vexozanzhu
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 503
- 615
Niliangalia malumbano ya hoja wiki iliyopita akili ya wema na mchangia mada mmoja ambaye niliamini ni msomi wanafanana na inawezekana huyu Wema ana afadhali sababu yule aliyetoa hoja yake alikuwa jinsia (ME) kwa jinsi alivyoliongelea hilo swala kwenye mjadala uliohusu tozo za kodi kwenye pads, nilipata ukakasi kuelewa ni mfumo wa elimu au jamii umetufikisha hapa...“ Nilishindwa kupanda mahakamani, ninapofika kwenye siku zangu huwa napata maumivu makali, nilienda kuchoma sindano ya maumivu, nikapumzika kisha nikarudi nyumbani “
Hivi ni kwanini Wanawake wa Siku hizi huwa hawana Aibu hasa katika Kuongelea Masuala yao ya Hedhi jambo ambalo naamini kwa Maadili ya Kiafrika si vizuri Kuyaongelea hadharani hivi tena Mtu akiwa hana hata Chembe ya haya ( aibu ) au hofu?
Tujadili.