Mtoto wa masikini anatumia akili kubwa ili apate pesa ila mtoto wa tajiri anatumia akili kidogo ili kupata pesa. Hivyo watoto wa masikini wana upeo mkubwa kuliko watoto wa matajiri.Je viongozi wanatoka kaya masikini nao wanaakili za kimasikini mfano Mwigulu!?
Nasema hivi kwasababu nimegundua wakati mwingine ukitoka kwenye familia masikini sana sio wote lakini wengine bado wanabaki na akili za kimasikini. Wanafikiri utajiri ni kulimbikiza mali na kuiba lakini wanasahau kwamba unatakiwa kubadilika kimawazo
Mwigulu ukiangalia tu majigambo yake mfano utajua katokea familia masikini sana na bado ana mawazo ya kimasikini
Mfano. Kwa Mwigulu anaona ni bora sana kupeleka watanzania wakafanye kazi za ndani kwa waarabu huko Qatar kazi za kitumwa na unyanyasaji bila kipato cha maana. Majirani zetu wanafikiria uwekezaji na kazi nzuri kama viwanda mfano hapo Kenya juzi. Huyu ni mtu ambaye akienda kwa diaspora kama USA ambao wengine wana kazi za maana na wasomi anawakimbia na hata hawezi kuongea nao lakini akienda sehemu yenye wafanyakazi wa ndani kama nchi za uarabuni anakuwa kimbele mbele kuongea nao maana watamuona wa maana sana kwao na anaweza kujigamba kwao zaidi. Hizi ni fikra za kimasikini
Tusiogope kabisa kuchagua watu ambao wana fikra kubwa mfano Dr Kimei kapuuzwa kwasababu hizi ana mawazo na akili kubwa kuliko wenyewe. Haya ni mambo yanayo zuia maendeleo
Baba yangu alikuwa mkubwa CCM na serikalini miaka ya 1970s, akanunua ardhi kwa hela halali aliyokuwa anapata.Mtoto wa masikini anatumia akili kubwa ili apate pesa ila mtoto wa tajiri anatumia akili kidogo ili kupata pesa. Hivyo watoto wa masikini wana upeo mkubwa kuliko watoto wa matajiri.
Kongole sana ndugu kwa kuufunga huu uzi kwa mchango bora wa uhalisia na ukweli.Mara nyingi mtu anayependa kuongelea mambo ya maskini na umaskini ni mtu aliyezungukwa na umaskini. Huwezi kukuta mtoto wa tajiri hasa aliyezaliwa kwenye mzunguko wa pesa anaanzisha thread kama hizi. Kwani kuzaliwa kwenye umaskini dhambi!?,kwanini tusiache nature ijiendeshe?,kuna umuhimu wowote wa ku identify mtu asili yake na juhudi zake kwa vigezo vya asili yake ya umaskini!?,nitajie mtu/tajiri mmoja ambaye Babu wa Babu yake hakuwa maskini wa kutupwa kuanzia Jk,Dangote, Bakhressa, hata huyo Chivayo aliyekufa Jana ambaye generation yake huko nyuma haikuwa maskini!?, nadhani una chuki binafsi na Mwigulu.
Mtoto wa masikini anatumia akili kubwa ili apate pesa ila mtoto wa tajiri anatumia akili kidogo ili kupata pesa. Hivyo watoto wa masikini wana upeo mkubwa kuliko watoto wa matajiri.
Hakuna akili ya kimaskini, unajua form four,form six na vyuo kwasasa wanaomaliza hizo level na kuingia mitaani ni watu wangapi kwa mwaka!?,kwahiyo waziri mkuu kuwatafutia fursa za kazi Qatar ndo akili za kimaskini!?,hao Kenya unaowatolea mfano unajua kwamba wanaongoza Africa mashariki kufanya kazi za ndani na ulinzi uarabuni!?,je hawana viwanda kibao nchini!?,tatizo hujui ukubwa wa tatizo la ajira na nilichogundua huna takwimu zozote na nina uhakika wewe ndo una akili za kimaskini.Hatuongelei upeo hapa Mwigulu ni mwana Ilboru mwenzangu na akili anayo sana tu lakini kuwa na akili za kimasikini haina maana huna akili!