Naona watu wamecomment kwa ghadhabu sana, especially wale ambao thread hii imewagusa, kitu cha Muhimu tujue kwamba hii issue ni nzito wala si ya kupuzwa kiasi hicho. Wenzetu nchi zilizoendelea hasa za Ulaya kuna legal binding za kuzisimia nchi kutekeleza mshikamano kwa jamii mbalimbali zinazounda nchi zao. Mnaweza pitia European Charter for Regional and Maniority Languages (1992) na pia Convention for Protection of Maniorities (1994). Nchi zilizoendelea wanasoma vyuoni kozi kama Diversity managements, Social Cohesion na Social Intergration kwa ajili ya matatizo kama haya. Sisi tunafumba macho huku watu wengine wanaumia kama tunavyoona kwenye hisia zao kwenye michango yao katika thread hii. Ni muhimu tukaelewa tofauti ya ajira ya Umma na Ajira Binafsi. Kama serikali inalengo la kutumia ajira kama kigezo mojawapo cha kuleta mshikamano katika nchi si sahihi kuajiri watu kwenye sector za umma kwa kufuata kigezo cha merit tu. Kwenye suala la Umma hakuna merit hata siku moja la sivyo hata wanawake wasingeweza kuwezeshwa ili wapate ajira au kujoin vyuo kama serikali ingekuwa inafuata merit tu. Kwa tuliofanya kazi serikalini tunajua kwamba kuna kazi ambazo hazina utalaamu sana kiasi kwamba uhusiano wa merit na utendaji kazi serikali si wa kuzingatia sana. Common service ya serikali ya Tanzania wala haiitaji merit recruitment kama inavyofikilika, hiyo ingeweza kutumika kubalance uiano wa watumishi baina ya makabila.
Na siyo sahihi kabisa kuwa wachaga hawapati upendeleo katika kupata ajira kwani wanaweza wakawa wanapata upendeleo inderectly kwa kuwa ndugu na jamaa wengi wako jikoni. Kwa wale wataalamu wa Social Science, Jaribuni kujikumbusha, Social Capital ya Bourdeux na Social Network ya Granovettor ili kujua jinsi gani mambo haya yanafanyika pasipo hata wakati mwingine kujua.
Swala la wachaga, wahaya, wanyakyusa kuwa na elimu zaidi ya mabila mengine ni swala la Kihistoria toka enzi za mkoloni wala haina maana kuwa hayo makabila ndio yamedondoshewa akili toka mbinguni. Mimi natoka mojawapo ya makabila hayo na nimeowa uchagani, kama serikali itakaa kimya na haioni matatizo ya baadaye inapandikiza mbegu za ubaguzi mbaya sana. Hiyo portifolio ya ndugu Stiven Waasira ndio kazi yake, lakini wala haitumiki hivyo imekaa kisiasa tu. Kwa tuliopitia kozi za Social Diversity management, ni wazi Tanzania imeundwa na vipisi vingi vya makabila na mapande mawili ya Dini (Muslim and Christian). Na hivyo vipisi vya makabira na mapande ya dini yanahitaji hekima na utaalam kuyamanage wala si kwa kufuata merit ambayo mwisho wake inatoa ajira ya makabila machache kwenye sector za umma pia kama inavyofahamika dini mojawapo inanung'unika kwa swala hili. Ieleweke hizo ni ajira za umma wala si mtu binafsi. Ajira za Umma zitumike kujenga taifa kama inavyofanywa kwenye ajira za vyombo vya ulinzi na usalama.
Nimeambatanisha paper ya Mtalaam wa Social Capiatl and Social Networks- Robert D Putnam kwa wale wanopenda kujielimisha kwa undani nadharia hii ya Social Capital and Networks na jinsi gani unaweza husianisha na makabila yenye nguvu na dini yenye wasomi wengi kwa Tanzania jinsi yanavyofaidika na hiyo hali ili hali wengine hawajui kama wanafaidika.
Mungu ibariki Tanzania.