JE, UTARATIBU WA MAHARI SI MZIGO KWA UPANDE WA MWANAUME?

Joined
Oct 5, 2026
Posts
31
Reaction score
51
Wazazi wa mwanaume wanahangaika kumlea, kumsomesha na kumjenga mtoto wao kwa gharama kubwa. Akifikia umri wa kuoa, bado wanatarajiwa kutoa mahari kwa wazazi wa mwanamke.

Je, huu ni utamaduni wa kuunganisha familia au ni mzigo unaowekwa zaidi upande mmoja?

Kwa nini familia zote mbili zisishirikiane kusaidia wanandoa kuanza maisha yao badala ya mahari kuwa sharti linaloweza kuleta madeni na kuchelewesha ndoa?

Je, mahari inahitaji kufanyiwa marekebisho kulingana na maisha ya sasa? Tujadili kwa hoja.
 
Huyo mwanamke unaeenda kumuoa unadhan hajalelewa...? ,hajasomeshwa...?

Kama unaona ni gharama,...oa kwenu.
Nani kasema mwanamke hajalelewa au hajasomeshwa? Hoja yangu si kupinga malezi ya mwanamke, bali kuhoji kwa nini gharama za kulea watoto zigeuzwe sababu ya upande mmoja kulazimika kutoa mahari kwa upande mwingine. Kama wote wamelelewa na kusomeshwa na wazazi wao, kwa nini tusiangalie usawa wa majukumu badala ya kuhalalisha utaratibu kwa hoja hiyo hiyo? Kujadili utamaduni si kudharau mwanamke, ni kuhoji kama utaratibu wake unapaswa kuendana na maisha ya sasa.
 
Wazazi wa mwanaume wanahangaika kumlea, kumsomesha na kumjenga mtoto wao kwa gharama kubwa. Akifikia umri wa kuoa, bado wanatarajiwa kutoa mahari kwa wazazi wa mwanamke.

Je, huu ni utamaduni wa kuunganisha familia au ni mzigo unaowekwa zaidi upande mmoja?

Kwa nini familia zote mbili zisishirikiane kusaidia wanandoa kuanza maisha yao badala ya mahari kuwa sharti linaloweza kuleta madeni na kuchelewesha ndoa?

Je, mahari inahitaji kufanyiwa marekebisho kulingana na maisha ya sasa? Tujadili kwa hoja.
Licha ya kuwa mzigo, mahari inashusha utu wa mwanamke.

Mwanamke anakuwa kama bidhaa kanunuliwa kwa mahari.

Ndiyo maana wanaume wengine wanajiona wana haki ya kupiga wanawake.

Kwa sababu wanaona wewe nimekununua kwa hela/ng'ombe etc.
 
Nashukuru kwa maoni yako. Nakubaliana kuwa mwanamke si bidhaa ya kununuliwa kwa mahari. Hoja yangu ni je, mahari inaweza kubaki kuwa ishara ya heshima bila kuwa mzigo kwa upande mmoja? Kuhusu ukatili wa kijinsia, hilo ni suala tofauti; hakuna mahari inayompa mwanaume haki ya kumpiga mke wake. Lengo ni kuona familia zote mbili zinashirikiana kwa haki na maelewano.
 
Mahari haiwezi kuwa ishara ya heshima ikiwa itakuwa ya kutolewa na upande mmoja.

Kwa sababu, hata heshima inatakiwa kuwa pande zote mbili.

Sasa utatoaje heshima kwa upande mmoja tu?

Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ukatili wa kijinsia na mahari.

Katika jamii hizi za kutoa mahari kwa mwanamke, mwanamke anaonekana kuwa yupo chini ya mwanamme. Ndiyo maana kiutamaduni, hata kwenye lugha, anaolewa, haoi.

Mwanamke anaonekana ni mali ya mwanamme, ndiyo maana ananunuliwa kwa mahari, na kwenye tamaduni nyingine kaka akifariki, mke wake anarithiwa na kaka mwingine mdogo.

Sasa, ukishamfanya mwanamke mali ya mwanamme, hapo mwanamme akijisikia kumpiga mwanamke atampiga tu. Kuna siku mwanamme atamwambia mwanamke apike, aoshe vyombo (afanye kazi alizolipiwa mahari kufanya), mwanamke atasema kachoka, mwanamme ataona hapa mbona napunjwa? Nimelipa mahari mwanamke afanye kazi hizi, halafu hafanyi, nampiga huyu ajue kuwa mimi ndiye bwana hapa, siku nyingine asinibishie.

Sisemi kuwa mahari inampa mwanamme haki ya kumpiga mke wake, nasema kuwa wanaume wengi wanaona mahari inawapa nguvu hiyo.

Wanaona "Wewe mwanamke ni mali yangu, nimekununua kwa mahari, sasa ukikataa kufanya ninalosema nakupiga tu".

Ukiondoa mahari, ukifanya ndoa kuwa ni jambo la watu wawili walio sawa waliokubaliana kukaa pamoja, ukaondoa habari nzima ya nani kamnunua nani, unakuwa umeanza ndoa kwa usawa na kupunguza haya mambo ya mwanamme kujiona yeye ana haki ya kumpiga mwanamke kwa sababu mwanamke ni mali yake aliyoinunua kwa mahari.
 
