Je Unataka Kumwacha Mke/Mume Wako Na Kumpa/Kudai Talaka Yako?

Je Unataka Kumwacha Mke/Mume Wako Na Kumpa/Kudai Talaka Yako?

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Bila kujalisha dini yako inakuruhusu kufanya haya au haikuruhusu, nipe dakika chache nikushauri jambo ambalo ukilifanya hatakaa akusahau katika maisha yake yote.

Kama jibu ni ndio unataka kufanya hayo, Fanya mambo haya sita(6) ya kumuumiza moyo wake asije akakusahau maisha yake yote?

1. Fanya kila njia ya kumfurahisha. Najua amekuumiza, amekukera, huna hamu naye, huna hisia naye tena za Upendo, ila katika kipindi hichi ya kutaka kumwacha hakikisha unamfurahisha, usiigize juu ya hili, fanya kwa bidii zote. Hili lifanye kwa mwezi mmoja, ukiona haitoshi ongeza wa pili.

2. Mfanyie vitendo vyote vya ukarimu. Kama vile kumsaidia baadhi ya majukumu yake, kumshukuru kwa mazuri yote anayofanya katika kipindi hicho, kumpongeza anapofanya vizuri, kumjali, na kuzungumza naye kwa upole. Kumpeleka maeneo ya utulivu na kupata chakula pamoja.

3. Mtii na mheshimu. Akikuambia usifanye jambo fulani usifanye, hoji baadaye kama unapenda kufahamu sababu za kukuzuia, hili unapaswa kulifanya mwanamke.

4. Ongea naye kwa heshima na Upendo. Haitakugharimu chochote kufanya hili, wala haitakupunguzia chochote, mpe heshima sirini na hadharani, mwonyeshe Upendo wa kweli, kumbuka unaenda kumwacha kumfanyia hili haitakupunja/kukupunguzia lolote.

5. Usiwe na malalamiko yeyote juu yake. Hata akikosea kitu nyamaza ukijiona umepata hasira, ukiwa kwenye utulivu mwambie kwa upendo ulikosea hili na ulipaswa kufanya vile.

6. Usijitenge chumba cha peke yako, lala naye chumba kimoja na kitanda kimoja. Katika kipindi hichi cha mwezi au miezi michache hakikisha unalala naye chumba kimoja, kama ulishajitenga naye, hakikisha mnakuwa pamoja siku zote hizo.

Baada ya kufanya haya kaa chini na kutafakari kama bado una msimamo uleule wa kumwacha mke wako ama la.

Bila Shaka hutakuwa na wazo tena la kumwacha mke wako, utakuwa umerejesha Upendo na kuondoa pengo lililokufanya msielewane na mwezi wako, utakuwa umetibu tatizo la ndoa yako.

Mungu anachukia kuachana
Tunza ndoa yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom