Je, utumiaji wa kiyoyozi(AC) unaongeza matumizi ya mafuta kwenye gari?

Je, utumiaji wa kiyoyozi(AC) unaongeza matumizi ya mafuta kwenye gari?

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakiamini ukitumia AC unatumia mafuta mengi kuliko ukiendesha bila AC[vioo wazi].

Kiufundi ili AC ifanye kazi inahitaji nguvu ya ziada kutoka kwenye engine ili compressor izunguke,sitaingia kiundani kwasababu mimi sio mtaalam wa AC. Na kwa kuzingatia hili watu wengi wanaamini ukitumia AC unatumia mafuta mengi kuliko ukiendesha bila AC.

Hili si kweli. Ukitumia AC gari inatumia nguvu zaidi LAKINI ukiacha vioo wazi gari inatumia nguvu zaidi ya ukifunga vioo na kuwasha AC. Vioo vikiwa wazi gari inatengeneza kitu kinaitwa 'DRAG' yaani upepo unajaa ndani ya gari na kuifanya iwe nzito kwahio inatumia nguvu nyingi kutembea kuliko ukifunga vioo na kutumia AC.

Kwenye speed ya 80kph ukifungua vioo unatumia mafuta 20% zaidi ya ukifunga vioo na kuwasha AC. Kwa maelezo haya nahitimisha kuwa UKITUMIA AC GARI INATUMIA MAFUTA KIDOGO KULIKO USIPITUMIA AC NA KUACHA VIOO WAZI.

Hiki nilichoandika hapa ni scientifically proved ya SOCIETY OF AUTOMOBILE ENGINEERS[SAE],sikuweka link ili nichangamshe mada,jisomeeni hapo chini. page 1,2 even 3 mkiweza

http://auto.howstuffworks.com/fuel-efficiency/hybrid-technology/driving-with-windows-down1.htm

CC: OLESAIDIMU MANI Kaizer Kalamzuvendi Titans
 
Lakini sio tofauti kubwa sana maana hata rpm haipandi sana ukiwasha ac unless gari liwe na matatizo mengine kama miss.

kidoooogo sana ndio maana wanasayansi wamesema ukishusha vioo unatumia mafuta mengi kuliko ukiwasha AC
 
RRONDO;
umewahi kukaa kwenye foleni??? Kama upo Highway sawa, pandisha vioo, weka AC. Hapo sawa sawia kabisa, lakini kwenye foleni, mafuta ya lita 2 uweke AC?

sijakuelewa,yaani ukikaa kwenye foleni ndio??? mafuta ya lita 2 hata usipowasha AC ni kidogo.
 
kama unaona mafuta ni bei panda pikipiki mkuu..

ndetichia;
Tatizo si bei ya mafuta, yapo matatizo mengi ya kujaza full tank. Pia hizo pikipiki haziruhusiwi City Center. Nasema, AC itakugharimu zaidi kama gari halitembei kwa kasi. Upo gea namba moja full time na huendi popote. Karibu sana watu wayatupe magari yao kwani ni adhabu hata kuliendesha
 
ndetichia;
Tatizo si bei ya mafuta, yapo matatizo mengi ya kujaza full tank. Pia hizo pikipiki haziruhusiwi City Center. Nasema, AC itakugharimu zaidi kama gari halitembei kwa kasi. Upo gea namba moja full time na huendi popote. Karibu sana watu wayatupe magari yao kwani ni adhabu hata kuliendesha

kwa hali hii hata usipowasha AC inakugharimu
 
uwelewa mdogo tu wa sisi baadhi ya watanzani kuhusu ac za magari,aina maana kwamba ukisima au.ukiwa unaendesha ac itakuwa inamaliza mafuta kwa maana hata kama haujawasha ac lakini gari likawa linaunguruma bado mafuta yatakuwa yanaendelea kutumika tu so bora ujilie ubaridi wako tu ndani.....
 
Mimi hua sishushi vioo hata kidogo....inakera pale unapompa mtu lift halafu ile kupanda tu anaanza na kupunguza au kuongeza sauti ya redio,akimaliza hapo anabonyeza button ya vioo sasa kwa vile ume-lock button utasikia "bro shusha vioo basi tupate fresh air".


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom