Je unaweza kupaka rangi nyumba bila kuweka wall putty?

Je unaweza kupaka rangi nyumba bila kuweka wall putty?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Wakuu kama lipu imeshafanyika je unaweza kupaka rangi nyumba bila kuweka wall putty?

Hii putty ina ulazima gani wakuu?
 
Wakuu kama lipu imeshafanyika je unaweza kupaka rangi nyumba bila kuweka wall putty?

Hii putty ina ulazima gani wakuu?
Kufanya skimming katika kuta hakukwepeki ndg, ukipaka rangi kwenye kuta moja kwa moja bila kuweka putty, utatumia kiasi kikubwa cha rangi kutokana na rangi nyingi kunyonywa na kuta

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Wakuu kama lipu imeshafanyika je unaweza kupaka rangi nyumba bila kuweka wall putty?

Hii putty ina ulazima gani wakuu?
Inawezekana ila kunakuwa na utofauti Mkubwa wa Aliefanya skimming akapaka na rangi na yule ambae hajafanya skimming amepaka rangi tu.

Skimming ina smooth ukuta na inasaidia pia kupambania na fungus pia Inapendezesha Zaidi nyumba.
 
Ni sawa na kupaka mafuta mwili bila ya kuoga
Tatizo Ni nini Ndugu? Uchumi mdogo au fashion?
 
Kufanya skimming katika kuta hakukwepeki ndg, ukipaka rangi kwenye kuta moja kwa moja bila kuweka putty, utatumia kiasi kikubwa cha rangi kutokana na rangi nyingi kunyonywa na kuta

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
🤝🙏
 
Wakuu kama lipu imeshafanyika je unaweza kupaka rangi nyumba bila kuweka wall putty?

Hii putty ina ulazima gani wakuu?

Mi siyo fundi ila nimeona maeneo wamepaka rangi bila wal putty.na ilipendeza sana.nikauliza ilikuwaje.wakasema wall putty pamoja na chokaa ni chakula kizuri cha fangasi, hivyo hufika mahali kama kuna magadi inatuna na kubanduka.Ila shart yule anayepiga lipu anyooshe sana lipu yake asiweke matuta.

Ila kwa kuwa wallputty na kina watu wanaishi kqa kuuza wallputy wanaweza kuja hapa wakapinga kabisa hiyo idea.

Ila kujibu swali lako ni kweli inawezekana kupaka rangi baada bila wallputy na nyumba ikapendeza tuu kulingana na aina ya rangi na uwezo wa fundi rangi
 
Suala hapo ni ubora na muonekano, maana hata rangi iliyopigwa juu ya wall putty nayo mwishowe itachakaa na kuchunika tu.

Ila kupiga wall putty kabla ya kupiga rangi ni bora zaidi na inakuwa na muonekano mzuri zaidi, japo inatakiwa upate rangi sahihi katika mazingira sahihi, na umpate fundi mwenye weledi.
 
Inategemea aina ya rangi. Ile silcoat(rangi zenye vipele) inapigwa baada ya plaster tu haihitaji ufanye skimming na wallputty.
 
Inategemea aina ya rangi. Ile silcoat(rangi zenye vipele) inapigwa baada ya plaster tu haihitaji ufanye skimming na wallputty.
zinauzwqje hizi mkuu, kama unaweza kujua bei
 
Back
Top Bottom