Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Mkuu,
MMKJJ kaandika kwa mtindo wa kejeli... soma tena uelewe

Wako wengi watu wa hivyo. Typical Tanzanians. Hawasomi habari/mada kwa undani. Ndio maana wanadanganywa sana na magazeti ya udaku, pamoja na yale ya alasiri. Mtu anasoma headline tu, basi ana-conclude na anaanza mashambulizi.

Hapo juu, MMJJ ameshambuliwa na watu ambao hawakuisoma ile mada kwa umakini.
 

Mkuu raymond hapo kwenye nyekundu kwa wale wasoma biblia tunasemaaaaaaaaa...... "tafuteni kwanza ufalme wa mbingu na mengine yoooooote mtapewa kwa ziada"....kwe kwe kweeee!!! helo helooooo!i laf JF
 

Mkuu JMushi1

Hapo kwenye nyekundu; nadhani ni tafsri mbaya ya ule uelewa wa wa Mangis. Unajua Mangis walishtuka mapema na wakawa wanasemaaaaaa....tafuteni kwansa ufalme wa mbingu na mengine mtapewa kwa siada.... sasa inaelekea wensetu hawakuelewa visuri ufalme wa mbingu ni upi!!! wakasani ni madraaaa----madrasa kweliiiiiiii,,,,, Kele uuuuuuwi!!! mblah!! seeeeh!!
 

Mkandara umehit patamuu!! kaka ndo maana waambiwaaa, mchaga ni mchaga, ni kazi kaaaazi, no kulala kaka. tena ongezea wengine tulianza kwa kuuza sigara moja moja mtaani, then pakti nzima, then katoni nzima, then cartons and cartons, then 40feet meli, hujazungumzia wauza njugu na kikapu barabarani hadi u-milionea na hat ubilionea.....kaka hawa jamaa utawachoka kwa kuzisanya. na wakati wa kuzisanya kaka ni no starehe, mademu mbali kwan ni sumu kubwa ya utaftaji, ikibidi umezidiwa wagonga tu chweeee then huyoooooo, no kujenga kibanda, njoo kwa wensetu waswahili sasa!!!! kwe! kwe! teh! teh!

na hapo kwenye bluu.....ndo umemalisa kasi kaka.......shiiiida kaka Mkandara shiiiida baba, nyumbani Moshi arsi (ardhi) toho monamaaaayo! tufanyeje sasa si lasima tujitume tuuu. ndo maan hatulali kaka, halafu hatujaanza jana, ni tangu ensiiiii, wakti huo hata RTD haijaanza achilia mbali JF, TEH TEH TEH!
 


hapo kwenye nyekundu jamani massawe wensangu fipi huyu mkandara??? sasa madaraka wataka wapewe nani!!!! wasioshughulika, wapiga soga, washikina, wacheza ngoma, acha blah blah...kachape kazi kaka, wamangi tunasemakaaaa..fanya kasiiiii


hapo kwenye bluu, JMushi kashakuambia... lete wewe hizo data za ambao c wachaga ni wangapi??? unalia lia tuuuuuuuuu, unaikalia tu politic, kazi haufanyi, utakula nini??? unafkiri maendeleo yatashuka kama mana kutoka mbinguni??!! fanya kasi baba!!
 
wewe Mushi mzima? kuuza mtori kuna qualification gani? kupiga KIWI viatu au shoeshine unahitaji digrii gani?ufundi gereji n.k.
kazi za wachagga hadi kuuza mishikaki na kuwa wahudumu wa Bar, kama wamesoma wasingefanya kazi hizo.


Hapo kwenye nyekundu, wewe Mgagagigikoko: wee bakia tu kwenye blah blah, sisi Wamangi twabonyeza tuuu koto kote kama msumari wa mzee Yusufu-----bonyeeeeeeeeeeeeeeee; yaan tunapress tu kama Ronaldo, ikija kazi ya TRA...tuna-press, ikija ya kushona kanda mbili...tunapresss, yaan kaka ni TOTAL FUTIBOLU, wewe piga politic ukimaliza kamtafute yule mangi anayekuuziaga mtori kama yupo tena pale kwenye mtori...weeeee thubutu akae hapo kukusubiri wewe au??? wewe shika pembe sis tunakamua....kama hukusoma mzumbe ntafute nikwambie maana ya kushika pembe na kakamua (eeeh ndiyo, kukamua maziwa ndiyo)
 
JMushi,

Kubwajinga aweza kuwa ni mchanga na wala usishangae! Ila pengine ni mchaga ambaye hana chuki na makabila mengine! Hapana, mimi natania tuu..