Je Adam alimlipa mahari kwa Eva? kama jibu ni ndio mahari alipokea nani? na kama jibu ni Hapana Huu utaratibu wa kulipa mahari kwa mwanamke umetoka wapi???
 
Licha ya kuwa mzigo, mahari inashusha utu wa mwanamke.

Mwanamke anakuwa kama bidhaa kanunuliwa kwa mahari.

Ndiyo maana wanaume wengine wanajiona wana haki ya kupiga wanawake.

Kwa sababu wanaona wewe nimekununua kwa hela/ng'ombe etc.
Yeah, kwa maisha ya miaka hii mahari haifai kutolewa kwa sababu wanandoa kwa kiasi kikubwa wanayaoambania maisha yao wenyewe. Zamani mwanamke alikuwa anapelekwa nyumbani/kwenye familia ya mume, anapiga kazi pale labda ndiyo maana mahari ilionekana kuwa na maana kidogo.
 
Je Adam alimlipa mahari kwa Eva? kama jibu ni ndio mahari alipokea nani? na kama jibu ni Hapana Huu utaratibu wa kulipa mahari kwa mwanamke umetoka wapi???
Ndugu yangu, hoja ya Adamu na Eva ni simulizi la kibiblia linalokubalika kwa imani ya dini, lakini si ushahidi wa kihistoria au kisayansi unaothibitisha moja kwa moja kwamba mahari ilianza hapo. Tusichanganye imani na ushahidi. Hoja yangu ni kuhusu utaratibu wa mahari katika jamii zetu za sasa: je, ni lazima gharama hiyo ibebwe zaidi na upande mmoja, au familia zote mbili zinaweza kukubaliana kwa kuzingatia uwezo wao? Tujadili hoja yenyewe badala ya kutegemea simulizi la dini pekee.
 
MAHARI ANAPASWA KUTOLEWA MWANAMKE BIKRA
Hiyo bikra yenyewe mbona wanairudisha tu siku hizi mkuu kama yale magari yenye mileage kubwa yanavyochakachuliwa unanunua kwa kuona mileage imeshukaaa 😂😂😂

Hapa kuna hoja kubwa ya kifalsafa umeidogosha sana iende kinyegenyege tu.
 
Bikra hairudi na hakuna bikra bandia
 
Mkubwa, usitafute kichaka cha kujificha. Toa mahari ya watu, usilete hoja zako ambazo hazina mantiki, mahari ni mila na desturi za africa kama hauna kibunda pita kushoto wenye mahari tunakuja kuoa.
 
Ndugu yangu, badala ya kujibu hoja kwa hoja, umeamua kutumia kejeli na dharau. Kutaja mahari kama mila ya Kiafrika hakumaanishi kwamba haiwezi kujadiliwa au kuangaliwa upya kulingana na mabadiliko ya maisha. Mila ni sehemu ya utamaduni wetu, lakini kujadili namna ya kuiboresha si kuipinga Afrika. Kama una hoja inayopinga ninachosema, iweke wazi tuijadili kwa mantiki. Mjadala haujengwi kwa kumdharau mwenzako, bali kwa hoja na maarifa.
 
Mahari haiwezi kuwa ishara ya heshima ikiwa itakuwa ya kutolewa na upande mmoja.

Kwa sababu, hata heshima inatakiwa kuwa pande zote mbili.

Sasa utatoaje heshima kwa upande mmoja tu?

Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ukatili wa kijinsia na mahari.

Katika jamii hizi za kutoa mahari kwa mwanamke, mwanamke anaonekana kuwa yupo chini ya mwanamme. Ndiyo maana kiutamaduni, hata kwenye lugha, anaolewa, haoi.

Mwanamke anaonekana ni mali ya mwanamme, ndiyo maana ananunuliwa kwa mahari, na kwenye tamaduni nyingine kaka akifariki, mke wake anarithiwa na kaka mwingine mdogo.

Sasa, ukishamfanya mwanamke mali ya mwanamme, hapo mwanamme akijisikia kumpiga mwanamke atampiga tu. Kuna siku mwanamme atamwambia mwanamke apike, aoshe vyombo (afanye kazi alizolipiwa mahari kufanya), mwanamke atasema kachoka, mwanamme ataona hapa mbona napunjwa? Nimelipa mahari mwanamke afanye kazi hizi, halafu hafanyi, nampiga huyu ajue kuwa mimi ndiye bwana hapa, siku nyingine asinibishie.

Sisemi kuwa mahari inampa mwanamme haki ya kumpiga mke wake, nasema kuwa wanaume wengi wanaona mahari inawapa nguvu hiyo.

Wanaona "Wewe mwanamke ni mali yangu, nimekununua kwa mahari, sasa ukikataa kufanya ninalosema nakupiga tu".

Ukiondoa mahari, ukifanya ndoa kuwa ni jambo la watu wawili walio sawa waliokubaliana kukaa pamoja, ukaondoa habari nzima ya nani kamnunua nani, unakuwa umeanza ndoa kwa usawa na kupunguza haya mambo ya mwanamme kujiona yeye ana haki ya kumpiga mwanamke kwa sababu mwanamke ni mali yake aliyoinunua kwa mahari.
Mkuu wewe umeoa..?
 
Back
Top Bottom