Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Jinsi nipikavyo Makande ya nazi.

Kwanza huwa nina sufuria moja hivi hilo ndio maalum kwa kuchemshia Makande 🙈🙈 hapa ni mchanganyiko wa mahindi ya kukobolewa na maharagwe. Basi yakishaiva nayashusha kisha nachukua sufuria nyingine kwa ajili ya kuungia.

Hapo tayari nimeshaandaa kitunguu maji, karoti, hoho , nyanya na nazi yangu ambayo nimeshaichuja katika sehemu mbili.

Nabandika sufuria kisha naweka mafuta kidogo yakishapata moto naweka kitunguu maji vikishachemka kidogo naweka hoho na karoti baadae naweka nyanya na chumvi kidogo. Vikishaiva namiminia makande yangu niliyoyachemsha kisha nachanganya pamoja na vikishachanganyika naweka tui langu lile jepesi ambalo huwa naliweka chache mno lengo ni nazi ikolee baada ya hapo nasubiria ichemke kwa dkk mbili tatu kisha naweka tui langu zito nalo nachanganya kidogo na kuangalia kama chumvi imekolea likishachemka kidogo nashusha. Hapo Makande yangu yanakuwa tayari kwa kuliwa.

Pia huwa siku nyingine naweka sukari kidogo. Hii huwa ni hiari ya mtu.
 
Nakitoa wapi[emoji23][emoji23][emoji23] si bora nikanunue kwa wale wanaokuna kkoo[emoji23]
Hahahaaa. Lol. Ununuage sasa my dear au huna familia?

Mi mwenyewe kipindi mdada mdada sikuwahi kufikiria kuwa na kibao cha mbuzi ila ile siku ya kitchen party nililetewa zawadi ya kila chombo cha jikoni mpaka hicho kibao cha mbuzi tena kililetwa toka Mombasa yaani pale uletwaji wa vyote vile wanamaanisha ushindwe mwenyewe kupika na ninacho miaka nenda rudi kazi yangu kunoa tu yale meno ya kukunia yakiwa yameisha makali. 😀😀😀😀
 
Jinsi nipikavyo mchuzi wa samaki wa nazi.

Huwa naandaa kitunguu maji, ngogwe na nyanya, nazi matui mawili zito na lile jepesi pamoja, ndimu na samaki wa kukaanga iwe ni tasi, changu, sangara, yaani ilimradi samaki. Hapa nikishachuja tui la nazi lile jepesi huwa nakamulia ndimu yangu kabisa. Mana kwetu nilivyofundishwa na Mama huwa anasema ukiweka ndimu kwenye lile tui jepesi ndio huwa inakolea.

Basi baada ya hapo nabandika sufuria langu la kupikia mchuzi ambalo ndani naweka maji kidogo yakishachemka naweka kitunguu baada ya kukoroga kidogo naweka ngogwe zangu na hapa maji hanatakiwa yawe madogo ila sio madogo sana yaani ni yale ambayo yatafanya kitunguu kilainike na hata zile ngogwe ziwe zimeondoka ubichi kidogo baada ya hapo naweka nyanya na chumvi kidogo halafu nakoroga mpaka zilainike.

Zikishalainika zile nyanya namimina lile tui jepesi ambalo lina ndimu kisha nakoroga bola kuacha mpaka lile tui lichemke. Baada ya hapo naweka samaki wangu ambao watachemka kiasi na tui lile likishaanza kupungua wingi basi namiminia lile tui zito nalo nakoroga baada ya hapo likishachemka naangalia kama chumvi imekolea basi nashusha mchuzi wangu na hapo upo tayari kwa kuliwa.
 
Shadeeya ukifungua shule ya upishi utapata wanafunzi lukuki, ukifungua restaurant halafu mapishi yako yakawa kama hayo unayoyatolea darasa hapa Wallah utafunika, maana watu wanapenda misosi iliyopikwa kwa vionjo vya utaalamu wa kale kama huu ambao siki hizi unatoweka. Hebu fanya hamu uanzishe kimojawapo katika nilivyokushauri mamii
 
Hahahaaa. Lol. Ununuage sasa my dear au huna familia?