Kungurumweupe, hapo kwenye nyekundu, hapana siyo hivo, ni kwamba ni mchaga ambaye ni mvivu, mpiga soga badala ya kufanya kazi ndo maana he remains unfit to chagaism coz he contradicts the very core values and principle za wachaga......kazi, elimu, kujituma, heshima kwa pesa.....and name it!!!

wale mabilionea wa kichaga under std 7 kule Kariakooo wanasema-ga....eshimu maaaaare wawa!!!! ie heshimu majani (i.e pesa) baba!!!!
 

weee Kungurumweupe
kama huamini ukweli wake unaandika ya nini? hap JF tunataka kusoma facts siyo udaku wa mitaani. halafu jipange fanya kazi acha kuzunguka mitaani kutafuta udaku. ndo maana Wa-mangiz twakupiga bao. wewe na wenzako mwazunguka mitaani kutafuta udaku sisi tunasoma ramaaaaa......ramani kweliiiii
 

hapo kwenye nyekundu...weeee tulia hapo hapo, hizo za kwenye magazeti mashughuri ya tz ni za mtaani ndiyo lakini tunazifanyia utafiti na uchambuzi wa kitaaluma kwanza kabla ya kupost. huo udaku wako umeufanyia utafiti gani???? nyamaza kimya kama huna la kusema, usiharibu taaluma za watu hapa, watu tumesotea bwana, ie tumesomea sis wachaga teh! teh! teh!
 
Naona watu wamecomment kwa ghadhabu sana, especially wale ambao thread hii imewagusa, kitu cha Muhimu tujue kwamba hii issue ni nzito wala si ya kupuzwa kiasi hicho. Wenzetu nchi zilizoendelea hasa za Ulaya kuna legal binding za kuzisimia nchi kutekeleza mshikamano kwa jamii mbalimbali zinazounda nchi zao. Mnaweza pitia European Charter for Regional and Maniority Languages (1992) na pia Convention for Protection of Maniorities (1994). Nchi zilizoendelea wanasoma vyuoni kozi kama Diversity managements, Social Cohesion na Social Intergration kwa ajili ya matatizo kama haya. Sisi tunafumba macho huku watu wengine wanaumia kama tunavyoona kwenye hisia zao kwenye michango yao katika thread hii. Ni muhimu tukaelewa tofauti ya ajira ya Umma na Ajira Binafsi. Kama serikali inalengo la kutumia ajira kama kigezo mojawapo cha kuleta mshikamano katika nchi si sahihi kuajiri watu kwenye sector za umma kwa kufuata kigezo cha merit tu. Kwenye suala la Umma hakuna merit hata siku moja la sivyo hata wanawake wasingeweza kuwezeshwa ili wapate ajira au kujoin vyuo kama serikali ingekuwa inafuata merit tu. Kwa tuliofanya kazi serikalini tunajua kwamba kuna kazi ambazo hazina utalaamu sana kiasi kwamba uhusiano wa merit na utendaji kazi serikali si wa kuzingatia sana. Common service ya serikali ya Tanzania wala haiitaji merit recruitment kama inavyofikilika, hiyo ingeweza kutumika kubalance uiano wa watumishi baina ya makabila.
Na siyo sahihi kabisa kuwa wachaga hawapati upendeleo katika kupata ajira kwani wanaweza wakawa wanapata upendeleo inderectly kwa kuwa ndugu na jamaa wengi wako jikoni. Kwa wale wataalamu wa Social Science, Jaribuni kujikumbusha, Social Capital ya Bourdeux na Social Network ya Granovettor ili kujua jinsi gani mambo haya yanafanyika pasipo hata wakati mwingine kujua.
Swala la wachaga, wahaya, wanyakyusa kuwa na elimu zaidi ya mabila mengine ni swala la Kihistoria toka enzi za mkoloni wala haina maana kuwa hayo makabila ndio yamedondoshewa akili toka mbinguni. Mimi natoka mojawapo ya makabila hayo na nimeowa uchagani, kama serikali itakaa kimya na haioni matatizo ya baadaye inapandikiza mbegu za ubaguzi mbaya sana. Hiyo portifolio ya ndugu Stiven Waasira ndio kazi yake, lakini wala haitumiki hivyo imekaa kisiasa tu. Kwa tuliopitia kozi za Social Diversity management, ni wazi Tanzania imeundwa na vipisi vingi vya makabila na mapande mawili ya Dini (Muslim and Christian). Na hivyo vipisi vya makabira na mapande ya dini yanahitaji hekima na utaalam kuyamanage wala si kwa kufuata merit ambayo mwisho wake inatoa ajira ya makabila machache kwenye sector za umma pia kama inavyofahamika dini mojawapo inanung'unika kwa swala hili. Ieleweke hizo ni ajira za umma wala si mtu binafsi. Ajira za Umma zitumike kujenga taifa kama inavyofanywa kwenye ajira za vyombo vya ulinzi na usalama.
Nimeambatanisha paper ya Mtalaam wa Social Capiatl and Social Networks- Robert D Putnam kwa wale wanopenda kujielimisha kwa undani nadharia hii ya Social Capital and Networks na jinsi gani unaweza husianisha na makabila yenye nguvu na dini yenye wasomi wengi kwa Tanzania jinsi yanavyofaidika na hiyo hali ili hali wengine hawajui kama wanafaidika.

Mungu ibariki Tanzania.
 

Attachments


Hivi hii success ya wachaga mbona siioni? unless our standards are too low, maendeleo ya wachagga ni ya kawaida kabisa na hayatofautiani kiadi kikubwa na ya makabila mengine.

Kama kuna tofauti, ufumbuzi wake wake ni KAZI. Wakinga ni wazuri sana katika biashara na wanapata maendeleo haraka. Hawakusaidiwa, wamrjisaidia, kwa kazi. Wamachinga wako kazini, na humo baadaye watatoka mamilionea, halafu wapo wataoanza kushangaa. KAZI, KAZI.
 
Ngoma inakuja kwa wale waliojenga utajiri wa kufa mtu Ukanda wa Afrika mashariki, kwa bidii zao bila ajira ya serikali ya bongo....[shirika landege precissiopn air][mabasi dar express].[Baa ya Mchagaa][duka la mchaga] [guest house ya mchaga] wakwere msijenichukia nishauri mchaga afunge guest house mnayoitumia iba wake za wenzenu mkijfanya vidume..haha.kuna wageni akina bakhressa, mohamed interprises.
Usishangae wabongo wakitimiza agenda wasizozijua kwa kutaja ukabila, udini etc
Naomba waingie hizo anga wakatoe wachaga, waarabu na wahindi ili wao wawe wakurugenzi....?tumekosa kazi wabongo.My friend mchaga ambaye elimu ya juu ni std seven. baba aliuza ng`ombe na kumpatia nauli ya kuenda mjini km wenzie .leo ni millionea wa kufa mtu ambaye ktk huduma zake amekuwa akikopesha wasomi wajinga wetu kwa kiasi kinachozidi mishahara yao(pombe,mahitaji ya nyumbani).Anashangaa watoto wa kiswahili wapo busy lalamikia ndugu zao hawawatoi, tangu anakuja mjini kuuza karanga, baadaye chipsi baadaye ndipo alipo...huyu ananiambia hahitaji hata kuwaajiri watu km hawa atawapa chakula, hela na sifa tuu.Ananiambia hela wanazopokea watoto wa mjini km msahahara au zawadi ni nyingi zaidi ya mataji anaohitaji leo kuanza kazi na kuwa tajiri tena within a year.Huwa anapata shida elewa hadithi ya ukabila na udini...
 
Mijadala mingine haitakiwi kufa maana nchi hii kila mtu haishi kwa jasho lake.
M'kijiji alitaka kuwatumia wachagga kueleza hali ya ukabila nchini. Michango yangu nimetoa mifano ya NBC ya Nsekela, NIC ya mwaikambo na sekta ya elimu enzi za Elinawinga.

Mwaka 1989 - 1992 ktk branch zote za NBC za jiji la Dar, ni mbili tu ambazo zilikuwa na Branch managers wasiyo Wanyakyusa! Hebu yaangalie matawi ya NBC Dar. Hapo kisomo cha Wanyakyusa kilishika kasi? Ni ukabila tu ndugu zangu.

Iangalie Wizara ya maji na wahaya. Mpaka Chuo kikapewa jina la mtu toka Bukoba, sasa hivi tena limeondolewa. Ina maana wahaya wanapenda sana kusoma mambo ya maji? NO! walipewa upendeleo wa kuingia na kuajiliwa. Hali ya wizara hiyo hadi leo iko hivyo. Makabila mengine wanangia kwa taabu saana!
 

Sikupenda kuchangia hoja hii lakini hapo kwenye red hapo juu imenilazimisha nichangie ili tuweke rekodi sawa. Huo ni uzushi mtupu. Toa ushahidi wa ubaguzi dhidi ya Chacha Wangwe. Ni bahati mbaya JF inaruhusu majina ya kuchonga vinginevyo uzushi kama huu usingekuwepo.

