Je, unawaza ujiajiri? Pita hapa na itazame hii biashara kama itakufaa

Je, unawaza ujiajiri? Pita hapa na itazame hii biashara kama itakufaa

paul c

Senior Member
Joined
Jan 20, 2015
Posts
123
Reaction score
110
Heshima kwenu wanajamii wenzangu tunaokutanika katika mtandao huu. Niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kutokana na hali ya uchumi kuwa ngumu na mazingira ya kibiashara kuwa magumu ni awzi sasa uwekezaji unatakiwa kufanywa kwa uwangalifu mkubwa. Hapa namaanisha kuwa na uhakika katika uwekezaji unaotaka kuufanya.

Watu wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya wapi hasa awekeze fedha aliyonayo ili kupata tija katika uwekezaji wake. Kwa kuzingatia hali ya kiuchumi na mazingira ya kibiashara basi nimekuja na hili biashara amabayo kwa sasa inashika kasi maeneo mengi ya Tanzania ili kwa watakaoona ni fursa basi tujadiliane namna ya kuanzisha hii biashara katika eneo lako unaloishi.

Aina ya biashara: STUDIO

Neno studio linatumika kama duka la kuuza cd, na dvd za movie, music, gospel, documentary etc. Kuweka music, movie na games kwenye hard disk, flash, memory card, laptops, etc. Pia kuuza flash disks, memory cards, card reader, usb cables etc.

Mahitaji:

1. Desktop computer iwe na processor kuanzia duo core, hard disk tofauti na ya operating system iwe kuanzia 4tb (terabyte nne). Hii ni ya muhimu zaidi kwani ndio mtaji kuu katika ofisi yako sehemu kubwa ya kipato itatokana na uwezo wa computer yako katika storage.

2. Sound system (subwoofer inafaa) hii ni kwa ajili ya kutangaza nyimbo na movie zilizopo ofisini kwako. Pia hutumika na wateja pindi wanapochagua nyimbo na movie.

3. Meza ya ofisi na viti vinne. Hii ni meza kwa ajili ya kuweka computer na vitu vingine. Viti ni kwa ajili ya mhudumu na wateja.

4. Mahitaji mengine ni kama extension, usb hub port 4, dvd na cd empty kopo moja, mabango ya ofisi, memory card, flash card, card reader, moderm, external hard disk 1, sleeves, marker pen, software na usb cable.

5. mazingira yanayofaa kwa kufanyia biashara husika kama chumba chenye usalama, shelve za kutundika vitu ka flash , memory n.k mapambo mengine unayopendelea katika ofisi yako.

Mahitaji yote niliyoorodhesaha hapo juu yanaghrarimu shilingi za kitanzania 3,000,000/= (milioni tatu) bila kuhusisha gharama za kodi za nyumba, leseni na mapatao na kodi nyininezo.

Baada ya kupata ufafanuzi huo sasa tuangalie masuala muhimu ya kuhusiana na biashara hii.

1. Eneo la biashara: hili ni jambo la muhimu sana wakati unachagua eneo la kuanzisha hii biashara. Kuna maeneo mengi watu wanakosa huduma ya hizi studio. Sehemu nyingine unakuta kata nzima hakuna au kijiji kizima hakuna hata moja. Anzisha kwenye hayo maeneo ndio fursa ilipo.

2. Mhudumu : hapa inahitajika mtu mwenye ujuzi wa computer katika basic issues kama kuburn cd na dvd, kusend file kwenye flash memeory, n.k, kuconvert files, kudownload, na uelewa wa format mbali mbali zinazotumika kataika simu, deki na tv. Mtu mwenye ujuzi wa kawaida wa computer anaweza kufundishwa na akaelewa kwa muda mfupi.

3. Upatikanaji wa mahitaji yote niliyoyataja: yote yanapatikana utakapo kwama utaniuliza mimi na nitatoa ufumbuzi na hata kukuletea mahitaji unayotaka kwa gharama nafuu.



4. Mapato: biashara hii inaweza kuzalisha fedha nyingi kwa kadiri unavyoweka usimamizi mzuri na upatikanaji wa mahitaji ya wateja kwa muda muafaka. Kama eneo ulilopo lina umeme wa uhakika na hakuna hii biashara unaweza kutengeneza hela nyingi kwa siku. Hapa Mara nyingi ni uwezo wa mtu kibiashara ndio unampa mapato mengi kwa siku.



5. Usimamizi : usimamizi wa karibu ni muhimu sana katika biashara hii ili kuweza kujua mahitaji ya wateja na mapungufu ya kibiashara ili kuyaborsha kwa wakati. Unaweza ukafanikiwa sana kama utafanya bishara hii peke yako kabla ya kuajiri mtu.


Chanagamoto :

1. Umeme: umeme unasababisha biashara kuwa ngumu kama utakuwa unakatika mara kwa mara. Hata wateja wengi wanategemea umeme ili kufurahia huduma hii.

2. Ujuzi: hii ni changamoto kwenye kujua format na matatizo mbalimbali yanayaowakabili wateja na kuyatatua.

Mwisho : kwa waliokuwa wanatamani kufanya biashara hii na ukawa hujui pa kuanzia karibu tuelezane namana ya kuanza na kuendesha hii biashara. Pia kwa wale waliovutiwa pia karibuni tuanzishe hii biashara na kupata kipato nitatoa muongozo wote katika hili.

Kwa wale ambao hawajavutiwa pia karibuni kwa michango mbalimbali yenye kujenga na kuelimishajuu ya kujikwamua kimaisha.

karibuni wote kwa maboresho au maswali au maoni kuhusiana na hili.
 
Nimekuwa na mpango sana na ofisi kama hiyo ..kitu nilichojifunza ni location na Kuweka mahusiano mazuri na wateja maana kuna sehem unakuta hata wenye hiyo biashara wapo Wengi ila bado inakuwa inalipa tu...bianfsi nimeanza kununua vitu kidogo kidogo.
 
Pamoja na maelezo yako yoote mazuri hivi unajua biashara yako ni HARAMU??
 
Mtoa mada nakupongeza ...
Wengi wetu hawako wazi kuweka mawazo hayo wazi ...

Pili anayesema hiyo kazi ni haramu .. simwelewi ... mambo yote yanayokatazwa ndo yana faida.. kinachotakiwa ni kutengeneza mazingira ya kuyaharalisha.
 
Mtoa mada nakupongeza ...
Wengi wetu hawako wazi kuweka mawazo hayo wazi ...

Pili anayesema hiyo kazi ni haramu .. simwelewi ... mambo yote yanayokatazwa ndo yana faida.. kinachotakiwa ni kutengeneza mazingira ya kuyaharalisha.
"mambo yote yanayokatazwa ndo yana faida"
Nimekuelewa vizuri sana
 
Hapo tatizo ni msimamizi mwaminifu tu mkuu,hayo mengine yanawezekana
 
Wazo zuri Sana mkuu ,nimeanza kununua baadhi ya vitu kwa ajiri ya kazi hii
 
movie naweza kupata wapi wakuu, zilizotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.
"respect kwake captain derick gaspal mukandara....rufufuuu"
Wewe upo wapi... Movie zina patikana kariakoo wanauza 1000 kwa movie moja ukichukua nyingi bei pia wana kushushia... Nenda aggrey na likoma utakuta maduka ya movie kibao ushindwe wewe tu... Ukishindwa ni pm niku elekeze vyema
 
Simpo Startup
1. Computer tower (500GB) 250,000
2.internal HDD 1TB 80,000
3.empty CD 12000
4.empty DVD 13500
5.meza 40000
6.viti 3x15000 45000
7.extension 15000
Kwa namna ulivyoiweka itakuwa unataka na wew uwe msindikizaji katika biashara. Iyo hard disk ya tb1 utaweka nini? Kama utaifanya Kama kazi utaishia kupata elf 10 ya nyimbo kila siku.
 
Back
Top Bottom