Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
Hivi yule Ally Maswanya aliyeukataa UDC wa jiwe, yuko wapi sasa? Hahahaa
 
Usimtie ubaya raisi. kukubali au kukataa uteuzi ni hiari, wapo wengi tu waliwahi kukataa huko nyuma na Wala haikua issue.

Raisi Samia hawezi kusema eti wafanyiziwe kisa tu wamekataa uteuzi. Haipo hivyo

Mwaka 2017, Rais Maguful alimteua Kanali mmoja kuwa mkuu wa wilaya akagoma kwasababu alikua mkuu wa kikosi na alijua madili yataisha, kilichofata ni kustaafishwa

Neno la Rais halipingwi
 
Kitu gani hicho kikubwa kinakuja? Katiba mpya, sivyo?
 
Amri ndiyo
Kuteuliwa na raisi si amri bali ni mapendekezo,ndio maana hata yeye akiona hutaki uteuzi anabadilisha ndani ya muda mfupi. Mfano ni uteuzi wa chegeni kuwa RC

Wapo wengi wamewahi kukataa teuzi na raisi akabadilisha. Hata huyu mkurugenzi wa sasa wa shirika hili kubwa tu alikataa, Ila baadae akaulizwa anataka nini ili aweze kukubali. Ingekua ni amri basi asingeulizwa chochote Bali angeteuliwa tu.

Yule prof wa kihaya kule US, alisema hapana na Wala hakukua na shida.

Wakati wa magufuli Kuna wanne pia walisema hapana, na wakateuliwa wengine. Ambao naona ngumu kukataa ni wale makada wa chama
 
ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
Unampa mtu offer akikubali ndio unamtangaza, sasa hapa naona mkuu wa nchi au watu wake hawakufuata protocol, wanatangaza tuu watu utafikiri watu hawana plan nyingine za maisha, lakini huyu mama anaonekana hana roho ya kipuuzi na mambo ya kishamba kuanza kufuatilia au kuwakomoa waliokataa hizo nafasi, naamini hakuna kibaya kitakachotokea kwa waliokataa hizo nafasi
 
Zama za Giza zilishapita, Mungu alimaliza ugomvi Kwa umahiri.
 
Mimi ningekuwa DC tu.

Kwanza marupurupu.

Ninaweza kukopa zaidi ya million 100 na kufanya miradi.

Ntaendeshwa na gari na kuwa bosi wa wilaya nzima.

Mwisho nitakuwa chawa wa mama hadi anarudishe Tena madarakani niendelee kula mema ya ya nchi.
cwt kuna marupurupu Zaid, maana hela ni nyingi Sana na utaratibu kukaguliwa mahesabu sio kama serikalini, Kuhusu mkopo Cwt viongozi hua wanajikopesha tena bila riba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…