Mimi si mchaga wala si mbantu- mimi nimetoka mpakani mwa Singida na Manyara. Kama mwana Chadema na kama Kiongozi kwa miaka kadhaa japo kwa ngazi ya Chini - Mkiti wa jimbo la Ubungo na mjumbe wa Baraza kuu ninaomba nikuhakikishie kuwa Chadema hakuna ubaguzi anaouzunguzia Gamba la Nyoka. Hii ni proganda ya CCM na Mafisadi wake na baadhi ya watu walioajiriwa kufanya kazi hiyo humu ndani jf. Hamtaweza.
Kama ubaguzi ungekuwepo basi sisi amabao si wachaga tungeuhisi siku nyingi. Halafu labda niwakubushe.
Kamati kuu ya Chadema wachaga wako wako kama 4 au 5 ( sina hakika ) kati ya wajumbe karibu 35.
Baraza kuu lenye wajumbe karibu 200 wachaga ni wachache sana. Huu ubaguzi wa wachaga uko wapi mbona sis tulio ndani ya Chadema ambao si wachaga hatuuoni?
Mkutano mkuu ndo usiseme kabisa. wachaga ni wachache mno. Mbowe ni mkiti si kwa sababu ya Uchaga wake bali uchapaji kazi wake. Angalia rekodi yake wakati anaaza uenyekiti na mahali tulipo sasa. Yeye na Dr Slaa, Mnyika na viongozi wengine walichapa kazi.
CCM walipiga kelele miaka iliyopita kuhusu wabunge viti maalum wengi ni wachaga wakati wabunge wale kila moja alitoka mkoa wake kiasi kwamba hata chama ilikuja kushtuka baadaye- Maana sisi hatuulizana wewe kabila gani. Mwaka huu CCM na makuwadi wake wamefunga midomo kuhusu Viti maalum ya Chadema.
Chadema ni Chama bora cha Upinzani Tanzania, hakina ubaguzi kabila au dini. Mlio nje jiungeni tujenge nchi yetu.
 
Nimekuwa naiignore hii thread kwa muda mrefu sana, kumbe I was making a mistake.
Nauhakika kwamba mchaga mmoja akitangaza kuachia ngazi alafu kajitokeza ****** kuiomba, Mwanakijiji utalazimika kuja na proposal mbadala.

Baada ya wachaga kumaliza, na wakisto wawaachie waislamu....
 

Weye kweli ni spiner. Mbona una spin toka kinachozungumziwa unakwenda kinyume. Theme ni ukabila, ajira (serikalini) na usomi. Mambo ya kuuza karanga, bar, mbege, n.k. unayaingiza ya nini?

Lakini pia lazima nikukomalie sijui kama umesoma messages zote. Ukiwasifu kwa kupewa nauli na kuelekea mjini na baadaye kuibuka mamilionea ni sawa na kuwasifu waarabu kwamba waliuza hata binadamu ili maisha yawe mazuri kwao. Hata hivyo kuna mtu kisha uliza, Huko Moshi mbona hawavumilii makabila mengine kuanzisha biashara wakati wao wako miji ya wengine?
 
Baada ya wachaga kumaliza, na wakisto wawaachie waislamu....

hapa umepatia kabisa kejeli inakoelekea; kama "tatizo la Tanzania ni wakristu, basi wakristu walioko madarakani waachie ngazi na kuwapisha watu wa dini nyingine"
 

Kinachoongelewa hapa ni ajira ya Umma wala si biashara binafsi. Hakuna mtu anazuiwa kuwa mjasiria mali. Sio kila mtu anauwezo wa kunzisha biashara kubwa. Hata kwenye biashara kuna networks, leo hii ni rahisi sana mkinga kujua biashara gani nzuri na kujua kama kuna chumba cha kukodisha au kinauzwa sokoni kariakoo kuliko makabila ambayo hayana network pale kariakoo. Hivyohivyo ni rahisi sana Mhindi kujua kuwa kuna nyumba ya serikali iko wazi upanga kuliko mswahili anayeishi Tandale kwa Mtogole. Na ndio hilo linalosemwa kwa ndugu zangu wachagga, wanyakyusa, wahaya na wapare, wako wengi serikalini wanajua kinachoendelea huko. Kuwepo wengi serikali tu ni network tosha ya kumanipurate chance zinazotokea serikalini. Jaribu kusoma social networks zinavyofanya kazi. Ukiwa ndani ya network wala hata huwezi jua kama unapendelewa na mfumo uliopo
Vilevile hapa sijasema kuwa wachagga wameendelea sana, hapa swala ni ajira ya umma ambayo inatakiwa uwiano wa Taifa, ajira ya umma ni sura ya Taifa. Sijui kama itakuwa vizuri kwa ajira ya umma waajiliwe wabembe tu, eti kwa kuwa hailipi, au hakuna mshahara wa kutosha, hilo si sahihi kabisa. Kama vyombo na Ulinzi na Usalama ajira zinatoka kwa kanda, kwa nini TRA, PSPF, BOT, PCCB, IMMIGRATION na sector zingine nyingi ambazo wamejaa wachagga, wahaya na wanyakyusa haziendi kwa uwiano. Hilo unaona ni sahihi?. Je tuendelee kuajiri kwa merit tu?. Je merit ni sahihi kwa Taifa kama hili lenye makabila lukuki?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…