Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

Je, unaweza kuacha mshahara wa milioni 7.8 na kuwa Mkuu wa Wilaya anayelipwa milioni 3 kwa mwezi?

Mbona kuna mwamba alimkazia Magufuli akakataa ukuu wa wilaya na mpaka leo fureshi tu.

Mama ni muungwana, machawa kibao Ccm wanazitaka hizo nafasi, wacha wapewe wenye uhitaji wapo wengi sana.

Kuna tatizo kwenye vetting, huwezi kumteuwa mtu bila kupewa briefing kwamba anateuliwa, papo hapo mtu anakuwa na muda wa kukataa Kwa wanausalama wanaomfanyia vetting.
Alifukuzwa Tigo Yule mwamba
 
Ukiwa mpigaji mzuri huo mshahara 3m ni WA kununua soda tu! Kumbuka wewe unaidhinisha kila kitu, mkurugenzi hawezi kula kabla wewe hujala. Ila tatizo ni kutumbuliwa wakati wowote.
Hujui usemacho.
DC anatenga mkono wa DED, hadi mafuta anasubiria apewe.
Hawezi ondoa gari bila kumtaarifu DED
 
Kila MTU ana Uhuru wa kuchagua lakini Uhuru huo haupo kama unavyotamkwa,kuna watu wanatolewaga huko UN,Bank ya dunia na baadhi kwenye international organization wakiwa na mishahara mikubwa na kuja kupewa majukumu ya mishahara midogo na inawalazima kufanya kwa kuwa ni presidential appointee sembuse U DC ndio ukatae??
Wote hao huwa mishahara inakuwa matched unless awe ni TISS
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
Kama ana nia ya RC au mbunge KISHA aje awe waziri Ili aje apige zaidi ya hio 7.8.
Maisha ni hesabu na kila mtu anazake
 
Ndipo mjue kuwa viongozi wengi wa nchi yetu sio wazalendo.
Wanavaa tai zenye alama yq bendera ya Taifa huku wakiwa wachumia matumbo tu.
 
Ukiwa DC unakula mema na tunu ya Taifa aisee
Nje ya msgaara Kuna usalama mkubwa sana wa mambo Yako ...
Rais wa Wilaya si kitu Cha kawaida
 
Jua miradi yote wilayani yeye ni wa mwisho kuidhinisha, hapo unaasemaje? Kuna mmoja alilalamika kwa raisi kuwa DC anachelewesha miradi, DC kajibu hawezi kusaini visivyoeleweka. Jamaa kaondolewa DC kabaki, enzi ya mwamba JPM.
 
16751391011740.jpg
 
MAMBO yamekuwa MAMBO .Wewe ni MTUMISHI wa TAASISI fulani unalipwa MSHAHARA wa Tsh.Mil.7.8
UNATEULIWA kuwa DC ili Upate MSHAHARA wa Tshs Mil.3 na SHANGINGI
Je UTAKUBALI TEUZI au UTAKATAA?
It's more than that ndugu, Sir robby !!

Money is very important but money is not everything in life..

Life is about happiness, freedom, security and peace of mind..

Kwa mfumo wa utawala wa nchi yetu, u - DC ni cheo cha madaraka cha kuonea na kunyanyasia watu hususani wenye mawazo na itikadi za kisiasa zinazokinzana na mtawala..

Ukifanya Kwa kufuata Sheria, kesho yake aliyekuteua atakuona hujui kazi na utarudi shamba kwenda kulima..!

Kwanini ujiingize kwenye shida na UTUMWA wa namna hii iwapo Mungu tayari kakujalia kuwa na kazi nzuri, yenye mshahara mzuri na marupurupu na uhuru binafsi wa kutosha..??

Kama wanalipwa mshahara mkubwa kama unavyosema, hilo sio kosa lao. Ni utaratibu na makubaliano ya walimu wenyewe kuwa viongozi wa level hiyo walipwe hivyo!!
 
DC ni raisi wa hilo eneo kila kitu kipo chini yake,, ni kazi ya heshima sana. Raisi Akija anaonana na DC na sio mkurugenzi. Akishirikiana vizuri na walio chini yake anapiga pesa nzuri. Hapo ninazungumzia upigaji japo ni vibaya.
 
Kila MTU ana Uhuru wa kuchagua lakini Uhuru huo haupo kama unavyotamkwa,kuna watu wanatolewaga huko UN,Bank ya dunia na baadhi kwenye international organization wakiwa na mishahara mikubwa na kuja kupewa majukumu ya mishahara midogo na inawalazima kufanya kwa kuwa ni presidential appointee sembuse U DC ndio ukatae??
Ukiona hivyo tambua teuzi inalipa.
Hakuna mtu aachae kikubwa na kufuata kidogo
 
ILA watajutia kukataa uteuzi ni dharau na kibri kwa mkuu wa nchi....kuna kitengo kitashughulika nao tena kimyakimya bila kelele! Labda kelele watapiga wao na si ajabu mkashangaa watu wakakimbilia kuropoti.. Serikali ni sirikali haijawahi kushindwa!
Nishasema huna unalolijua zaidi ya uwongo. Acha ujuaji hakuna kitu kama icho unachofikilia kwenye libongo lako mzee mzima ila hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom