Je, unaweza kutambua video zilizotengenezwa kwa AI? Shiriki kuthibitisha video hii

JamiiCheck

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
245
Reaction score
267
Mdau

Je, unaweza kutofautisha video halisi dhidi ya zile zilizotengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde?

Mtu mmoja alichapisha video hii hapa chini katika mtandao wake wa kijamii na kueleza kuwa tukio hilo limetokea Afrika. Kipande cha video ambacho kimeibua maswali mengi kwa waliyoiona kuhoji uhalisia wake.

Tushirikishe vigezo ama nyenzo ulizotumia kubaini uhalisia.

Uhalisia wa video hiyo

JamiiCheck imehakiki video hiyo na kubaini kuwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde.

Ufuatiliaji umebaini kuwa video hiyo ina matukio yanayokosa uhalisia ambayo yanadhihirirsha kuwa si video halisi.

Mathalani tukio la duma mdogo aliyenyanyuliwa juu na kubadilika kuwa kiumbe kingine. Rejelea pia tukio la Tai kung'atwa shingo lakini hakuna alama yoyote ya makovu ama damu ingawa manyoya yake ya shingoni ni meupe.

Aidha Tai huyo mwenye kichwa (Bald Eagle) cheupe asili yake siyo barani Afrika bali ni Tai mashuhuri huko Amerika ya Kusini hivyo kuhusianisha tukio hilo na bara la Afrika pia ni upotoshaji.
 
Mdau

Je, unaweza kutofautisha video halisi dhidi ya zile zilizotengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde?

Mtu mmoja alichapisha video hii hapa chini katika mtandao wake wa kijamii na kueleza kuwa tukio hilo limetokea Afrika. Kipande cha video ambacho kimeibua maswali mengi kwa waliyoiona kuhoji uhalisia wake.

Tushirikishe vigezo ama nyenzo ulizotumia kubaini uhalisia.
View attachment 3411951
Nafikiri inaweza kuwa imetengenezwa kwa AI mana ni kama huyo Chita mdogo alivyobebwa alipofika juu ni kama amebadilika
 
ni AI kwa sababu zifuatazo!
kwanza chui hawezi pita maeneo ya wazi hivyo anakuwa insecure
pili Kunguru hao hiwa wanasogea kama kuna nyama na hapo chui hata alama ya kuua na kuacha damu haijaonekana

Tatu chui mtoto aliyebebwa na Tai ghafla ameonekana ametulia pembeni kwa amani halafu amekuwa mkubwa kwa size ambayo hawezi bebwa na huyo ndege

ni ngumu sana kwa binadamu kuwa nje ya magari hivyo sehemu ambayo huyo chui yupo aggressive hivyo!
 
Background imebadilika magari yalikuwa sehemu ya wazi mwanzo mbeleni kukaonekana Kuna miti.

Pia background imecheza yaani imekuwa inayumba kama mawimbi ya bahari.

Tai anauwawa huku akiwa katulia tuli kama mdoli sekunde za mwishoni hapo.

Magari yamebadilika idadi na rangi za magari tofauti kati ya mwanzo na mwisho.

Sababu ya 🦅 kuanguka ni kaanguka mwenyewe huyo kaja kuvamia baadaye.

Hao washuhudiaji haijulikani wameshuka muda gani kwenye gari maana sekunde 11 ni chache sana, kuweza kuwa umeshuka kwenye gari Kisha uwe unarekodi tukio au unatazama kinachoendelea huku ukiwa na utulivu kama hao waliopo kwenye video.

Hiyo ni AI.
 
Background imebadilika magari yalikuwa sehemu ya wazi mwanzo mbeleni kukaonekana Kuna miti.

Pia background imecheza yaani imekuwa inayumba kama mawimbi ya bahari.

Tai anauwawa huku akiwa katulia tuli kama mdoli sekunde za mwishoni hapo.

Magari yamebadilika idadi na rangi za magari tofauti kati ya mwanzo na mwisho.

Sababu ya 🦅 kuanguka ni kaanguka mwenyewe huyo kaja kuvamia baadaye
Safi 👏
 
ni AI kwa sababu zifuatazo!
kwanza chui hawezi pita maeneo ya wazi hivyo anakuwa insecure
pili Kunguru hao hiwa wanasogea kama kuna nyama na hapo chui hata alama ya kuua na kuacha damu haijaonekana

Tatu chui mtoto aliyebebwa na Tai ghafla ameonekana ametulia pembeni kwa amani halafu amekuwa mkubwa kwa size ambayo hawezi bebwa na huyo ndege

ni ngumu sana kwa binadamu kuwa nje ya magari hivyo sehemu ambayo huyo chui yupo aggressive hivyo!
Safi👏
 
Video inaanza chui hadili na alipo ndege bali anadili na atakapoenda, AI
 
Kitu mojawapo ninachokizingatia ili kujua picha au video imetengenezwa kwa Ai ni kwa kuangalia background ya eneo husika pamoja na kuangalia mambo mengine ambayo hayapo kwenye main target YA picha/video husika.

Kwa kuzingatia hilo, naomba niseme hy video imetengenezwa kwa Ai
 
Back
Top Bottom