Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...
Nikweli mengi mazuei kayafanya.. yotebhayo nami naunga mkono. Ila pia sitamsahau wakati wa utawala wake kumpoteza mdogo wangu...
 
Nakumbuka na
Nitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha

1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia

2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini

3. Bila kujali kuwa watu wameshahudumu serikalini kwa muda mrefu na wanategemea kustaafu, akapitisha hoja ya uhakiki na kuwafukuza maelfu ya watu hao Huku akiwaacha bila kuwagusa wanasiasa na wateule wake katika hilo zoezi

4. Kubabikizia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatesa kupitia mfumo wa mashitaka na kuzisababishia familia zao maumivu makubwa na hali ngumu

5. Kuendelea kuwashikilia mamia ya masheikh walioko jela huku akisamehe wabakaji akina Babu Seya

6. Kukataa kuwapa watumishi wa serikai stahiki zao kwa wakati, ikiwemo kupandishwa madaraja na nyongeza za ishahara

7. Kuharibu chaguzi zote zilizofanyika chini ya serikali yake, kuanzia zile za marudio, serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Alidhuluu haki ya wananchi kuchagua viongozi wao

8. Magufuli alitunga sheria kandamizi, na kuvuruga misingi ya katiba. Kafanya kia jitihada kulifanya bunge liwe butu, kuiweka mahakama mfukoni etc

9. Magufuli alikuwa na kauli mbaya zisizo na staha mfano "sisomeshi wazazi, serikali siyo iliyoleta tetemeko, baki na mavi yako nyumbani, nitapiga mashangazi.. etc"

10. Alikuwa na miradi kadhaa au mpango wa miradi kadhaa ambayo ni white elephant mfano, uwanja wa ndege Chato, Midege,Mpango wa Uwanja wa mpira Chato

11..Magufuli alikuwa mdini, huhitaji kuwa mwanasayansi wa elimu ya jamii kuona kuwa teuzi zake ziliaia sana watu wa imani moja

12. Magufuli alikuwa haheshimu katiba waa sheria pale zinapokinzana na anachokitaka yeye, mfano haki ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa iliyokuwepo kikatiba hakuiheshimu

13. Magufulu hakuthubutu na wala hakujali kufanya uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na waliompiga risasi Lissu

Kwa hiyo mimi nakichukulia kifo cha Magufuli kama nafasi muhimu ili Taifa letu lipone.

Na sisi kama Taifa, tumeona kwa macho yetu namna katiba ya sasa ilivyokuwa hatari kama tunampata mtu mmoja asiyejali, ambaye ana element za udikteta, basi tuitumie nafasi hii kuliponya Taifa

Tangulia Magufuli, uwongo mbaya sitokumiss na sijawahi kukupenda kwa style ya uongozi wako, ninatamani Taifa lisipate Kiongozi mwenye mapungufu ya aina yako, ni mapungufu hatari kabisa
Maneno kuntu.
 
Rais wa ovyo, mbinafsi aliyependa kutukuzwa... Wajanja wakamjulia... wakamtanguliza...
Alitaka kwenda haraka haraka mwenyewe badala ya kuunganisha wengine na kuwa imara zaidi ili kwa pamoja tufike mbali zaidi...
Yako wapi sasa...
Ila wajinga wataona yeye ndo yeye...
 
Nitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha

1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia

2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini
Daah, umesahau dharau zake kuhusu korona ambayo imemfyeka
 
Nitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha

1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia

2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini

3. Bila kujali kuwa watu wameshahudumu serikalini kwa muda mrefu na wanategemea kustaafu, akapitisha hoja ya uhakiki na kuwafukuza maelfu ya watu hao Huku akiwaacha bila kuwagusa wanasiasa na wateule wake katika hilo zoezi

4. Kubabikizia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatesa kupitia mfumo wa mashitaka na kuzisababishia familia zao maumivu makubwa na hali ngumu

