Je, unayafahamu maneno haya? Ni lugha gani?

Nguniani, majani ya maharage. Wanyakyusa wanaoenda kuchanganya na maharage au kuunga na karanga. Tukiwa Kantalamba secondary, ilikuwa siku ya ugali maharage, ili kupata "appetite" ya dona, sisi tunachuma hayo majani bustani ya shule, kwa kificho tunachemsha, tunachanganya na maharage. Alitufundisha mnyakyusa mmoja hivi ni CPA sasa hivi wakuitwa Mponjori. 😊
 
Matombolilo ni hatua ya ukuaji ya chura ambayo kwa kimombo yanaitwa Tadpole

huwa kama korokoro



Matakapela ni Maparachichi

Mafyurisi nayajua hivyo hivyo kama mafyurisi

Nguniani ni majani ya maharage, yani kama yale majani ya kunde yanavyoliwa basi kule mbeya majani ya maharage ndio dili na yanaitwa jina la nguniyani.

Sehemu za bush ndani ndani utakutana na wabibi fulani hivi wabishi wanayakausha hayo majani halafu yanakuja kutumika kipindi cha kiangazi ila awamu hii hayaitwi tena nguniyani, yanapewa jina jipya yanaitwa sansa.

Hayo yote ni maneno ambayo yanatumika kule Mbeya. Mfano huo mti wa mfyurisi ni nadra sana kule Isanga kuona ntyumba imekosa huo mti ndani.
 
Kinyengo - mpira
Mafyulisi - peaches
Mang'ang'a - berries
Matombolilo - vyura wadogo
Posolo
Katapera - parachichi
Nguniani - sikumbuki ila nalijua Hilo neno

Zamani nilidhani ni kiswahili kumbe ni kilugha 😅
Mpaka leo mafyulisi wanyaki wengi wanajua ni kiswahili.
 
Matombolilo ni viluwiluwi?
 
Mlikuwa mnapata virutubisho!
 
awamu hii hayaitwi tena nguniyani, yanapewa jina jipya yanaitwa sansa.
awamu hii hayaitwi tena nguniyani, yanapewa jina jipya yanaitwa sansa.
Sansa sio nguniyani ni majani ya kunde-Tbr-Shy
Nguniyani majani ya maharage-Mbeya
 
awamu hii hayaitwi tena nguniyani, yanapewa jina jipya yanaitwa sansa.

Sansa sio nguniyani ni majani ya kunde-Tbr-Shy
Nguniyani majani ya maharage-Mbeya
Ni kweli.
Nsasa ni mboga ya wanyamwezi na wasukuma (Majani ya kunde yaliyokaushwa), kuna nyingine wanaiita nswalu.
 
awamu hii hayaitwi tena nguniyani, yanapewa jina jipya yanaitwa sansa.

Sansa sio nguniyani ni majani ya kunde-Tbr-Shy
Nguniyani majani ya maharage-Mbeya
Labda uniambie majani ya maboga ila kunde hapana

Kwanza majani ya kunde kule Mbeya sio mchongo kabisa.
 
Ni kweli.
Nsasa ni mboga ya wanyamwezi na wasukuma (Majani ya kunde yaliyokaushwa), kuna nyingine wanaiita nswalu.
Kisukuma ni kipana sana sehemu nyingine wanaita lhumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…