Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Hivi nikienda ATM kuchukua fedha zangu natakiwa kuisifia machine ya ATM? barabara zinajengwa kwa kodi zetu vipi tunaambiwa tumsifie mtu? Tena aliyeanza kuijenga (Kikwete) hakutaka kusifiwa kwani alijua anatimiza wajibu wake!
 
Pesa zetu tumshukuru yeye tena yeye anapaswa kutushukuru sisi kwakuwa malengo yake huko Chato yanatimia
wacha uongo ni msaada wa japan na korea, mshukuru jpm tu, kodi yako imeliwa na mdee kamuulize hela za mfuko wa jimbo ziko wapi?
 
Hivi nikienda ATM kuchukua fedha zangu natakiwa kuisifia machine ya ATM? barabara zinajengwa kwa kodi zetu vipi tunaambiwa tumsifie mtu? Tena aliyeanza kuijenga (Kikwete) hakutaka kusifiwa kwani alijua anatimiza wajibu wake!
kwakipato gani unalipa kodi? hako ka payr kako hata mita moja ya mtaro hakawezi jenga
 
Hivi ndugu yangu Mayala tangu lini umekuwa kichaa????Tumpe jpm asante kwani Fedha katoa mfukoni mwake??hata jiwe la msingi nakumbuka ni Gharib bilal ndio aliweka akiwa makamu wa raisi tz!!!
 
mimi nakula vumbi huku kasulu wew unaleta habari za fly ova wew ni mpuuzi kabisa mimi inanihusu nini..? atoe vumbi mkoa wa kigoma acheni ubinafsi hii nchi ni ya wote
 
Wajinga ni wale wanaomuona Lissu kuwa ni mkombozi wakati ni dalali wa Amsterdam na wapumbavu wengine wa huko ulaya.
Na magu ni mkombozi na dalili wa nani? Kama si dalali wa Barrick awake hadharani makubaliano aliyoingia na barrick tuone? You are a stupid ideot
 
Sasa ndio tukeshe kwa kumsifu na mapambio? Je hakuna eneo alilokosea katika utawla wake? Sisi tunaona Hafai si kwa kuwa hakujenga Barabara ,laa bali kwa Mengine yahusuyo haki za watu na maisha yao,Katiba Mpya n.k upande huu kateleza. na kwa hiyo Tutamuhukumu kwa kutomchagu kuwa raisi., akiwa Ubaoni Tutakwenda kuchukua Ushauriwake akiwa kama Mpizani. Mbola limekaa vizuri hili.

Baada ya Kupata Katiba yetu mpya ambayo CCM hawawezi kulifanya hilo Tutawaalika waje kuibariki na kutia neno

Yatupasa kuwashukuru wakoloni pia ,maana hata wao waliikuta Tanzania haina shule , wala Hopitali wala Reli wala Barabara.
Wao walijenga vitu hivyo kama serikali pamaoja na Haja za kiuchumi walizokuwa nazo lakini Serikali ndio ilisimamia kuyafanya hayo kwa manufaa ya Taif zima.
Je na wao Tuwatupie Sifa kabla ya CCM na serikali yake??

Hebu tukubaliane kuwa Serikali kusimamia Maendeleo ni wajibu wake wa Msingi na wa Lazima, si suala la kuwaaliye fanya katufanyia Fadhila na kwa hiyo Tukeshe kwa kumsifia.
Kwani sisi Wapinzania tumemlaumu Raisi kwa kujenga Reli, bwawa la umeme au Hospitali? Si katimiza wajibu wake.
sisi tunamlaumu kwa Kunyima haki za watu z Kujieleza, kisiasa, kiuchumi na ukandmizaji mwingine wa uhuru wa watanzania.
 
Wee jamaa kanjanja sana, unaingia kwenye uchaguzi unaambulia kura yako mwenyewe. Unaonyesha jinsi gani usivyoweza kujenga hoja hata kushawishi watoto wa chekechea..
 
Umemena vyema kwamba "kujidharilisha kutokana na njaa (aka mayalla kule kwetu) ili apate chochote". Sina uhakika, lakini pengine jina linaakisi ukweli huu.
 
NGOJA nikukumbushe kidogo!Wakati wa Mwalimu Nyerere .Wasafiri wa Tanga walikuwa walipanda mabasi pale mnazi mmojq kama saa 12 .30 hivi za jioni kuelekea Tanga .Na walikuwa wakifika Tanga majira ya saa 10 hivi za alfajiri sababu ya ubovu wa barabara .Kiongozi anapotengeneza miundo mbinu ni jukumu lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…