5. Kuendelea kuwashikilia mamia ya masheikh walioko jela huku akisamehe wabakaji akina Babu Seya

6. Kukataa kuwapa watumishi wa serikai stahiki zao kwa wakati, ikiwemo kupandishwa madaraja na nyongeza za ishahara

7. Kuharibu chaguzi zote zilizofanyika chini ya serikali yake, kuanzia zile za marudio, serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Alidhuluu haki ya wananchi kuchagua viongozi wao

8. Magufuli alitunga sheria kandamizi, na kuvuruga misingi ya katiba. Kafanya kia jitihada kulifanya bunge liwe butu, kuiweka mahakama mfukoni etc

9. Magufuli alikuwa na kauli mbaya zisizo na staha mfano "sisomeshi wazazi, serikali siyo iliyoleta tetemeko, baki na mavi yako nyumbani, nitapiga mashangazi.. etc"

10. Alikuwa na miradi kadhaa au mpango wa miradi kadhaa ambayo ni white elephant mfano, uwanja wa ndege Chato, Midege,Mpango wa Uwanja wa mpira Chato

11..Magufuli alikuwa mdini, huhitaji kuwa mwanasayansi wa elimu ya jamii kuona kuwa teuzi zake ziliaia sana watu wa imani moja

12. Magufuli alikuwa haheshimu katiba waa sheria pale zinapokinzana na anachokitaka yeye, mfano haki ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa iliyokuwepo kikatiba hakuiheshimu

13. Magufulu hakuthubutu na wala hakujali kufanya uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na waliompiga risasi Lissu

Kwa hiyo mimi nakichukulia kifo cha Magufuli kama nafasi muhimu ili Taifa letu lipone.

Na sisi kama Taifa, tumeona kwa macho yetu namna katiba ya sasa ilivyokuwa hatari kama tunampata mtu mmoja asiyejali, ambaye ana element za udikteta, basi tuitumie nafasi hii kuliponya Taifa

Tangulia Magufuli, uwongo mbaya sitokumiss na sijawahi kukupenda kwa style ya uongozi wako, ninatamani Taifa lisipate Kiongozi mwenye mapungufu ya aina yako, ni mapungufu hatari kabisa
Asante sana Mkuu.
 
Mweee. Ulitaka uchapwe bakora jichoni???
1. Ajira za walimu na madaktari zilikuwa zinatoka kila mwaka lkn awamu hii.
2. Hakuna nyongeza ya mshahara
3. Ukichelewa kwenye kituo cha kazi, unaweza kushangaa unawekwa lock up au afisa elimu akakuchapa viboko vya makalio
 
E government ni project ilianza toka enzi za kikwete , awamu ya 5 imekuja kuwa implemented tu.
Ni kweli lakini wakati wa JK waliihujumu lakini wakati wa Magu waliogopa maana Magu angewafukuza kazi
 
1.Mi namkumbuka Ubaguzi wake wa kidini Tanzania bara wakuu wa mikoa waislam hawafiki sita.
2.viongozi wa Ccm waliweza kuifanya kazi bila mipaka anaweza akamsweka Sello Daktari kisa yeye ni katika wa ccm wilaya.
 
KWELI KUFA UWE MZURI humu jf tumetukana,sana matendo yaliyokuwa yakifanywa na serikali kiasi kwamba hada uongozi wa JF ulikuwa bize ukifuta THREAD za matusi.
 
Kuminya uhuru wa habari mf: alizuia binge live kwa madai wananchi hawapati muda kufanya kazi cha ajabu akawa anaonekana yeye live kila anapoenda
 
Ukwepaji kodi ulipungua kwa kasi sana na janja janja zote za kukwepa zilitiwa kapuni. Aliinyoosha sana
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo kimsingi ilikuwa imeoza na kufifia kiutendaji. Kwa hili nampa big up maana huu ndiyo umekuwa msingi wa sasa kutamba kwa nchi yetu.
Japo hajaiboresha sana Mamlaka (to world class standards) lakini amejitahidi kuboresha baadhi ya vitu
 
Kuwaweka wafanyakazi wa Uma miaka 7 bila nyongeza ya mshahara wala kupanda daraja. Hili haliwezi kusahaulika

