda gan mpaka kuvuna,na pia soko lake lipo natarajia kulima hili zao mkuu naomba uchanganuzi
 
hiyo multi k kama iko na p sifuri (0) kweli , haitofaa katika viazi kama viko katika steji ya kutengeneza viazi, labda kama ipo katika stegi ya kukua hiyo itafaa. Hiyo multi k ingefa vizuri zaidi kama ingekuwa katika zao unalovuna matunda kama nyanya/bilinganyi ingefaa sana, coz hiyo n-nitrogen ingesaidia katika majani,na hiyo k-potassium ingesaidia sana katika matunda kunenepesha. Ila kwa viazi ilipaswa iwe na p-phosphorus kubwa (%) ili ile mizizi isaidie katika kupeleka chakula katika kiazi ili kiazi kiwe kikubwa. Kama uchumi wako si mzuri, unaweza piga hiyo hiyo multi k, but chini katika mizizi weka can mbolea kwa wingi ikusaidie kunenepesha kiazi... uote=nina imani;14911529]nilimwagiza mtu akaninunulie multi k booster, kanunua yenye namba (n)13%(p)o%(k) 46% je hii inafaa kwa viazi na nyanya
[/quote]
 
Nakushukuru MNO kwa elimu unayotoa kuhusiana na kilimo cha mboga mboga na matunda. Nina swali kidogo naomba kusaidiwa.
Ni aina ipi hasa ya nyanya ndefu (Hybrid F1)inayozaa zaidi ya nyingine kati ya hizo ulizozitaja, yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa na mvua nyingi?
Aina hiyo utakayoitaja inahiji punje ngapi kupandwa kwa shamba la ekari moja?
 
Nakushukuru MNO kwa elimu unayotoa kuhusiana na kilimo cha mboga mboga na matunda. Nina swali kidogo naomba kusaidiwa.
Ni aina ipi hasa ya nyanya ndefu (Hybrid F1)inayozaa zaidi ya nyingine kati ya hizo ulizozitaja, yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa na mvua nyingi?
Aina hiyo utakayoitaja inahiji punje ngapi kupandwa kwa shamba la ekari moja?
Natanguliza shukrani.
 
Mimi nina shamba la Hekari 20 mkoani Kilimanjaro, karibu na kilipo kiwanda cha sukari tpc lipo na visima 3, ndio nimetoka chuo, na naona hakuna uelekeo wa kupata kazi hapa mjini, na pia niliweza kusave kama million 2 hivi nikiwa chuo, sina uzoefu sana katika kilimo, japo niliwahi practice nlipomaliza advance. Hivo naomba ushauri wenu nini nifanye, na je naweza pata wapo wafadhili katika kilimo.
Tafathali ushauri wenu ni muhimu sana katika hili, kabla cjaanza kufanya White color job.
 
mkuu,naomba msaada kuhusu kilimo cha matango kinavyolimwa na ni msimu gan mzuri na vp kuhusu soko? tafadhali mkuu msaada.
 
je naweza kupiga polyfeed wakati jua linawaka? kuna minyanya imeanza kuweka maua ila hayajachanua.Sasa leo ni siku ya tatu jua linawaka, kesho nikienda kupiga polyfeed kuna madhara? Asante.
 
Naomba kuuliza je naweza kukuzia can kwenye nyanya na nikapiga polyfeed kwenye majani siku hiyo hiyo, au can itanyonya nguvu ya polyfeed? Asante
 
Mkuu habari ya Leo.nimeanza kuchuma Nyanya hybrid kipato f1 sasa bado zinazaa niweke mbolea gani ili Zinfanye vizuri na nichume muda mrefu?
 
Back
Top Bottom