Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

shukrani kwa world bank waliotupa pesa ya kujenga pale toka wakati wa kikwete
 
Nimekuelewa japo sio sana, nitakuelewa zaidi ukinisaidia pia maswali haya...

Nilipopita pale tazara, (FLY OVER YETU) niliona bango limeandikwa "kwa ufadhili wa watu wa JAPAN" (najiuliza hapa tuwashukuru watu wa JAPAN au JPM?)

NASIKIA ubungo pia kutakuwa na bango kubwa lililoandikwa "KWA UFADHILI WA BENKI YA DUNIA" (Kama ni kweli, tushukuru benki ya dunia au JPM?)

Lakini pia, naomba nisaidie mkuu, baba yangu aliye staafu tangu mwaka 2018 amekuja lipwa mwaka 2020, yeye pamoja na wenzake waliokumbana na adha hiyo nao wamshukuru JPM?

Watumishi wa umma waliokaa miaka 5 pasipo kulamba nyongeza ya mishahara yao wala kuona juhudi zozote za makusudi kuboresha basic salary zao (wamshukuru JPM?)

Wakulima wa korosho kule kusini je? Nao wamshukuru JPM?

Vipi wahitimu wa elimu ya juu,tangu mwaka 2015 ajira zao ni kitendawili haswa, nao wamshukuru JPM?

Wananchi wa kimara, waliopoteza makazi yao, wakiishi kama wakimbizi baada ya bomoa bomoa iliyozuiwa na mahakama, lakini ikaagizwa zivunjwe haraka, nao pia wamshukuru JPM?

Ukinifafanulia haya machache nitakushukuru sana na pengine nitaungana nawe kuhakikisha natoa shukrani zangu za dhati pia...
 
Mimi siwezi kusema Asante mpaka tuzione hesabu za pesa na tujiridhishe ccm hawa kuiba kabisa.

Mi ccm mipigaji sana.

Halafu pesa ni zetu walipa kodi.

Kodi zetu halafu tumshukuru mtu asiye lipa kodi?!
 
Kwa maana hiyo lazima uwashukuru na wakooloni. Hivi sio kodi yako na yangu.
 
Acha njaa na kufanya watu hatuna akili, Kodi zetu na vinapaswa kufanya zaidi ya hivyo.
 
Alichoandika ni ukweli japo ametumia lugha kali sana!
Utakumbuka wasomi aliowataja hapo juu namna walivyokuwa mstari wa mbele kupigania mabadiliko ya kimfumo (katiba) walizunguka kila mahali kutuaminisha kuwa ili nchi ikae sawa sawa tunalazimika kubadili msingi wa uendeshaji nchi, leo hii wao ndiyo wanawafokea wanaopigia kelele kile walichokipigia kelele wao!
 
Anaweza kuthibitisha kuwa yeye ni PhD holder bila kuua mtu!?
 
Ujinga mzigo yaani hata ww umepofushwa ubongo! zaidi ya miaka 50 ya uhuru mnashangaa daraja SHAME ON THEM
 
Usiposema ni. Unafki.. kazi imefanyika pale
 
Yale ni madaraja interchange unazijua ww vile ni vivuko tuu vya juu
 
Mkuu Paskali, hivi magufuli alipotumia fedha za ndani ambazo ni kodi za watanzania kujenga hiyo interchange amefanya wema au ametimiza wajibu wa serikali kwa wapiga kura wake? Mbona hata wewe msomi kabisa unakuwa carried over na propaganda za kiCCM? Serikali kujenga barabara, hospitali, reli, interchange, nk sio HISANI bali ni WAJIBU wake kwa wananchi. Ni sawa na wewe unafanya kazi mahali na unalipwa mshahara wako kila mwezi unataka watu wakusifie kwa kazi unayofanya wakati huo ndio wajibu wako na ndivyo ulivyosaini mkataba. Mkuu Paskali wewe vipi?

Lakini nakujua wewe ni mzuri katika kuchokoza mada ukitaka watu wafunguke zaidi. Unajua kabisa unachokifanya, wala watu wasikuone kama kibaraka wa CCM wakati wewe sio mchumiatumbo na mwenye kujikomba kiasi hicho. Unajitambua sana tuπŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Elimu na usomi ni endelevu. Elimu haina mwisho.
Kwenye tafiti kuna ugunduzi mpya na uvumbuzi wa kitu tofauti hilo linakubalika.
Yawezekana wamegundua kitu tofauti
Hahahaaa, wanapaswa kutwambia sasa kipya walichogundua, ili wote tufahamu kwamba kumbe yale waliyoyapigia kelele si muhimu tena, na sisi tutapima ugunduzi wao kama ni wenye manufaa kwa vizazi vya sasa na baadaye...
 
Rest in peace my former mentor Pascal Mayalla! Siyo kupumzika kwa sababu ya kifo! La hasha!!

Ni kutokana na huu wakati mgumu unaopitia kwa sasa tangu ulipoamua kwa makusudi au hata kwa bahati mbaya, kuchagua maisha ya unafiki, kisa tu njaa.

That is Democracy! Na hayo ni maisha yako binafsi. Hayupo wa kukupangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…