WanaJF,
MMK nashukuru kwa makala yako. Nilikujibu kule kwenye CEO WA TANROAD bila kujua kuna makala mpya. Najua lengo lako la kuandika hili ni kuwasha MOTO. Huu moto hata mie ndiyo lilikuwa lengo langu kuwa hii habari ni vema tuijadili ikibidi tuanze kufikiri nini kifanyike maana huko twendako inaweza kuwa hali mbaya. Mama kasema kuwa sasa hivi wasomi wengi Tanzania hivyo wengi kukataa kuwa akina Msuguri. Sasa wanakuta juu KUMEZIBWA. Hapa kwenye neno KUMEZIBWA kuna maana nyingi saana na chanzo chake kiko kwa walioziba na waliozibiwa. Ila ningelipenda pia kusema "form uliyotumia kuandika inaweza kuleta maana mbilimbili". Moja wapo ambayo naweza kuina haraharaka ni hii kuwa "Wachaga wakiondoka, nyie Wadanganyika mtafanya nini..?" Inanikumbusha yale maneno "mimi ndiyo njia ya kweli na uzima, mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.." Anyway huo ni muono wangu. Na hata wakiondoka ukweli ni kwamba "Kufa hatutakufa ila Cha mtema kuni tutakiona.."
Naomba niweke ile makala yangu iliyokuwa kwenye thread nyingine....::>>>>
Hapa tatizo si WACHAGA. Kwa wengine tunajua hili ila "ukiingia kichwani kwa watu wasioona mbali kwa mbele na kwa nyuma utaona kabisa wao tatizo ni Mchaga/Mhaya..." Tatizo ni kuwa kwa nini wengine WAMEBAKI NYUMA? Wamebaki nyuma kiasi kwamba hata ungelikuwa Chenge, ukitaka kuajiri na kutafuta hizo SIFA utaona kuwa waliokuzunguka ni Wachaga/Wahaya. Nilipokuwa JKT tulikuwa tunaandikisha na dini yako/Kanisa. Mhhh, asilimia 90 ya watu JKT walikuwa WAKATOLIKI. Pia hapa ukitaka kuajiri utaona kuwa WANAOSTAHILI ni hawa Wakatoliki. Sasa tatizo ni WAKATOLIKI WANAPENDELEANA??? Hapa tatizo ni kama alilosema Jokakuu na mimi kulielezea mapema kuwa ni HISTORIA imefanya hivi. Tatizo si kuwa WACHAGA waache kazi au wasiajiriwe. Itakuwa yaleyale ya Uganda kufukuza Wahindi ingawa kuna wengine wanasema INAWASAIDIA SANA LEO. Sijui kama ni kweli au kwa sababu wana M7. Hili swala inabidi kwenda MORE DEEP na si kulichukulia juu juu. Kama ni hivyo, na mie napendekeza "Wakatoliki waache kazi na au wasiombe/wasipewe kama kwenye hicho kitengo juu yupo MKATOLIKI".
Narudia tena kuwa jamani makabila makabila mengine yako nyuma saana. Nafikiri kuna haja waliojuu kukaa na kupanga jinsi ya kubadilisha maisha ya MAKABILA yaliochini sana. Hii ifanyike kwa njia zote ziwezekanazo na HARAKA. Kwa kuwasomesha, kuwapa misaada ya maendeleo na kuhimiza hayo maendeleo na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwaeleza umuhimu wake na ikibidi (kama hawataki) basi hata kwa VIBOKO. I wish kule kwetu aje dikteta atakeyutumia mabavu kuwatoa masikini wale Misri na kuwafikisha nchi ya ..... ehhh naogopa kusema maana mabomu yanalipuka kila siku.