Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Mengi yameandikwa juu ya utawala wa Marehemu Rais Dr. John Pombe Magufuli. Mimi binafsi nakili kuwa ingawa wengi wamemnanga kuwa alikuwa katili na hana huruma wakitolea mfano kuhusiana na kauli zake kwa ndugu zetu wa Kagera baada ya tetemeko kama ndio mfano hai; hata hivyo nadhani kuna mambo fulani aliyatekeleza ambayo yalikuwa na faida kwa nchi hivyo warithi wake hawana budi kuyaendeleza.

Marehemu alikuwa hana msalie Mtume kwenye suala la kukusanya kodi ingawa mbinu zake zilikuwa hazina utu lakini pia alihakikisha kuwa kodi iliyokusanywa ilikuwa haitumiki hovyo hovyo na ndio maana aliagiza mambo yafuatayo ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa Serikali na Taasisi zake:

1. Alipiga marufuku safari za nchi za nje zilizokuwa zinatumia fedha nyingi bila tija na hasa safari za wabunge . Hizi Ndio safari wakina Ndugai walikuwa wanapiga mabilioni!

2. Alipiga marufuku utamaduni uliozoeleka hasa wakati wa utawala wa Kikwete wa mtu mmoja kuwa na vyeo zaidi ya kimoja. Kwa Mfano mtu mmoja anakuwa RC halafu huyo huyo anakuwa mjumbe wa NEC etc. Mtu mmoja anakuwa Mjumbe wa bodi za mashirika zaidi ya moja!

3. Alipiga marufuku seminar za wafanyakazi serikalini na mashirika ya umma kufanyika kwenye mahotel makubwa na badala yake wafanyie kwenye kumbi zilizoko kwenye maofisi yao. Hili la seminar Rais Samia aliangalie sana kwani wameishaanza kumchezea hijab kwa kusema sasa ameruhusu seminar!!!

Haya yalikuwa ni maamuzi ambayo hayana budi kuendelezwa ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa matumizi mabaya ya kodi zao!
Kazee kalikuwa kajinga sana kale!
 
Mleta mada, ninachokumbuka kabla Magufuli haijaingia madarakani ni kwamba hayo yote uliyoyaorodhesha yalikuwa yakipigiwa kelele sana na Chadema na vyama vingine vya upinzani

Wakasema Serikali ya JK inadili na vidagaa ktk ishu ya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi ila mapapa wanaachwa wanadunda mtaani

Ila Magu alipoingia Ikulu na kuanza kuchukua hatua, Chadema wakasema jamaa anaiga yaliyo katika Ilani yetu

Alipoanza kudili na mapapa kama kina Habinder Seth na wengne ktk rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi Chadema wakasema Jpm anabambikia watu kesi na kandamiza haki za watu

Kwa kifupi, kuna baadhi ya vyama vya siasa na wananchi ni kama vinyonga au mbayuwayu
 
mbona yeye alikuw na vyeo vingi Rais ,Mwkt wa Ccm ,Amir jeshi mkuu na mwekiti wa EAC. kwann asingeachia kimoja hapo.
 
Chato siyo mji wa wasukuma
............Vyovyote ilivyo cha kujiuliza alifikiria nini kwenda kujenga international airport sehemu ambayo hata miaka 300 ijayo mbele hakuna uhakika kwamba ingehitajika uwepo wake pale?
 

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.


Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Kutuletea watu wasiojulikana
 
Jana usiku nilienda kumtembelea mzee mmoja ambaye ni mtu wangu wa karibu anae jihusisha na biashara ya madini,akinipa story fupi tu ya rafiki yake ambayo ilinihuzunisha sana.

Jamaa yake alikua na zaidi ya bilioni 7 kwenye account yake bank mwaka jana mwanzoni,alipigiwa simu na branch manager aende urgently na alipofika pale mida ya mchana akajulishwa kwamba account yake imepigwa spana na tra (task force). Ikabidi aende tra mkoa ili kufuatilia hiyo ishu.

Tra mkoani wakamwambia inabidi awasiliane na TRA makao makuu,ikapigwa sim akapewa appointment saa tatu asubuhi next day. Akapanda ndege jioni hiyo kuelekea huko, asubuhi kafika mapema kasechewa kweli kweli then akaingia ofisini kuzungumza na team roho mbaya.

Wewe ndio fulani? Ndio, inaonekana una pesa nyingi sana kwa account ila hulipi kodi. Jamaa akasema akasema kodi nalipa na ninapata tax clearance kila mwaka mbona sielewi? Wakamwambia ana option 2 TRA wachukue 5B wamuachie 2 au akalete vielelezo huku wakiendelea kuzuia hela zote. Vielelezo visipo jitosheleza watachukua hela zote pamoja na kesi ya uhujumu uchumi.

Pale ulikua huruhusiwi kwenda na mwanasheria wala accountant,jamaa akatoka nje kufikiria kwa muda akaona isiwe nongwa akawaachia 5B lakini pia akaambiwa arudi CCM kwa kujitangaza kwenye media kwa sababu alikua supporter mkubwa wa lowasa uchaguzi wa 2015.

Matajiri wengi wa mawe wameumizwa sana huko kanda ya kaskazini ila wamekaa kimya tu,bora huyu jamaa amekufa maana alikua anatupeleka shimoni/motoni kiuchumi na kijamii.
Kuiba Pesa za watu napo kumechangia kumpoteza.Unakula vipi pesa ya mtu pesa zingine za majini mtu kaingia mkataba na shetani pesa zimetoka kwenye benk za majini,wanakushtakia direct kwa shetani umemzulumu pesa zake hapa unategemea nn utaponea wapi.Umepora pesa za mikataba.
 
Nitamkumbuka kwa:
1. Wasiojulikana
2. Ukabila
3. Kutoheshimu katiba
4. Kuwatesa wakosoaji wake na hata kuwapoteza au kuwaua.
5. Kujimilikisha mamlaka yote ya nchi. Kila kitu ni mpaka aseme yeye.
6. Unyama kwa majirani mfano kuchoma vifaranga vya Kenya na kuuza mifugo yao.
7. Ushamba wa kutozingatia weledi katika teuzi zake
8. Kujenga nchi ie barabara, madaraja, ununuzi wa ndege japo zimeleta hasara kubwa kwa Taifa, upanuzi wa bandari, viwanja vya ndege, SGR, Stiglers Gorge nk
9. Upendeleo wa Chato.
10. Kuwachukulia wanawake kama watu hafifu, vyombo vya starehe (rejea kauli zake kuhusu wanawake)
11. Kutojali maumivu ya anaowaongoza (kuongoza kwa kuburuza watu)
12. Unafiki mfano alikuwa anasema maendeleo hayana Vyama wakati mkichagua upinzani anawatisha hadharani kuwa hataleta mradi wowote wa maendeleo.
13. Hofu ya kupinduliwa.
14. Double standards kwa wateule wake. Wengine wakikosea kidogo tu wanatumbuliwa, wakikosea wapendwa wake anawatetea.
15. Kuwajengea ujasiri Wananchi kipindi cha Korona
16. Misimamo isiyoyumba hata kama ni ya kijinga.
17. Kufilisi wafanyabiashara.
18. Kutumia dola kuvuruga uchaguzi mkuu wa 2020 na ule wa serikali za mitaa 2019.
19. Kuiba rambirambi na michango ya maafa.
20. Kutunga sheria kandamizi zinazokinzana na katiba ya nchi.
21. Kulinda raslimali za nchi.
 
Miaka 6 ya utawala wa Mwendazake ilikua ya Machozi, Jasho na Damu kwa Watanzania. Haya ni baadhi ya matukio niliyoyakumbuka kwa haraka, baadhi yalitokea nikiwa huko nyumbani na mengine yametokea nikiwa nimeshaondoka.

1. Alizika uhuru wa vyombo vya habari na kutia saini sheria kandamizi kwa vyombo vya habari. Vyomno vyote vililazimishwa kumuandika kwa kumsifu na kumpamba, kilichothubutu kumkosoa kilifungiwa.

2. Alitumia nguvu nyingi kupambana na upinzani na kutesa wanasiasa wa upinzani kwa kuwafungulia kesi za uongo mpaka leo bado wengi wapo jela kwa kesi za kisiasa za kubambikiziwa.

3. Aligawanya nchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na udini na ubaguzi wa kijinsia. Serikali yake ilijaa watu wa kanda ya ziwa na 75% ya serikali yake ilijaa wakristo.

4. Alikua na ubaguzi wa kijinsia na aliendekeza mfumo dume. Wanawake walikua 17% tu ya mawaziri katika serikali yake.

5. Alihakikisha wakuu wa vyombo vya ulinzi wanatoka kanda ya ziwa ili kumlinda likitokea lolote, CDF - Mara, IGP - Mara na CGP - Geita na CGF - Mwanza. Madikteta wote hufanya hivi maana wanajua watu wa kwao hawawezi kuwageuka.

6. Hakupandisha mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa miaka yote 6 ya utawala wake.

7. Hakutangaza ajira mpya katika kipindi chote cha utawala wake. Waalimu waliomaliza vyuo mwaka 2015 hadi leo wapo mtaaji jobless.

8. Aliua sekta binafsi kwa kutoza kodi kubwa, na kuharibu mazingira ya biashara. Hoteli nyingi za kitalii zimekufa kama vile Ngurdoto, Impala, Naura Spring na nyingine zimegeuka hostel za wanafunzi kama Landmark ya Ubungo.

9. Alipunguza mzunguko wa pesa mtaani na kuhakikisha matajiri wanaishi kama mashetani.

10. Katika utawala wake waliibuka watu wasiojulikana ambao waliteka, kujeruhi na kuua watu wasio na hatia. Watu hao walimpiga risasi Tundu Lissu mchana kweupe na mpaka leo hawajakamatwa.

11. Aliwapa nguvu baadhi ya viongozi kama vile Makonda na Sabaya kutesa na kuumiza wananchi kadri walivyojisikia. Makonda alishambulia kituo cha CMG kwa mitutu ya bunduki lakini hakuchukuliwa hatua yoyote. DC Sabaya majuzi kampiga diwani wa Sombetini nusura kifo.

12. Alifuta fao la kujitoa na kusababisha watumishi wengi wenye mikataba ya muda mfupi kuishi maisha magumu baada ya ajira zao kukoma.

13. Katika serikali yake Wapinzani walionekana maadui na sio watu wenye mawazo mbadala. Waliteswa na kufunguliwa kesi za uchochezi. Wengine walipotezwa na hata kuuawa. Alitamani upinzani ufe.

15. Katika utawala wake maiti 17 ziliokotwa ufukwe wa Coco na nyingine 6 ziliokotwa mto Ruvu kwa pamoja zikiwa zimefungwa kwenye sandarusi, na baadhi zikivuja damu.

16. Aliharibu mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengi ukimwenguni. Serikali yake ilichoma vifaranga vya kuku kutoka Kenya na kutaifisha ng'ombe waliovuka mpaka kuja Tanzania.

17. Alisababisha wanasiasa wa Tanzania wakimbie nchi na kuishi uhamisho kama wakimbizi wa kisiasa wakiwemo Ansbert Ngurumo, Tundu Lissu na Godbless Lema.

18. Alitumia mabavu kulazimisha ushindi kwenye uchaguzi wa 2020 na kuhakikisha CCM inashinda majimbo yote. Alipora ushindi wa upinzani kwenye majimbo mengi kwa mtutu wa bunduki.

19. Alitumia sheria ya uhujumu uchumi kutesa wapinzani wake kisiasa na wafanyabiashara aliokua na kisasi kwa mfano Rugemala na Lema wa Elerai Construction.

20. Alipenda kuabudiwa, kutukuzwa na kuogopwa. Wote waliomnyenyekea aliwapa vyeo.

21. Aliamini mawazo yake ndio sahihi na hakutaka kushauriwa kwenye jambo lolote. Aliwahi kusema yeye hapangiwi cha kufanya.

22. Alipenda kuonekana mcha Mungu japo kiuhalisia ni dikteta katili aliyetisha. Alimpoteza Ben Saanane baada ya kuhoji kuhusu PHD yake.

23. Alitangaza kuwa Tanzania haina corona na akataka watu wasivae barakoa wala wasikubali chanjo kutoka nje ya nchi.

24. Alipeleka miradi mingi ya maendeleo kijijini kwake Chato kama uwanja wa ndege, hospitali ya rufaa, benkiz barabara za lami na mbuga ya wanyama ambayo haikua na wanyama ikabidi kuhamisha kutoka mbuza zingine.

25. Aliingilia mihimili yote ya dola ikiwemo mahakama na bunge. Aliwazawadia vyeo vya ujaji mahakimu waliowafunga wapinzani jela.

26. Aliigeuza Tanzania kama mali yake binafsi na katika kila mradi alipenda atajwe yeye. Aliamini akiondoka hakuna atakayeweza kuendeleza yale aliyofanya. Bunge liliwahi kupendekeza kumuongezea muda wa kutawala atakapomaliza mihula yake miwili, kumbe Mungu ana mipango yake hata hiyo miezi 4 hakumaliza ya kura alizoiba

Angalia list ya mabaya ya magufuli uliyoolozesha na angalia likes ulizopata
 
Angalia list ya mabaya ya magufuli uliyoolozesha na angalia likes ulizopata
Magufuli alikuwa wa HOVYO tu wala usihesabu likes za wasomaji. Mungu ameipenda nchi yetu akasitisha maisha yake kwa kuwa alitaka kutugeuza Burundi.
Huyu Pimbi tuliyemfukia Chato amewajaza propaganda za kijinga za upande mmoja na wapumbavu mumeingia kingi.
 
Mosi Kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na kumaliza kabisa mbio na matamanio ya zaidi ya Wanachama 42 wa CCM kuwa Rais.
ii) Kuhamishia Serikali Dodoma na kuipa hadhi ya Jiji
iii) Kuanza Ujenzi wa Ikulu mpya kwa kutumia JKT.
iv) Kuanzisha Ujenzi wa Stigler's gorge HEP .
v) kuanzisha Masoko ya Madini kila Mikoa zenye Madini.
vi) Kuanzisha Maduka ya Madawa muhimu ya Serikali yaani MSD
vii) Kufufua TTCL
viii) Kufufua Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
ix) kufufua ATCL
x) Kufufua Viwanda vilivyokufa kama Tanlec, kurudisha Mali za Nyanza Cooperatives , nk
xi) kumteua CGP kutoka JWTZ hakika imeleta sura na taswira mpya ndani ya Magereza.
xii) kujenga Daraja la Tanzanite
xiii) Kusimamia ujenzi wa Barabara karibia 80% zimejengwa akiwa Waziri wa Ujenzi na Rais wa Nchi.
xiv) Kujenga Interchange za Dar
xv) Ujenzi wa Nyumba za Magereza
xvi) Ujenzi wa Hostel za UDSM,
xvii) Kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe,
xviii) Kuua Vyama vya Upinzani
Xix) Ujenzi wa Uzio wa Mererani kuzunguka mgodi wa Tanzanite,
xx) Kuwapatia na kuwajengea Wachezaji wa Taifa Stars Viwanja pamoja na Nyumba
xxi) Ujenzi wa Viwanja vya Ndege akiwa Waziri wa Ujenzi na Rais ,
xxii) Ununuzi wa Rada 4 za kuongozea Ndege,
xxiii) Ujenzi wa SGR,
xxiv) Ujenzi wa Hostel mpya za MUST
xxv) Kusomesha Wanafunzi wa Kidato ha kwanza hadi cha Kidato nne bila malipo
xxvi) Kutosafiri kwenda Ulaya akiwa Rais,
xxvii) Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Musoma (Kwangwa)
xxviii) Uanzishaji wa Hifadhi ya Nyerere
xxix) Uanzishaji wa Hifadhi ya Burigi-Chato
xxx) Uanzishwaji wa Kampuni ya Twiga Corp.
xxxi) Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mtwara
xxxii) Ujenzi wa Hospital ya Uhuru Mkoani Dodoma
nk

Pumzika kwa amani Hapa Kazi Tu.
Sawa kabudi
 
Mchaka mchaka wa maendeleo aliyokimbiza within 5yrs more than 50yrs
Kufanya nchi kuweza kujiamulia mambo yake yenyewe huu Ndio uhuru wakweli against Neo Colonialism
Akiongea dunia nzima inamjadili
Hotuba zake anavojua kuji connect na hadhira yake popote pale daah
Ukitoa mapungufu yake the guy was iron man !
Maamuzi magumu !nk
Rip legend!
 
Back
Top Bottom