Kiongozi kuhusu mbaazi take time pitia uzi wangu namba 20 ukurasa wa kwanza nilikuwa namjibu mdau mmoja, upitie. Kuhusu Matango, ziko aina nyingi kutoka makampuni mbalimbali ila nazijua aina mbili[ 1. Darina F1, 2. Botonya F1, Darina ni makubwa sana kiumbo, na Botonya ni madogo kiumbo. Ziko aina za OPV kama Ashley hii ndio inapendwa sana Sokoni , umbo iko saizi ya kati na inavimiba kiasi. Utahitaji punje 13500 kwa eka moja, Matango ni kama maboga au matikiti yanapenda maji Mengi sana mwanzoni ila kadri yanavyokaribia kukomaa maji yapubguzwe. Matango yako ya kukomaa siku 45,60, na 75. Ili kuyalinda yasiharibike ni vizuri ukayafanyia staking yaani yakawa na Nguzo za kutambalia kwenda juu.MBEGU GHARAMA, punje za Hybrid 1000 zinauzwa kti ya tsh40000 hadi 45000, Mavuno yanategemeana sana na Management( Lishe, kucontrol Magonjwa,) Mavuno kwa Eka 1 ni kati ya tani 5 hadi 15. MBOLEA kama shamba ni lako ni vizuri mwanzoni ukatumia Samadi au Mboji mixed with DAP utapata mavuno mengi mazuri. WADUDU- Wengi wanaishambulia matikiti na maboga hushambulia matango, kuna wadudu kama thrips, white flies, fruit worm, na mites ( Red). Magonjwa ya UKUNGU pia huathiri sana matango,magonjwa kama UBWIRI PODA/ UNGA - Powderly Mildew,dawa kama Ivory, au Ebony72 zafaa kumaliza matatizo hayo ya Ukungu, ila ni vizuri sana ukaanza na kutumia dawa za Jamii ya Copper mapema,kama blue Copper au Tan Copper ili kukinga mimea na shida ya fangasi- Ukungu. Dawa za kutumia dhidiya wadudu ni Nyingi tu kama karate,duduall, Suberclones. BOOSTER, NImuhimu kuspray booster ili zikupe maua mengi na yasidondoke,MAANA MAUA MENGI NDIO MATUNDA MENGI,MATUNDA MENGI BORA NDIO PESA NYINGI NDIO MAENDELEO. QUOTE="brenda18, post: 15053570, member: 171429"]Mkuu kuna maswali mawili nitashukuru kama utanisaidia
1)je naweza kuendelea na kilimo cha mbaazi kwa sasa au nimeshachelewa nisubiri mpaka kipindi kingine,shamba lipo ikilishi wilaya ya kiteto
2)naomba unielezee kuhusu kilimo cha matango,mbegu ipi nzuri,maeneo gani inakubali nk