Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
National hero ni Hamza pekeee yake aliyesimamia kidete kupinga unyanyasaji.
Kabla yake, kipindi chake na baada ya yeye kuondoka kuna tofauti kubwa sana! Wengine mpaka ganzi imeisha ndio tumeanza kusikia maumivu[emoji24]
 
John Pombe kaniachia tatizo kubwa

SIKUJUA NI VIGUMU KIASI GANI KUPAMBANA NA UNENE....hata nisipokula nanenepa, juisi wiki nzima nanenepa kila nikukumbuka siko chini yake...mwili unaongezeka tu.

Dah: Sijui afufuke ili nikondeane kama mwanzo....unene unanipotezea shape yangu jaman
Deal zako Sasa zimefunguka,mnapiga tu kama hakuna Serekali vile,utaacha kunenepa Mwana!!??[emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli hakuwahi kusafiri nje ya Africa na wala hakupandisha gharama za maisha lakini alifanya yafuatayo.............[emoji116]

1. JPM anajenga Reli ya Mwendo kasi – SGR.
2. JPM anajenga Bwawa la Umeme – Nyerere HydroPower.
3. JPM amenunua Ndege 13 aina tofautitofauti.
4. JPM amejenga Ikulu kule Dodoma na yale Magorofa ya Wizara kule Mji wa Serikali Dodoma ( Mtumba) Magufuli City
5. JPM amehamisha Makao Makuu ya Serikali na ameijenga Dodoma imekuwa Jiji
6. JPM amejenga FlyOver Dar es Salaam pale Ubungo na TAZARA.
7. JPM amejenga daraja la Tanzanite pale Selander.
8. JPM ametengeneza huu Mfumo wa Kompyuta wa Malipo ya Serikali.
9. JPM alikuwa anaweka umeme hadi Vijijini (kwa Tsh. 27,000/= tu.)
10. JPM ameshawishi Bomba la Mafuta kutoka Uganda lipite Tanzania.
11. JPM anajenga daraja la Kingongo Ferry Busisi kule ziwa Victoria.
12. JPM amejenga Meli kubwa mbili mbili kila ziwa, yaani Ziwa Victoria 2, Ziwa Tanganyika 2 na Ziwa Nyasa 2.
13. JPM amejenga Hospital za Kanda kubwa nne… Dodoma, Mara, Mtwara, Geita na Songea
14. JPM amejenga Hospitali za Wilaya Zaidi ya 70
15. JPM amejenga Mradi Mkubwa wa Maji ya Victoria kule Tabora
16. JPM amejenga Mradi wa Maji Mkubwa Arusha
17. JPM amejenga Barabara ya Njia Nane Dar es Salaam hadi Kibaha
18. JPM alikuwa anajenga Mizani za Kisasa kabisa Kwenye Barabara zote kubwa
19. JPM amejenga Vituo vya Afya Zaidi ya 500
20. JPM amejenga na Kununua Rada 4 za AirPort
21. JPM amejenga Viwanja vya Ndege Mara, Iringa, Mbeya, Chato, Songea na Rukwa
22. JPM amejenga Masoko ya Madini kila Mikoa yenye migodi ya madini
23. JPM amejenga ukuta wa Mirerani na kuweka Camera za Ulinzi
24. JPM amejenga Bandari Kilwa, na kuzipanua Bandari Mtwara, Tanga na Dar es Salaam
25. JPM amejenga Masoko ya Kisasa zaidi, ya maana kama Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam
26. JPM amejenga Bus Stand za Kisasa Zaidi mikoani kama Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam
27. JPM amenunua Vifaa Tiba kama MRI, CT Scan, Vifaa vya Kufanyia Oparations za Moyo pale JKCI Wagonjwa wanatoka nchi jirani kuja kutibiwa.
Huwezi amini yaani! Mpaka unasisimka kutaka kuendelea kujua na vingine umeviacha!

- Wazungu walikua wanakuja kutalii kipindi cha corona

- Hakukua na lockdown kipindi cha corona kitu ambacho karibu dunia nzima ilikua imejificha ndani ila tz tulikua tuna puyanga huku na huko kutafuta chochote kitakacho wezekana, na angetutia lockdown tungeisha maaninah

- tembo walianza kuongezeka na wanyama wengine waliokua wanawindwa kiholela

- madawa ya kulevya yalikua ya moto na mateja walipungua kwa kiasi kikubwa

  • maji yalikua haya katiki hivyo
  • umeme ulikua online mda wote

- tulikua na adabu 12 sio sasahivi kila mtu ni usalama wa taifa, unaporwa haki zako hadharani na huna pakwenda kushtaki

- kulikua na ujenzi kila mahala hivyo kulikua na kazi nyingi kuliko sasahivi

- machinga na mama ntilie watakua wanaelewa sshv nini kimewapata

- na mengine meeeeeengi

Ubaya wake huyu ndugu ilikua ni matumizi ya mahakama, polisi na bunge kitu ambacho kilikua hakimbuguzi mwananchi moja kwa moja bali yeye alikua anatafutana na wakutafutana nae tu usiombe uwe kwenye target yake ujue umesha enda na maji
 
ndani ya miaka mitano na miezi kidogo aliyokaa ikulu,Rais Magufuli alifanya Mambo makubwa ambayo Marais wa nne kabla yake walishindwa kufanya,kama Rais wa Malawi alivyosema siku ya msiba wake,"No body new Magufuli was coming,and no body new Magufuli was going, Magufuli himself new he had little time,he did everything like he was in a rush to go somewhere,thank you President John Magufuli"

Hakika Mungu alitupa zawadi,na sasa zawadi hiyo ameichukua mfano wa Musa na wana wa israel kutoka misri.
Katika harakati za Musa kumtafuta Mungu arekebishe mambo,Aliinuka Haruni,raia wakamzidi nguvu akawatengenezea ndama sawasawa na matakwa yao(Wengi wape)

Tunamsubiria Yoshua aendelee na kazi,mengine yote ni kipindi cha mpito.Kanaani ni lazima tufike.
"No body new Magufuli was coming,and no body new Magufuli was going, Magufuli himself new he had little time,he did everything like he was in a rush to go somewhere,thank you President John Magufuli"[emoji848][emoji22][emoji22][emoji24][emoji24]
 
Atakayekulaani na kukudhihaki atalaaniwa kabisa na atakayekutetea wazi wazi atabarikiwa hakika.
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

Matendo ya mtu huwa wazi, nayo humpeleka mtu kwa yule amtumikiaye.

Kuua, kuteka, kudhulumu, ulaghai na ghiliba, ni matendo ya shetani. Naye ayatendayo hayo huuinua utawala wa shetani maana ndjo autumikiao.

Matendo ya wenye haki ni wazi na dhahiri, nayo ni upendo, hekima, kiasi, fadhila na huruma. Hawa ndio watakatifu wake Mungu, nao humwinua Mungu kwa maisha yao ya fadhila na upendo.
 
Aliuza nini hadi akapate pesa zote hizo na je kodi iliyotozwa toka kwa Watanzania ilifanya kazi gani?
Ndio ujiulize! Alikuja kutufungua macho na kutufanya tujielewe kua tuna nguvu gani, kumbe tuna nguvu tofauti na tunavyo jifahamu
 
Atakayekulaani na kukudhihaki atalaaniwa kabisa na atakayekutetea wazi wazi atabarikiwa hakika.
Watalii.jpg

Picha haihusiani na Habari
 
mtu akivaa suti akaja kwenye tv akaanza kumsema makufuli huyo mtu huwa anaonekana yupo uchi ila yeye hajijui, kiongozi mwenye heshima akikosa ajenda akaanza kumsema makufuli huwa anaonekana kama mbeba magunia. chadema na vyama vya upinzani tangu mlipo ruhusiwa na mama kufanya mikutano ya hadhara mmeona sifa kumpa zawadi ya kumsema makufuli kila mnapoalikwa kwenye mahojiano kwenye media zote hamtaki kuongelea vyama vyenu vitaifanyia nini tanzania mmekaa kumsema jpm mwanzo wa kipindi mpaka mwisho sasa nawaambieni majukwaa yenu baada ya muda mtakosa watu watabaki manyumbu kama nyinyi na huyo nabii wenu lisu ndio anakuja yeye hana jipya ataanza kumsema jpm mwanzo mwisho utafikiri aliwachukulia wake zenu
Kwani kumsema muuaji si jambo jema? Shetani tunamsema kila siku. Na huyu wakala wake atasemwa kila siku kwa maovu yake.
 
1. "Hawa wanaoropoka ropoka huko bungeni wafukuze watoke huko na wakija huku nje 'I will deal' with them...
Mimi jkinishauri, ndiyo umeharibu. Sishauriwi, mimi ni jiwe.

Wewe mpina nimekuteua kuwa waziri wa uvuvi ukapambane na wavuvi, maana wewe ni kichaa kama mimj.
 
Magufuli ndio mfano wa kiongozi anaehitajika katika nchi za Africa.

Alikuwa kiongozi asiependa masihara linapo kuja swala la uwajibikaji.
Mtu aliejitoa muhanga kuipambania nchiyake bila kujali maadui wa ndani na nje.

Wachache wanao mdhihaki na kumsingizia mambo ya uovua ni kama wale waliokuwa wakishangilia kuteswa na kuuwawa P.Limumba wa kongo miakaile.

Lumumba alikamatwa akateswa na kuuliwa na waasi kwa mpango ulioratibiwa na Wabelgiji nchi anayo ishi lisu.

Wasaliti ni watu wabaya sana.
 
Ndio ujiulize! Alikuja kutufungua macho na kutufanya tujielewe kua tuna nguvu gani, kumbe tuna nguvu tofauti na tunavyo jifahamu
Alikuwa mpiga dili tu,alianzisha miradi mingi kwa gharama za juu apate kuiba.
Amini nakwambia gharama za miradi haziendani na thamani halisi na itatutesa kwa miaka mingi sana.
 
Mkuu, kitabu huwa hakifungwi, ndo maana huwa kuna tarehe kila mwaka kuwakumbuka Viongozi.
Mfano, tarehe 14, October nk.
Unam-beep God, unataka afunge kitabu chako ndio ujue kinafungwaga. Hiyo kumbukumbu unayoisema wewe, ni historia ndio iliobaki. Kile chenyewe ni bye bye hakuna kurasa mpya zitakazojitokeza
 
Kwa kweli ukipita hii barabara lazima ukumbuke jitihada za rais magufuli kufanikisha huu ujenzi wa barabara. Kwa sasa foleni imeisha kabisa hii barabara.

Pumzika kwa amani mzalendo. Tunaamini watanzania ungekuwa bado hai ungefanya makubwa zaidi ya ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom