Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?


Kweli Pasksli ww ni bonge la msukuma, kwa jinsi watu walivyokuwa wanashobokea ndege hapa nchini kipindi cha Magufuli,basi unadhani ni jambo litakalowastua hata wamerakani kuwa kuna ndege imetoka Tanzania. Ni sawa na watu watoke huko misungwi waje na Coaster hapa Dar utegemee eti watu wa Dar watanote kuna Coaster toka misungwi, hivyo waanze kuvutiwa na kwenda kutembelea misungwi. Kwa taarifa yako ni watu wachache sana huko US wanaojua kama kuna nchi inaitwa Tanzania,na hata wakiona hiyo ndege ya Magufuli watadhani ni ndege ya Ukraine imepotea kwenye uwanja wa vita. Huko kuna ndege za kutosha, kiasi hata ni ngumu kujua kuna ndege ya Tanzania imeingia huko. Ukitaka kujua ninachokuambia, fuatilia hata hiyo ziara ya rais, ni watu wachache sana huko wanajua kama Rais wa Tanzania yuko US. Yaani ni wa kawaida sana sembuse hiyo ndege?
 
Kabisa, ili watu wajue kuna ndege imetoka Tanzania na kuingia US labda ipate ajali na kuangukia huko US, sio zaidi ya hapo.
 
KQ inakuaje Direct flight to NY kwa abiria anayetokea TZ? Umezungumzia watalii matajiri nikawakumbuka ndugu zetu toka China na kidogo India (bahili kupitiliza) baadhi wanabebaga mpaka msosi
 
Mkuu Pascal Mayalla unaweza kuwa na mawazo mazuri lakini umesahau wale wadeni wetu waliopewa hati za kukamata mali zetu pindi wakipata fursa. Hili limefanya ndege zetu zingunguke humu humu ndani kama kuku mgeni
Tanzania hatudaiwi na mtu yoyote huko nje ambae anaweza kukamata ndege zetu. Hii kauli ameitoa juzi tu Waziri wa Fedha Bungeni.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Its obvious
KLM for Europeans.,
US ni kweli
Itakua wana sababu
 
Niliwahi kusikia route ya Mumbai,mara nikasikia ya DAR-Heathrow hivi hizi ziliishia wapi?? Ukitaka kuona hili shirika menejiment yake haipo serious waulize hizi Route kwanini zilikatishwa?
Route kati ya DAR na BOM bado ipo mara mbili kwa week - Jumatatu na Ijumaa.

Hiyo ya Heathrow uliisikia wapi?
 
Route kati ya DAR na BOM bado ipo mara mbili kwa week - Jumatatu na Ijumaa.

Hiyo ya Heathrow uliisikia wapi?
Tanzania tuna landing rights Heathrow, mpaka kesho, Kwa sasa Kwa vile hatuendi zinatumiwa na SAA. ATC ilipanga kutimba London, tena hadi mimi nilipanga kuwemo kwenye Maiden flight. Msikilize DG wa ATCL, Eng. Ladislaus Matinde akizungumzia route ya China
P
 
KQ inakuaje Direct flight to NY kwa abiria anayetokea TZ? Umezungumzia watalii matajiri nikawakumbuka ndugu zetu toka China na kidogo India (bahili kupitiliza) baadhi wanabebaga mpaka msosi
Wakenya wako so much business minded, Kwa mujibu wa sheria za anga, wanaweza kuruka direct flights only from Nairobi, to JFK, sasa wanachofanya ni ndege inaanzia DAR as a regional flight ikifika Nairobi ndio inakuwa International flight.
P
 
Wakenya wako so much business minded, Kwa mujibu wa sheria za anga, wanaweza kuruka direct flights only from Nairobi, to JFK, sasa wanachofanya ni ndege inaanzia DAR as a regional flight ikifika Nairobi ndio inakuwa International flight.
P
P! Kafuturu Kwanza naona swaumu inakuchanganya
 
Mkuu Paskal umeongea Jambo muhimu sana, ni Kama tumefungwa ufahamu.
Ndio tusaidiane kufunguana, juzi kati pale Dubai kwenye Expo Dubai, Watanzania walitimba usipime!. Wanachotaka Watanzania ni kuwa organised tuu, wahamasishwe, wanaojitokeza na Dreamliner linajazwa!, labda zitokee figisu za US visa, maana wazamiaji wasije kuutumia mwanya huo kuzamia!.
P
 
Niliwahi kusikia route ya Mumbai,mara nikasikia ya DAR-Heathrow hivi hizi ziliishia wapi?? Ukitaka kuona hili shirika menejiment yake haipo serious waulize hizi Route kwanini zilikatishwa?
Hakuna haja ya kuwauliza, ni changamoto za Covid 19, mashirika mengi ya ndege, yameyumba.
P.
 
Route ya China ipo na kwa mara ya kwanza tulienda April last year, baadaye wakasimamisha kwa sababu ya sheria za Covid-19. Kuna mashine ya kipimo walikihitaji, tumeshanunua na soon tutarudi Guangzhou.
 
Kuingiza ndege USA direct kutoka Tanzania sio rahisi kama unavyodhani. Kenya walikua na hiyo ruhusa sijajua kwa sasa wanaendeleaje.
Kuna michakato mingi sana ya kiusalama before kupewa hicho kibali.

Nitashangaa sana kama hata hili haulifahamu.
Kwanza unapata wapi abiria 200 plus wa kujaza ndege inayoenda Marekani direct toka Tanzania?!
Airlines zinatumia mtindo wa “Hub and Spoke”, yaani abiria wanakusanywa toka sehemu mbalimbali kwenye point(Hub) moja kama vile pale Dubai (Emirates) na kupelekwa sehemu husika.
Pia kukidhi masharti ya kuingia US kama airline sio mchezo. Kenya Airways waliona shughuli yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…