Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
kuna siku ukabila utatushika pabaya huuu.......
mungu tunusuru kugeuka kenya, lakini naona huko tunakoelekea pabaya kweli kweli, twaweza waulisha wachaga hivi hivi!
 

sasa wapewe nafasi miority groups japokuwa mtu mwenye uwezo kwa nafasi ile anatoka kwenye majority group?
si itakuwa kujinyima maendeleo huko?
 
Mwanakijiji,

..kuna wengine wameoa au kuolewa uchagani. hao nao wanabemba "dhambi" ya uchaga.

..kama ulisikia madai ya Wangwe ni kwamba Anna Komu mzaliwa wa ZNZ anaingia kwenye kundi la Wachaga kutokana na ndoa yake.

NB:

..nategemea Mama Fatma Maghimbi wa CUF naye atashughulikiwa maana mumewe ametokea Kilimanjaro.

..hata Prof.Ibrahim Lipumba naye anaingia ktk kundi hilo.
 


sasa nani ataamua kuwa "Na Director au wafanyakazi wa hiyo directorate wasiwe wachaga, wanyakyusa, wasukuma, wapare wala wahaya."? Kwa hiyo itabidi tuingize kwenye sheria kipengele kinachokataza hivi siyo? Na hao watakaotunga sheria hizo miongoni mwao wawemo wachagga, wanyakyusa, wasukuma, wapare na wahaya? Au itatungwa na Bunge la Minorities?
 
Mzee Mwanakiji,

Naona sasa, Unaanza kujishushia heshima, Kila ukiamka Udini, Ukabila......Mambo unayoyandakika Humu yanasomwa na watanzania mamilioni.Na kama mengi ninavyoyaona unayaweka katika Hali ya Uchochezi.

Unapoona Vita vinaendelea nchi nyingine usidhani vilikuja tu, Kenya kwa ajili ya Mashada forums kuongelea Ukabila na kuweka probaganda za ugawanishi ndio zilichochea yale yaliyotokea last decembere.

Amani Tanzania hailindwi kwa uandishi unaoufanya sasa, Amani Tanzania Inakuja kwa kuchambua mambo yanayoweza kutijenga.

Swala unaliongelea kwasasa ni issue ya HR polices za makampuni ya Bongo kuwa refined and that is what is happenning. Ila ukileta Mambo ya UDINI,UKABILA NA MENGINEYO yanayofanana na hayo utakuwa Mchochezi.

Mimi sijawahi kufeel isolated Tanzania kwasababu sio Mchaga au Dini Fulani , Because I believe on Working Hard you can be wherever you want.

Leo wewe Uko Marekani si kwababu ni Fisadi au Mchaga, Balia ni kwa juhudi zako,We need to chang the perspective of the Dialogue and bring a bit of Construtive discussion.

Mwisho kama unataka Vita Tanzania, Ili Upate makaratasi Marekani, Acha Huo Mchezo , tutakushauri njia nyingine.

MUNGU IBARIKI TANZANIA DUMIHA AMANI, TUPE MOYO WA UVUMILIVU NA TUFUNGULIE NJIA YA KUSOLVE MATATIZO YETU BILA UZUSHI
 
Watoto wa MKAPA ni wachagga kwasababu mama yao ni Mchagga...Lakini Obama ni Mweusi kwasababu Mama yake ni mweupe!
Make sense?
 
..nategemea Mama Fatma Maghimbi wa CUF naye atashughulikiwa maana mumewe ametokea Kilimanjaro.

mama maghimbi anasameheka manake damu ya mpemba kama ya mchaga.....ukioa au ukiolewa na mpemba na wewe unageuka mpemba.....na watoto wanageuka wapemba japo kama mama yao tu ni mpemba.lol
 
sasa wapewe nafasi miority groups japokuwa mtu mwenye uwezo kwa nafasi ile anatoka kwenye majority group?
si itakuwa kujinyima maendeleo huko?

kuna kujifunza kuwa wakweli na kuact honestly hata kama ni kwa uchungu. Kiongozi wa hicho kitengo cha ajira akitoka kwenye minority group hata kuwa na upendeleo wa kuangalia huyu anayeomba kazi ametoka kabila gani. Atakuwa na interest ya qualifications tu as kabila lake watakuwa ni kati ya waombaji wachache.
 

leo kweli... ukiitikia hoja yangu kwa kutumia vionjo you'll miss the big point. Tulia na usome hasa kinachosemwa.
 