Huu ni uongo wa jumla, mimi na wenzangu tumepanda madaraja na kupata increments zetu kama kawaida.
Matatizo mengine ya kiutendaji na taratibu za utumishi zisikufanye ujumuishe hapo
 
Nitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha

1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia

2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini

3. Bila kujali kuwa watu wameshahudumu serikalini kwa muda mrefu na wanategemea kustaafu, akapitisha hoja ya uhakiki na kuwafukuza maelfu ya watu hao Huku akiwaacha bila kuwagusa wanasiasa na wateule wake katika hilo zoezi

4. Kubabikizia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatesa kupitia mfumo wa mashitaka na kuzisababishia familia zao maumivu makubwa na hali ngumu

5. Kuendelea kuwashikilia mamia ya masheikh walioko jela huku akisamehe wabakaji akina Babu Seya

6. Kukataa kuwapa watumishi wa serikai stahiki zao kwa wakati, ikiwemo kupandishwa madaraja na nyongeza za ishahara

7. Kuharibu chaguzi zote zilizofanyika chini ya serikali yake, kuanzia zile za marudio, serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Alidhuluu haki ya wananchi kuchagua viongozi wao

8. Magufuli alitunga sheria kandamizi, na kuvuruga misingi ya katiba. Kafanya kia jitihada kulifanya bunge liwe butu, kuiweka mahakama mfukoni etc

9. Magufuli alikuwa na kauli mbaya zisizo na staha mfano "sisomeshi wazazi, serikali siyo iliyoleta tetemeko, baki na mavi yako nyumbani, nitapiga mashangazi.. etc"

10. Alikuwa na miradi kadhaa au mpango wa miradi kadhaa ambayo ni white elephant mfano, uwanja wa ndege Chato, Midege,Mpango wa Uwanja wa mpira Chato

11..Magufuli alikuwa mdini, huhitaji kuwa mwanasayansi wa elimu ya jamii kuona kuwa teuzi zake ziliaia sana watu wa imani moja

12. Magufuli alikuwa haheshimu katiba waa sheria pale zinapokinzana na anachokitaka yeye, mfano haki ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa iliyokuwepo kikatiba hakuiheshimu

13. Magufulu hakuthubutu na wala hakujali kufanya uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na waliompiga risasi Lissu

Kwa hiyo mimi nakichukulia kifo cha Magufuli kama nafasi muhimu ili Taifa letu lipone.

Na sisi kama Taifa, tumeona kwa macho yetu namna katiba ya sasa ilivyokuwa hatari kama tunampata mtu mmoja asiyejali, ambaye ana element za udikteta, basi tuitumie nafasi hii kuliponya Taifa

Tangulia Magufuli, uwongo mbaya sitokumiss na sijawahi kukupenda kwa style ya uongozi wako, ninatamani Taifa lisipate Kiongozi mwenye mapungufu ya aina yako, ni mapungufu hatari kabisa
Nashukuru sana
 
Kwa kweli sijafurahi kabisa kumpoteza kiongozi mahiri kama john pombe magufuli alikua hodari sana katika uongozi wake mianya ya rushwa alikomesha, uonevu, huduma katika taasisi za kiserikali zilikua zikitolewa kwa heshima na bila ubaguzi, kajenga miradi mingi sana nchini, elimu bure, miundombinu, hudumu hospitalini ziliboreshwa, huduma za maji mikoa mbalimbali alitoa fedha miradi ikamilishwe, uwanja wa ndege wa mwl Julius Nyerere aliukarabati kwa ufupi Rais wangu kifo chako John Pombe Magufuli umeniachia simanzi moyoni mwangu,
Unaposema hujafurahishwa na kifo chake kwahiyo unamtuhumu Muumba aliyemtwaa! unamtunishia msuli Mungu! unasema kakosea! kwamba angemchukua nani! kwahiyo Mungu amekuudhi! we fanya tu ku celebrate kifo cha hayati
 
Back
Top Bottom