Je, unaweza ukawa una vidonda vya tumbo na usipate maumivu ya tumbo?

Je, unaweza ukawa una vidonda vya tumbo na usipate maumivu ya tumbo?

Abdull hameed

Senior Member
Joined
Jan 29, 2025
Posts
126
Reaction score
230
Mambo vipi wana jamvi, naomba kuuliza, kwa uchache sana. Hivi unaweza ukawa una vidonda vya tumbo halafu usiumwe na tumbo? (usipate maumivu) kama ni ndio naomba kwa ufupi sana dalili nyengine za vidonda vya tumbo
 
Ni nyingi sana na hazihusishi tumbo kuuma mf:gas tumboni,kujamba mara kwa mara hasa ukila kidogo tu,kizunguzungu,kiungulia ,uchovu mwingi asubuhi na jioni,tumbo kuwa la moto,kukosa hamu ya kula,kupata shida ya kupumua hasa usiku
Sure..
 
Saa nyingine unaweza kuhisi unaumwa kifua upande wa kushoto juu ukafikiri ni moyo au wakati mwingine unaweza kuhisi hofu kali sana lakini hujui unachoogopa...
yani hii ndiyo shida yangu. tumbo haliniumi lkn nikinywa soda au dagaa au limao tumbo linajaa sana natoa sana ushuz nakuwa na hofu sana na sijui nahofia nini yani nakosa hadi amani.nilienda benjamini mkapa wakanipima wakanambia ni vidonda vya tumbo wakanipa dawa nyingi lkn zimedunda nahitaji msaada kwa kweli
 
Peke la paracgichi yaani ile mbegu ya ndani, katakata vipande vidogo vidogo, anika kwenye kivuli, then blend au twanga kwenye kinu.

Ule unga kijiko kidogo tumia kwa kuchanganya na asali asubuhi na jioni siku saba.

Pole
 
Hii mbinu nilipewa mahali mkuu hivi inasaidia au ,aliyewahi kutumia atume mrejesho
 
habari member. hakika juice ya cabage na majani ya mashona nguo n kiboko,nimetumia siku mbili nipo fresh sana gas tumboni kwisha kabisa japo pia nazingatia vyakula stak hizi coca
 
Back
Top Bottom