Je, uongozi wa Roman Catholic ni 'ndumilakuwili' au huyu Papa tumepandikiziwa? Tutegemee nini?

Papa ni kiongozi TU na sio mkubwa kuliko kanisa
Mbona kanisa halipingi maagizo yake kama lina ukubwa?

Kwa nini kila akisemacho papa kina tekelezwa na waamini wote katika kanisa pasipo kuhoji au kupinga?

Yule Askofu wa Marekani aliyepinga mtazamo wa papa kuhusu kubariki mashoga mbona uteuzi wake ulitenguliwa?

Nakwambia hivi, Kanisa sio kubwa ila lina waumini wajinga na wapumbavu walio aminishwa kuto kuhoji maagizo ya huyo Papa.
 
Maamuzi ni mtu kufuata maandiko au mtu
 
.
Tatizo ni kwamba papa hajaamua mwenyewe, unafikiri papa peke yake anaweza kulisemea jambo nyeti kama hili bila msimamo wa kanisa? Think again.
 
Kanisa la matapeli Toka kitambo ila maskini hawajui hiki
 
Hili limenisikitisha sana kwa kweli japo nilikuwa najua litatokea siku sio nyingi baada ya kauli zake zenye utata, kuwa ushoga sio kosa
Pengine huu ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa Kanisa Katoliki
Kanisa katoliki halitakufa. Ni suala la muda tu madhehebu mengine yataunga mkono hoja wewe subiri utaona.
Anglikana siku nyingi walishahalalisha ushoga, hata maaskofu wao baadhi ni mashoga.
 
huyu papa ni C.I.A agent na wakala wa freemanson!!
 
Hili ni tatizo kwa kanisa katoliki.
Haliwezi kupita hivi hivi lazima lilete mpasuko mkubwa sana.
Wapo watakaohamia madhehebu mbalimbali.
Pia wapo wengi watakaokata tamaa nakuachana kabisa na mambo ya ibada za makanisani.
.
Nikushangaze? Watakaohama ni wachache mnoo kuliko unavyotegemea. Wengi watalalama tu lakini wataendelea kwenda huko kama kawaida.
 
Kanisa katoliki halitakufa. Ni suala la muda tu madhehebu mengine yataunga mkono hoja wewe subiri utaona.
Anglikana siku nyingi walishahalalisha ushoga, hata maaskofu wao baadhi ni mashoga.
Utakua ndio mwisho wa Ukristo huo.....Yatatamba haya makanisa ya akina Mwamposa na Gwajima
Ukristo umebaki Afrika, na hili ndio litakuwa pigo la mwisho
 
Utakua ndio mwisho wa Ukristo huo.....Yatatamba haya makanisa ya akina Mwamposa na Gwajima
Ukristo umebaki Afrika, na hili ndio litakuwa pigo la mwisho
Ukristo ndo wao wameuleta sisi tumeupokea tu. Sasa hivi wanaboresha ukristo wao sisi tunalalamika😀😀
Waachieni dini yao.
Dini ni utapeli tu kama ilivyo ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…