Tundu Lissu aliwahi kusema kuwa "Tunamshukuru Rais Magufuli kwani kwa namna moja ametusaidia kufagia takataka ndani ya chama chetu"
Na mimi namshukuru kwani amenisaidia kujua kuwa baadhi ya watanzania kuuza utu wao au kujidharaulisha kutokana na njaa ili apate chochote kitu ni swala la muda mfupi sana.
Unajua Tanzania ipo nyuma sana kidemokrasia na kuwa na watu wenye akili kwakuwa tumetengwa eneo moja na tukajikuta tumekaa na mazuzu wengi.
Pascal Mayalla anajua kuwa kwa vyovyote vile kama kiongozi huwezi kufanya jambo la maendeleo ya miundo mbinu kuwa hisani ya kutesa, kuua, kunyima wengine haki na kuzuia watu wasikukosoe. Ila kwa kuwa ni moja ya watanzania aliowasema Tundu Lissu ndiyo maana unamuona anachotuletea humu.
Hivi kweli ukiwa mtanzania mwenye akili timamu unaanzaje kumshabikia Magufuli? Narudia tena, unaanzaje? Emb tuweni na aibu jamani! Tunachekwa na dunia.
Ila ndiyo watanzania wenzetu, tunaishi nayo humu humu Tanzania.
Hili linchi nadhani limekuwa likubwa halafu hata faida ya kuwa linchi likubwa haionekani. Uwe na linchi likubwa basi walau ionekane faida yake. Halafu nawaza sana inakuwaje mfano mtu kama huyu mleta mada unaweza kukuta kasoma hadi chuo kikuu tena kwa kufaulu lakini ona alivyo na uwezo mdogo wa kufikiri mambo kwa undani.
Unajua zuzu likiona kitu kidogo tu linalipuka kwa shangwe maana huwa halina uwezo wa kujiuliza. Huyu mleta mada kapita tu kwenye barabara ya juu ghafla kaona ewaaa matatizo yote yameisha Tanzania. Anaenda kulala ana amani kabisa kabisa. Nataka uone ni jinsi gani tulivyo na watanzania mazuzu.
Walikuwepo kina Bashiru, Polepole kina Ryoba kina Kabudi. Hawa tulikuwa tukiwaona wakiwa mstari wa mbele kuhubiri haki. Lakini kumbe wooote ni mazuzu. Walikuwa wanaongozwa na shida binafsi. Sasa wamepata kidogo na kwakuwa hawana uwezo wa kufikiri tena baada ya kupata imekuwa basi. Hawa ni watanzania walioenda shule lakini ona vichwani mwao kwa sasa.
"Stupid generarion"