Je, vipofu huota ndoto?


Hili ni swali hupatikana sana kwenye elimu ya hisia ya sita. Kesho nikipata muda naweza kufafanua zaidi kuhusu jibu langu katika swali hili zuri.

Jibu lake hapa ni ndiyo, vipofu hata wa kuzaliwa nao huota ndoto ingawa hizo ndoto zao ni tofauti na za watu wenye uwezo wa kuona.

Kwa kukosa kwao uwezo kuona, ndoto za vipofu mara nyingi huwa zimejaa mguso, sauti, harufu na ladha.

Hisia ambazo kwa ujumla hutokea mara chache sana katika ndoto za watu wenye kuona.

Ova
 
Uthibitisho wa vipofu ninao mmoja, japo hauhusiani na ndoto,

Tungepata mchangiaji wa mada aliye kipofu wa Kuzaliwa, maswali yangepungua.
Hata kama ukiwauliza vipofu swali hili, watakujibu hapana. Ila sio lazima wakijibu hapana huwa ni kwa sababu hawaoti ndoto za kuona.

No! Wanaweza kusema hapana kwa sababu hawajui picha za kuona zikoje.

Mtu anayeona analitambua papai kwa macho kwa sababu amewahi kuliona papai na kulila katika ulimwengu wa kawaida.

Hivyo, ana uwezo wa kuunganisha picha ya papai na ladha, harufu, umbo na mguso wa papai hata kwenye ulimwengu wa ndoto.

Ikiwa mtu hajawahi kuliona papai kabisa kwenye ulimwengu wa kawaida, ikiwa ataliona kwenye ulimwengu wa ndoto, hata ukimuuliza kama amewahi kuliota papai ndotoni, atasema hapana kwa sababu halijui.

Ila tafiti zinaonesha vipofu wa kuzaliwa hupata ndoto za picha pia, lakini sio mara nyingi kama ndoto za harufu, sauti, ladha na kugusa.

Ova
 
🤣🤣🤣🤣Dogo huu ujinga wa out of body experience ushakuwa debunked ni story tu...ndo maana muislamu ataona mbingu yenye bikra mkristo ataona mansions na streets of gold Mhindi ataona mbingu yenye miungu yake...Sasa wewe niambie Kuna mbingu na hell ngapi kama kila mtu anaona Cha kwake...hizo ni product of mind na washatafiti wakagundua hamna Cha maana hapo
 
🤣🤣🤣So we elimu ya mudi ya kusema Kuna dunia Saba na mbingu Saba zenye majimaji katikati na kiti kwa juu...we unaona ndo elimu ya maana sio
 
Uthibitisho wa vipofu ninao mmoja, japo hauhusiani na ndoto,

Tungepata mchangiaji wa mada aliye kipofu wa Kuzaliwa, maswali yangepungua.
Yah ndio ugumu wa swali unapokuja hapo.
 
Hapo kwenye ndoto za picha Kwa kipofu wa Kuzaliwa ndo penye utata.

Tafiti zinasemaje?
 
Tulia WEWE YAI VIZA.

Acha wataalamu wajadili mambo mazito.

Kwani NOTES ZAKO ZA FOM FOO zinasemaje?
 

Mkuu tunapishana kwa sababu tunajadili vitu viwili tofauti

Mimi najadili kuhusu kipofu kuota
Wewe unajadili kuhusu kipofu kuota ANAONA

Ipp hivi
Kipofu anaota kulingana na anavyo experience maisha anayoishi
Mfano, kipofu ataota anazagamua, ataota mtoto wake kapasi mtihani, ataota kazinguana na mkewe nk nk

Zingatia
Kuota ndoto sio lazima uone
Hata ukizaliwa huoni husikii nk as long as brain yako ipo active basi utaota kwa kadiri ya namna unavyoishi
 
Ndugu, Mimi nimeenda kigoma majuzi tu hapa nikaliona Hadi ziwa Tanganyika na mchanga wake ulivyo na nikajua hapa ni kigoma kupitia NDOTO na sijawahi kufika kigoma tangu kuzaliwa.

Hilo unalielezeaje?

How did you know ulichokiota ndio ziwa halisi?
 
Vipofu huota pia mkuu,

Binadamu ni vitu vikuu vitatu yaani spirit soul and body, na kwenye hivi ni spirit pekee ndio hupelekea kiumbe anayeitwa binadamu kuweza kuota ndoto.
 
Hapo kwenye ndoto za picha Kwa kipofu wa Kuzaliwa ndo penye utata.

Tafiti zinasemaje?

Mwaka 1999 Dream researchers wa chuo kikuu cha Hartford walifanya tafiti kwa vipofu

Wale walio wahi kuona kabla huwa bado wanaota waliuoyaona kabla hawajapofuka, na kadiri muda unavyo kwenda nmna ya kuota inabadilika kadiri wanavyoishi

Wale amba hawajaona kabisa wanaota kwa kadiri wanavyoishi..... no visuals dreams
Wana namna yao ya ku genarate uhalisia wa umbo la kitu through touching na hisia
 
Ahsante.
 
How did you know ulichokiota ndio ziwa halisi?
Ile ilikuwa Si ndoto, ni Advanced ndoto, inaitwa MAONO.

Ni halisi kabisa, Si imagination, natembea ,nasikia na kuona kabisa.

Mtu Si mwili, mtu ni ROHO, unaweza Toka ndani ya MWILI na kwenda upatakapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…