Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

tapatalk_1601533924924.jpeg
 
Interchange ndo nini huku kigoma wala hatujui mkuu basi hapo dar mpeni kura kwa wingi ili mpite kwenye interchange mkiwa na hofu kama hamjawahi kuchangia kodi
 
Mkuu umesomeka kwa pamoja tutampigia kura za ndio JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Kwani hela katoa mfukoni mwake...

Ukipita pale unatakiwa kusema ahsante kodi yangu....
 
Hakuna cha asante hapo, atujipendekezi, ni kazi aliiomba na analipwa vizuri sana, na matunzo anayopewa ni makubwa kuliko mtanzania yeyote yule. Ndio maana tunampunzisha Oktoba 28.

Njaaa zako za kutaka uonekane kwenye TEUZI ukichanganya na ukabila ulio nao, Manjaa wewe, unaitia aibu sana taaluma ya Uandishi habari.
Kazi ya Serikali ni kusimamia, na pesa ni zetu, kodi zetu Watanganyika, koma kutuona watanzania wajinga.
 
Panda jukwaani brother ili uyafikishe yote yaliyoujaza moyo wako. Mimi nakaa Matare hiyo flyover ya ubungo inanisaidia nini mpaka nitoe Asante ya kura yangu. Danganya Ngosha wenzako mnaojiandaa kupewa Asante kwa ushabiki wa kuumiza .
 
Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...😀😀😀😀
KIla anayetimizawaji´bu wake anapewa hongera na asante. Vipi anayejiita mwanasheria wa CHADEMA anayewatoza wana-CDM milioni 20?
 
emoji2.png
emoji2.png
emoji2.png
emoji2.png
emoji2.png
emoji2.png
wewe kada ndo maana ulipata kura Moja tu.......Yani kodi ni yangu alafu nimshukuru Komeo tena.
 
Watu wengine wanaufinyu wa mawazo, sijui ni kutoelewa au ni ushamba.

Serekali ni dynamic, kadiri wananchi wanavyofanya kazi na kulipa kodi, ndivyo serekali inavyotumia mapato hayo kutoa huduma kwa wanachi.

Plan hizo zilikuwepo anatekeleza tu, hata angekuwa mwingine yangefanyika tu, sema yeye ni mpenda misifa, kila analofanya anajionyesha utafikiri anafanya kwa hela yake, mbona wenzake wamefanya mengi tu tunayaona? angekuta nchi iko hivi?
 
Mkataba ulisainiwa tangu oktoba 2015 tangu enzi za JK.
Na mkataba uliosigniwa ni kutengeneza flyover sio interchange. JK kama angekuwepo ile fly over iliyokuwa imeplaniwa apo, hata wakenya wangetuogopa
 
Hakuna hata haja ya kusoma article ya hovyo kama hii kwani amejenga kwa hela yake, si hizo ni kodi zinazokusanywa nchi nzima.

Ni serikali gani isiyofanya hayo huku ikikusanya kodi, hayo yalifanywa hata na wakoloni toka mwaka 1900.

Ni muda sasa watu muache kuwa mbumbumbu kiasi hicho, ndio yale yale ya kuisifia ATM Machine kwa kukupa pesa yako.

Acheni ushamba, kila serikali inayafanya haya haya iwapo madarakani sasa nyie wajinga Magufuli anawahadaa utafikiri yeye ndiye anaikopesha serikali pesa yake kujengea miundombinu, nendeni mkawadanganye watoto wa chekechea. Very silly mind.
 
Back
Top Bottom