Mi mwenyewe kipindi mdada mdada sikuwahi kufikiria kuwa na kibao cha mbuzi ila ile siku ya kitchen party nililetewa zawadi ya kila chombo cha jikoni mpaka hicho kibao cha mbuzi tena kililetwa toka Mombasa yaani pale uletwaji wa vyote vile wanamaanisha ushindwe mwenyewe kupika na ninacho miaka nenda rudi kazi yangu kunoa tu yale meno ya kukunia yakiwa yameisha makali. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Sina fam jaman mm mtu 1 nijijazie makorokoro ndani[emoji23]
 
Shadeeya ukifungua shule ya upishi utapata wanafunzi lukuki, ukifungua restaurant halafu mapishi yako yakawa kama hayo unayoyatolea darasa hapa Wallah utafunika, maana watu wanapenda misosi iliyopikwa kwa vionjo vya utaalamu wa kale kama huu ambao siki hizi unatoweka. Hebu fanya hamu uanzishe kimojawapo katika nilivyokushauri mamii
Yabidi nijitahidi Ses
 
Jinsi nipikavyo Makande ya nazi.

Kwanza huwa nina sufuria moja hivi hilo ndio maalum kwa kuchemshia Makande 🙈🙈 hapa ni mchanganyiko wa mahindi ya kukobolewa na maharagwe. Basi yakishaiva nayashusha kisha nachukua sufuria nyingine kwa ajili ya kuungia.

Hapo tayari nimeshaandaa kitunguu maji, karoti, hoho , nyanya na nazi yangu ambayo nimeshaichuja katika sehemu mbili.

Nabandika sufuria kisha naweka mafuta kidogo yakishapata moto naweka kitunguu maji vikishachemka kidogo naweka hoho na karoti baadae naweka nyanya na chumvi kidogo. Vikishaiva namiminia makande yangu niliyoyachemsha kisha nachanganya pamoja na vikishachanganyika naweka tui langu lile jepesi ambalo huwa naliweka chache mno lengo ni nazi ikolee baada ya hapo nasubiria ichemke kwa dkk mbili tatu kisha naweka tui langu zito nalo nachanganya kidogo na kuangalia kama chumvi imekolea likishachemka kidogo nashusha. Hapo Makande yangu yanakuwa tayari kwa kuliwa.

Pia huwa siku nyingine naweka sukari kidogo. Hii huwa ni hiari ya mtu.
Basi kwenye makande ongeza njugu mawe kidogo,tangawizi na pili pili pili manga (viazi mviringo pia ukiweza unavikata vidogo vidogo unaweka wakati wa kuunga kande)
 
Basi mi nimezoweaga vibaya yaani ubwabwa wangu wa nazi mpaka ukishakauka niweke lile tui zito hapo ndio naona nazi inakolea.

Hivyo tui lile la kawaida huwa nalikadiria lisiwe lenye kuivisha ubwabwa mpaka ukatota yaani naacha kiini kigumu kidogo ili nikiweka tui zito dkk ngapi tu nafunikia kiive.
Mie mchele nusu natumia nazi tatu ,napika kwa kutumia tui zito na sio jepesi ,zamani nilikuwa natumia tui jepesi lakin nazi ikawa haisikiki
 
Basi kwenye makande ongeza njugu mawe kidogo,tangawizi na pili pili pili manga (viazi mviringo pia ukiweza unavikata vidogo vidogo unaweka wakati wa kuunga kande)
Ahsante nitajaribu siku moja.

Vp hapo Mahindi na Maharage yanakuwepo au kuna kimoja naacha?
 
Mie mchele nusu natumia nazi tatu ,napika kwa kutumia tui zito na sio jepesi ,zamani nilikuwa natumia tui jepesi lakin nazi ikawa haisikiki
Saafi sana. Japo nawaza si nazi inakuwa nyingi sana?

Sababu kama mie nikipika mchele kilo moja naweka nazi moja na huwa naona inakolea vizuri tu.
 
Saafi sana. Japo nawaza si nazi inakuwa nyingi sana?

Sababu kama mie nikipika mchele kilo moja naweka nazi moja na huwa naona inakolea vizuri tu.
Sio sana napika kwa tui la kwanza tuu bila maji,yani nikisha chuja tui langu ,nalibandika jikoni natia chumvi tuu likichemka naweka mchele
 
Back
Top Bottom