Je, unaweza kutoboa kimaisha (biashara) nje ya miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma?

Kwangu mimi mkoani ni kutafutia na Dar ni kutumia.

Naamini nje ya Dar options zipo
Nimeshatembea mikoa ambayo unajiuliza wafanyabiashara wanafanyaje? Mfano kigoma duka lipo town kati kodi yake ni 1 million kwa mwaka, asubuhi mpaka jioni wateja wa kutafuta. Sasa hapo kuna kutoboa au kupoteza muda tu
 
Mikoani fursa nimeona zipo za usafirishaji, udalali wa mazao, kilimo na ubaya zaidi ni kwamba ni kama ni saresare hizi fursa
 
Kijana kama una akili bora Ubuni biashara ukatawala baadhi ya miji nje ya miji mikubwa kama wakima Aboud ...Mapapa wa Dar wanajulikana sana ila sehemu nje ya mji kun vijana sio wa mtandao wapo wana progress nzuri...kuna mwanagu anapiga ishu za kuzalisha tambi na unga wa ngano alihama town yupo wilayani huko Muheza anakula pesa kajenga huko huko..

Yeye anasema mjini competition ni kubwa..Usichokijua jamaa anauza mpaka mikoani ikiwa yeye yupo Muheza ndan huko

. Kikubwa ni brand biashara unauza popote kama ni hivi viduka njaa vya Mangi & Mgosi hata Dar havilipi.
 
Hii ni nzuri maana ni mfano halisia.
 
Biashara ni neno pana, mleta mada kazingatia uchuuzi tu.
Lakini mkoani panalipa sana.
 
Nina ndugu yangu mwaka 2017 alikuwa na mtaji wa millioni 20 leo ana almost 300 millioni na yupo mkoa wa geita

Anyway labda yeye anaweza kuwa exceptional sababu ni msambazaji wa bidhaa fulani kwenye mgodi wa ggm geita

Binafsi mi naamini kokote ukipata chanel unatoboa hata kama ni pangani tanga.
 
Biashara ni neno pana, mleta mada kazingatia uchuuzi tu.
Lakini mkoani panalipa sana.
Mkuu, nifungulie nipate elimu pana kidogo tofauti na huo huo uchuuzi wa kuchukua bidhaa kariakoo na kusalia kuuza bei za juu kuna kipi utakifanya mkoani hasa vijijini kwa mtaji wa million 5-10.
 
Mkuu, nifungulie nipate elimu pana kidogo tofauti na huo huo uchuuzi wa kuchukua bidhaa kariakoo na kusalia kuuza bei za juu kuna kipi utakifanya mkoani hasa vijijini kwa mtaji wa million 5-10.
Kilimo ni biashara
Ufugaji ni biashara
Uvuvi ni biashara.
Kama una mtaji unaweza fungua kiwanda kidogo ukazalisha bidhaa yoyote na ukaiuza mjini
Mfano pale ikwirir, pwani kuna kiwanda cha yoghurts na soko lao lipo dar
 
Sawa mkuu, nimekuelewa
 
Ngoja nikusanue pesa ipo vijijini maporini uko hii ipo tangu ukoloni mpaka leo mjini hakuna masoko mjini bidhaa nyingi faida unaipata wapi na ndio maana enzi za ukoloni wazungu walijimilikisha maeneo yao ili waweze zalisha mali na wengine wakaenda porini kabisa kutafuta masoko hii njia mpaka leo wajanja wanaitumia

Huwezi kaa mjini kisa wewe bodaboda eti utatoboa kisa kila siku unavichwa

Uwezi kaa mjini ukatoboa kisa wewe chinga unauza soksi, leso, visu ukaona game yako

Uko vijijini ndio kuna badilisha maisha ya watu wa mjini, na waliopo mjini waliotoboa wametoka vijijini wakaja mjini baada ya kujua ramani, vijijini watu wanalima, wanafuga, wana masoko ya bidhaa

So wee kaa mjini endelea kushangaa magorofa mapya kila siku na magari mapya hizo ni products za uko vijijini

Hii nawambia hata vijana mliomaliza vyuo mnatafuta ajira uko vijijini kuna fursa kuna wilaya kibao hazina watalamu wa fans mlizonazo ukienda uko ukakomaa miaka mitatu ukajenga jina ukapata connection mjini unarudi kwa kuvimba

Sasa nyie endeleeni kukaa mjini tu mtakula rami
 
Tatizo vijana wa mjini wakiwa na uhakika wa kwenda kidimbwi kila weekend kunywa bia basi wanaona wametoboa, hapo ukute kapanga Hana hata title deeds, ana crown basi halafu mwenzake nyanda kabundi kule ana ng'ombe 300 anakaa Simiyu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sure arafu wakiugua wanaanza tuchangisha au kuweka card ya gari bondi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…