Magufuli angeendelea kuepo sidhani kama nchi ingekuwa bado ipo hii ! He was a maniac!!
 
Hofu ilikuwa juu sana na uhuru wa kujieleza uliwekwa kapuni, nchi ilikuwa inajizamisha kwenye udikteta taratibu. Kupotea na kupigwa risasi hadharani watu kama Lissu kulitosha kumfanya Mungu aingilie kati.
Mkiendelea kujidanganya kwamba Mungu aliingilia kati ni utoto kabisa.
Babu,Bibi au Baba na Mama yako waliokufa ni Mungu aliyeingilia kati?
 
mkuu unaishi zambia?
 
Kwa nini mnasingizia sana matukio?
Mara mnasingizia Covid, mara mnasingizia Vita. Komaeni basi japo kidogo.
COVID ilianza mwaka 2019, lakini JPM aliingia madarakani mwaka 2015.
 
Ni kukosa ujasiri wa viongozi . Mafuta ya Urusi kwanini asinunue mbayo yana bei ndogo kwa ajili ya kukosa soko?
Hizo sababu si za msingi.
Tumepiga kura ya kutokuwa upande wowote wakati wa maazimio juu ya Urusi lkn bado tuko ndani ya boksi la vikwazo na tunaunga mkono . Huu ni UNAFIKI. Hatueleweki na Ulaya iliyoweka vikwazo maana hatukuwasapoti.
Wala hatueleki na Urusi maana tunatekeleza vikwazo. Whata shame. India , China zimetumia kura zao vzr.
 


Hakuna cha JPM wala nini ni kutokujua mambo kwa wengi kama wewe

1. Bei ya mbolea imepanda Duniani kama ilivyo ya mafuta na tanzania wakati wa JPM hatukuwa tunatengeneza mbolea bali tulikuwa tunaagiza. Sasa je JPM angepata wapi mbolea kwa bei ya chini ambayo kwasasa wanashidwa kupanda. Angalau sasa kuna kiwanda kinajegwa Dodoma
2. Bei ya mafuta imepanda Dunia nzima hapa Texas mafuta yalikuwa $2.5 kwa gallon wakati wa Magufuli sasa ni $4.99 sasa hii ni Dunia nzima unafikiri JPM angewezaje kupunguza nauli au kuwaamrisha wenye magari wapate hasara. Kupunguza makati Mama Samia ametoa ruzuku kwenye mbolea na Mafuta kitu ambacho hata JPM hajafanya

Tumpe JPM sifa za ukweli sio uzushi kama huu.
 
Ungejua kinachowafanya viongozi wa ulaya kujiuzuru huu Uzi usingeunzisha,
Binafsi nachoshukuru PUTIN katuondolea korona
 

Refinery ya kusafisha mafuta ya Urusi tunayo?
 
Hofu ilikuwa juu sana na uhuru wa kujieleza uliwekwa kapuni, nchi ilikuwa inajizamisha kwenye udikteta taratibu. Kupotea na kupigwa risasi hadharani watu kama Lissu kulitosha kumfanya Mungu aingilie kati.
Hofu ilikuwa kwa WAPIGAJI, WEZI, MAFISADI na wasio na UZALENDO.
Issue si kupigwa risasi au kutekwa.
Issue ni kwa nini yule au wale wametekwa na mimi na huyu hatujatekwa?
Kwa nini awe yeye au wao tu na wala si mtu au watu wengine?
Unadhani wewe ambaye hukutekwa walishindwa kukuteka?
La hasha. Hawakushindwa isipokuwa wewe hukuwa na sifa za kutekwa.

Kwa mfano, mtu mmoja anaiba fedha za ambazo zingetosha kununulia madawa Hospitalini. Je, ni watu wangapi watakufa kutokana na kukosa dawa?
Je, mtu wa namna hiyo akipigwa makofi kutakuwa na kosa gani?
 
Ni unafuu gani uliupata kwa Magufuli? Hivi umesahau Magufuli alikuta Kilo ya Sukari ni Tsh 1,800 akaivuruga ikafika mpaka Tsh 5,000 ?? Ilipoteremka ikagota Tsh 3,000.

Kuna watu wamepata hasara biashara ya korosho mpaka leo wamefilisika, kweli umesahau kuwa ni Magufuli ndiye alitibua?

Hivi alivyomfilisi Yusuf Manji ulitegemea wale wafanyakazi zaidi ya 3,000 wa Quality Group waende wapi? Ndiyo machinga wa mtaani unaowaona

Mbona hili Taifa lina wapumbavu wengi kiasi hiki?

Mwacheni Samia apige kazi hata kama mnamchukia mumchukie yeye binafsi lakini kazi yake ni TAKATIFU
 
Hofu ilikuwa juu sana na uhuru wa kujieleza uliwekwa kapuni, nchi ilikuwa inajizamisha kwenye udikteta taratibu. Kupotea na kupigwa risasi hadharani watu kama Lissu kulitosha kumfanya Mungu aingilie kati.
Lisu ndio mdudu gani na wewe?

Kuna watu 7 wa familia moja wameuawa wote kule kigoma juzi tu hapa, alafu unatuletea ngonjera za Lisu?
 
Mbona lipo wazi kua Hayati Magufuli , aliteuliwa na Mungu kwaajili ya Watanzania !!.


Kipande Cha sabuni Cha mia 300, saizi ni mia Tisa
 
Tumekuelewa,shukrani sana.Umetoa ufafanuzi mzuri.Kama ni Mwalimu au mkufunzi au Mhadhiri,mbali na kusomea uawalimu pia una kipaji,cha ualimu,ukufunzi uhadhiri.Mungu akubariki sana.
 
Umeandika ukweli mtupu.
 
Enzi zake kengele ya nguvu ya dola ilililia kwenye mind ya kila mtu. Alivaa vilivyo viatu vya mamlaka yake. Maamuzi yake bila kujali usahihi wake yalikua na nia njema kwa wananchi wote
 
Hatuna petrol refinery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…