Je, unaweza kutoboa kimaisha (biashara) nje ya miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma?

Hakuna kama Dar,huko mikoani michosho tu Yani Bora waajiriwa wenye uhakika wa mshahara wa mwezi,ila Kwa mtafutaji sikushauri mikoani Bora upambane Dar,maana hao vijana wa mikoani wenyewe wanapaota Dar kila siku,wanaamini ndoto zao zitatimia Dar,ila lazima uwe na focus nzuri hard working,nidhamu ya pesa na kuzijua fursa.Dar,mwanza Kuna unafuu sana Kwa wapambanaji kuliko huko wilayani,vijijini mikoani fursa ya kilimo Cha kumtoa mtu sio hichi tunachodanganyana hapa kilimo chenye tija kinahitaji pesa(mtaji).
 
Hivi ndio nawaambia watu, miji mikubwa ina wafovour wapambanaji sana.
 
Hii nimeipenda sana mkuu haya maamuzu yakutoka mjini kuja kijijini ndo nmeyafanya Mimi Sasa,kwani nmekuja kijijini tangu mwaka Jana na raman huku ziko kibao ispokuwa tu bado sijakaa vizur kwenye mtaji but hayo yote unayosema ni kweli,nataman hata ningweza pata muwekezaji tukashiriana kwan huku Kuna hitaji huduma nyingi sana ispokuwa pesa kiupande wangu haija kaa tu sawa.....,ila vijijini Kuna fursa sana nyingi
 
Njoo Kahama uone vijana wadogo wametoboa vizuri sana kibiashara
 
Mkuu, nifungulie nipate elimu pana kidogo tofauti na huo huo uchuuzi wa kuchukua bidhaa kariakoo na kusalia kuuza bei za juu kuna kipi utakifanya mkoani hasa vijijini kwa mtaji wa million 5-10.
Kilimo, madini, viwanda vidogo kwenye ya viwanda vidogo wachina wajinufaisha nayo sana huko vijijini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…