...wait a minute....na wale viongozi wa idara ambao ni wakristo na wenywe waachie ngazi!!!!!
 
Watoto wa MKAPA ni wachagga kwasababu mama ya ni Mchagga...Lakini Obama ni Mweusi kwasababu Mama yake ni mweupe!
Make sense?

sasa mushi obama anaingia vipi hapa?

nitakupa definition kidogo kama huelewi:
mweusi anakuwa mweusi ikiwa bibi yake mmoja ni mweusi, haitegemei bibi upande gani even
mngazija,mchaga,mpemba wanakuwa makabila hayo ukioa, ukiolewa na mtoto pia anakuwa kabila hilo hata kama ukoo wa upande wa baba ni kabila jengine
 

Yani kama nikiruhusiwa kutake a guess kuhusu majina base na kinachoandikwa...Basi you sound very presidential material!

Haya tuombe Mungu Kikwete arudi ili UZUSHI WOTE WA MAFISADI UFE!
 


sasa huyo director kutoka minority group, akiona kuwa kuna minority katika waombaji tena kutoka kabila lake awape ka"upendeleo" ka aina fulani? Tutamzuiaje yeye kutowapendelea watu wa kabila lake au kula njama na minority mwingine ili wabadilishane wanaowapendelea ili wasioneshe ukabila "mkwere ampendelee msegeju, na msegeju ampendelee mkwere"?
 

kwani hakuna mtunga sheria hata mmoja kutoka kwenye minority groups? Kina Shivji ni watu wa morogoro kwa mfano, na ni mtu professional na ana integrity ya juu, nina hakika anaweza kuja na sheria itakayokiwezesha hiki kitengo kufanya kazi. Tuondoe kwanza inferiority complex ya kudhani kila kitu wanaoweza kufanya nchi hii ni wachaga na hayo makabila dominant.
 

Mkuu ngoja nikueleweshe!
Wanasema kuwa wale walioowa uchaggani kama Mkapa..Na wao wanaangukia kwenye chagga!
Na mimi nikasema haiwezekani kwani kina Merinyo si wachagga kwasababu tu mama yao ni mchagga...Wao wataendeleza kabila la baba yao!
The same with Obama...Licha ya kwamba mama yake ni mweupe...Wao wanasema yeye ni mweusi...Na hii ni kwasababu ya baba yake!
Make sense now?
 
gaijin said:
mama maghimbi anasameheka manake damu ya mpemba kama ya mchaga.....ukioa au ukiolewa na mpemba na wewe unageuka mpemba.....na watoto wanageuka wapemba japo kama mama yao tu ni mpemba.lol

gaijin,

..Chacha Wangwe alikuwa challenged kuhusu madai yake ya Wachaga na wabunge wanawake wa Chadema kwamba Mama Anna Komu ni mzaliwa wa Zanzibar.

..majibu yake yalikuwa mama huyo ameolewa Uchagani, watoto wake ni Wachaga, hivyo ni wa huko huko Uchagani.

..tena mara nyingine watu wenye hoja kama za Chacha Wangwe huwatumbukiza hata Wapare ktk kundi moja na Wachaga, kuunda kabila la Wakilimanjaro.

..sasa hoja hiyo inaweza kuwasomba watu wengi wenye ndoa na Wachaga. ndiyo nikakupa mifano ya Mama Maghimbi na Prof.Lipumba.
 

Qualifications matters, kwa maana hiyo unataka kusema tutafute alliens kabisa kwenye suala la ajira???!!!! hili ni jambo linalowezekana, nothing is impossible under the sun. Mama Ghasia pia anaweza kuwemo humo, anatoka kwenye minority groups to mention a few wanaoweza kuwa kwa hiyo directorate.
 

Mwanakijiji,

Ulikuwa bored nini? Sidhani kama Wachagga wako wengi hivyo kwenye idara mbalimbali.

Kazi za serikalini iwe kwa uwezo wa mtu. Kwenye siasa ndiko inatakiwa kuwa mwangalifu lakini sio serikalini.
 

Thatha hapo umethema neno ati angalau na akina thithi tupate nafathi ya kujimwayamwaya kidogo jamani...Kha!! maana kila thehemu ni mathawe, kimaro, Shayo, thijui Urio....Kweli mwanakijiji.....
 
Mwanakijiji,

Unaweza kui print hii "modest proposal" kwenye magazeti bongo under your name?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…