Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
 
Mimi ningekuwa DC tu.

Kwanza marupurupu.

Ninaweza kukopa zaidi ya million 100 na kufanya miradi.

Ntaendeshwa na gari na kuwa bosi wa wilaya nzima.

Mwisho nitakuwa chawa wa mama hadi anarudishe Tena madarakani niendelee kula mema ya ya nchi.
Kwani milion saba mshahara huwezi kukopeshwa milioni 100?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Pengine kipaumbele si mshahara. Wengine huanzia hapo, ila wanajipambanua kiasi cha kupewa ubunge na hatimae uwaziri. Ukifikia uwaziri, unaweza kuwa yeyote hata rais kama tulie naye sasa.
 
ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
Mbona kuna mwamba alimkazia Magufuli akakataa ukuu wa wilaya na mpaka leo fureshi tu.

Mama ni muungwana, machawa kibao Ccm wanazitaka hizo nafasi, wacha wapewe wenye uhitaji wapo wengi sana.

Kuna tatizo kwenye vetting, huwezi kumteuwa mtu bila kupewa briefing kwamba anateuliwa, papo hapo mtu anakuwa na muda wa kukataa Kwa wanausalama wanaomfanyia vetting.
 
Back
Top Bottom