kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nchi hii vigogo wapigaji wa hela ya umma wanafikiri watu ni wajinga wote na hawana kumbukumbu. Suala la ufungaji flow meter bandarini wengi tunakumbuka lilifanyika kipindi cha awamu ya nne ya JK lakini zikawa hazitumiki kwa kuhujumiwa.
Iko hivi, yaani uwekaji wenyewe ni dili maana kuna ulaji hapo kwa vigogo kutoa kandarasi. Ni pesa nyingi za umma zinatumika. Kisha kwenye matumizi ulaji tena kwa vigogo unafuata. Yaani meter zikitumika ujazo kamili unafahamika kwa hivyo mleta mafuta itabidi alipe kodi sahihi. Kwa hivyo meter zinahujumiwa hata kuharibiwa ili itumike kukadiria au kiasi anachotaja muingizaji mafuta.
Huu ndio mzunguko kichaa wa upigaji wa kiwazimu nchini hapa.
Nimelazimika kuandika uzi huu baada ya kuona kwenye taarifa mkandarasi anafunga flow meter bandarini na eti karibu mbili zitazinduliwa na nyingine ya tatu itakua tayari mwakani. Taarifa inatoka kana kwamba flow meter ni kitu kipya hakijawahi kuwekwa bandari ya Dar es Salaam.
Hakika nchi yetu ina vituko na hasa bandari zetu ni wizi mtupu kuanzia juu hadi chini. Hata kuletwa DP World ni wizi mtupu.