Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Mkuu usizunguke kwa ajili ya kujitahidi kuuremba uongo kuwa ukweli.
Magufuli alifuata haki alichukuwa Kodi kwa usawa kwa wote. Tofauti na malalamiko ya sasa ambapo matajiri wanakwepa Kodi na masikini wanakamuliwa zaidi, sababu masikini hawezi kukwepa Kodi, hana ujanja huo.
Kosa la Magufuli ni kuanza kuchukua Kodi kwa Wakubwa ambao hawajazoea kulipa Kodi, hii ikawastua na kuanza kupiga mayowe.
Mtu akiwa Masikini ndio asilipi Kodi?
Mtu akiwa Masikini ndio asitoe Zaka?

Hakuna kitu Kama hicho.
Kodi iwekwe katika mfumo wa percentage.
Kama ni 10%
Basi Masikini mwenye Tsh 1000/= atatoa Kodi Tsh 100/=
Tajiri mwenye 1,000,000/= atatoa 100,000/=

Magufuli alikuwa kiongozi ambaye alitaka kuleta ubaguzi katika ujenzi wa Nchi. Alitaka kuwapendelea Masikini Jambo ambalo Kwa Kiongozi sio sifa njema.

Biblia inasema;

Kumbukumbu la Torati 25:13
Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako.

Kumbukumbu la Torati 25:14
Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako.
Kumbukumbu la Torati 25:15
Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 25:16
Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

Kodi lazima kila mtu alipe Kwa uwezo wake. Zikiletwa Tozo kila mtu alipe Kwa uwezo wake.
Sio huyu alipe alafu mwingine asilipe.

Biblia inamaliza Kwa kusema;

Mambo ya Walawi 19:15
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.

JPM amepumzika tuache apumzike lakini kuhusu clip hiyo Hakuwa sahihi, kwamba mtu akiwa Masikini basi ndio apendelewe au asikupe Kodi kisa umasikini wake.

Kodi iwekwe katika mfumo rahisi na nafuu Kwa kila mtu, katika namna ya percentage.
Ukiuza mchicha wa Buku basi hamsini iwe Kodi. Fresh.

Huko kunaitwa kuwajibika
 
Simba wa yuda hapana kabisa kwani hakuwa kiongozi bali alikuwa mtawala na laiti kama angefika mwisho wa uongozi wake hali ingekuwa tete sana.Na mbaya zaidi u-rais aliufanya ni wake na sio taasisi kama ilivyo sasa chini ya jemedari wetu Mh SSH.Simba kila kitu alifanya mwenyewe yaani dereva yeye,konda yeye na fundi yeye pia na mbaya zaidi hakuwaamini wateule wake na mbaya zaidi hadi kufikia kusema"I WISH I COULD BE IGP"
 
Mkuu usizunguke kwa ajili ya kujitahidi kuuremba uongo kuwa ukweli.
Magufuli alifuata haki alichukuwa Kodi kwa usawa kwa wote. Tofauti na malalamiko ya sasa ambapo matajiri wanakwepa Kodi na masikini wanakamuliwa zaidi, sababu masikini hawezi kukwepa Kodi, hana ujanja huo.
Kosa la Magufuli ni kuanza kuchukua Kodi kwa Wakubwa ambao hawajazoea kulipa Kodi, hii ika
SASA HIVI MATAJIRI WANA KWEPA KODI, WANAFANYA MAGENDO .
 
Asante sana ndugu mwananchi.
2022-06-16_10.18.21.jpg
 
..Kwa hiyo Mkuu Hawa wanaofuata Sheria na Kukutoza ovyo Tozo ndio Viongozi Wazuri? Hawa wasiotaka Katiba Mpya??
Mada hii inamhusu magufuli.. hata hivyo ajenda ya tozo na kupandisha bei za vifurushi zilianzia kipindi kile magufuli akiwepo.

Nataka viongozi na wananchi wote tuheshimu katiba na sheria.

Kwani magufuli aliitaka katiba mpya?
 
Wala leo sisalimiii, maana najuaa kichwa cha thread hii ni salamu toshaa

Wazalendo wakweli embu njoeni tuweke mafanikio ya JPM,

Mimi naanza na KUHESHIMIANA kwa watanzania bila kujali cheo, kabila, fedhaa na zingine kedekede.

Miundombinu alizoasisi na zingine nyingi ujenzi unaendelea wala sihitaji kujua maana wewe unayesoma unajua,

Kulinda RASILIMALI ZA NCHII HADI CEO wa BARRICK kufunga safari hadi Dar es salam

Tafadhalii kama huna cha kukoment usitie neno humu
 
View attachment 1734652
Picha: Hayati Rais Magufuli enzi uhai wake

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti (Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss, kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo.

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje, kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu, S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
USILOLIJUA SAWA NA USIKU WA GIZA , INAONEKANA WALA HUWAJUI VIONGOZI ULIOWATAJA. KASOME TENA HISTORIA ZAO NA WALIYOFANYA UJIONGEZEE UELEWA
 
Back
Top Bottom