Je, vipofu huota ndoto?

Je, vipofu huota ndoto?

Salaam, shalom!!

Twende haraka kwenye mada, nimekuwa nikipost mada za intelligence ya Mbinguni katika jukwaa hili na zinahamishiwa majukwaa mengine,

Leo tuanze mwaka na swali hili, Je vipofu wa Kuzaliwa huota ndoto?

Kurahisisha upatikanaji wa jibu kuhusu ndoto za vipofu, tupate tafsiri ya

1. Silver cord/ Kamba ya Fedha. 2. Mtu/ Roho/ Spirit 3. NAFSI 4. Mwili. 5. NDOTO. 6. ULIMWENGU WA ROHO.

1. SILVER CORD/ KAMBA YA FEDHA.
Hiki ndicho kiunganishi kati ya MWILI wa mtu na Roho. Inapatikana katika ( Mhubiri 12:6): Or ever silver cord to be loosed. Ukisikia mtu amekata Kamba, ndo hii silver cord.

2. MTU/ Spirit/ Roho.

MTU- Ni ROHO, ANAYO NAFSI NA ANAISHI NDANI YA MWILI.

3. NAFSI./ Soul.
Mwili/ udongo ulipopuliziwa Pumzi ya uhai, ikazaliwa NAFSI. (Mwanzo 2:7) Ikumbukwe, Pumzi ya uhai ndiyo Roho.

NAFSI ndiyo inayobeba hisia, akili, uwezo wa kufanya maamuzi. Hapa ndipo panapochakata taarifa Kutoka kwenye Mwili na Kutoka kwenye Roho( mtu). Kumbuka hisia, akili, will vyote havishikiki katika mwili physical bt vipo.

4. MWILI.

Hili ni frame, kopo, vazi la mtu ambaye ni ROHO. Mwili Si mtu, Bali mwili ni vazi la mtu ambaye ni ROHO.

Katika mwili Kuna Ubongo, lakini akili Iko katika NAFSI.

Ukienda msibani, utasikia tunaenda kuaga mwili wa marehemu, marehemu na mwili ni vitu viwili tofauti.

5. NDOTO - Ni tukio halisi Si illusions kama wanasayansi wengi wanavyodhani. NDOTO ni tukio linalofanyika katika Ulimwengu wa Roho wa mwili au katika Ulimwengu wa Roho.

NDOTO type 1- Hizi ni za Kutoka kwenye Mwili kupitia macho na mawazo ndizo ziitwazo ndoto kulingana na shughuli za Kila siku. ( Mhubiri 5:3). NDOTO huja Kwa shughuli nyingi.

NDOTO TYPE 2- Hizi ni Kutoka katika Roho, NAFSI inazipokea na akili itatunza kumbukumbu, ukiamka, utakumbuka ulichoota. NDOTO hizo ni HALISI Si imagination, ni wewe ambaye ni ROHO Huwa unaona au kwenda na kutuma taarifa katika NAFSI kupitia silver cord.

(Ayoub 33:15) katika ndoto, katika maono ya usiku, USINGIZI mzito uwajiliapo watu, katika USINGIZI kitandani.

6. ULIMWENGU WA ROHO.

Kwakuwa mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI, anapata na kutunza taarifa zote katika kitu kinachoitwa NAFSI.

Matukio yanayotengenezwa katika Ulimwengu wa mwili, NAFSI itayachakata na utayaota kupitia akili iliyo ndani ya NAFSI.

Matukio yaliyotokea kwenye Ulimwengu wa Roho, ,utayapata sababu silver cord imeungwa na mwili, NAFSI itakuletea tukio Hilo halisi kupitia ndoto, na ndoto zote ziko katika Ulimwengu wa Roho wa Nuru au Giza.

Hivyo mtu kipofu, kwakuwa Yeye ni ROHO, tutakuwa kwenye nafasi nzuri kujua ikiwa anaota ndoto au la. Na ikiwa anaota, ni Kwa mfumo upi?

MY LIFE EXPERIENCE.

Nimewahi Kutoka ndani ya MWILI wangu nikiwa mdogo na nikaenda mbali sana pazuri mno na kuona vitu ambavyo sijawahi kuviona duniani.

Swali ni je, vipofu waliotoka ndani ya miili Yao kama Mimi nilivyotoka ndani ya MWILI wangu, wanaweza kuona? Maana Mimi nilivyotoka ndani ya MWILI wangu sikutumia macho ya MWILI, kumbuka mwili niliuacha chumbani.

Cc:Sea Beast

Karibuni🙏

Hili ni swali hupatikana sana kwenye elimu ya hisia ya sita. Kesho nikipata muda naweza kufafanua zaidi kuhusu jibu langu katika swali hili zuri.

Jibu lake hapa ni ndiyo, vipofu hata wa kuzaliwa nao huota ndoto ingawa hizo ndoto zao ni tofauti na za watu wenye uwezo wa kuona.

Kwa kukosa kwao uwezo kuona, ndoto za vipofu mara nyingi huwa zimejaa mguso, sauti, harufu na ladha.

Hisia ambazo kwa ujumla hutokea mara chache sana katika ndoto za watu wenye kuona.

Ova
 
Uthibitisho wa vipofu ninao mmoja, japo hauhusiani na ndoto,

Tungepata mchangiaji wa mada aliye kipofu wa Kuzaliwa, maswali yangepungua.
Hata kama ukiwauliza vipofu swali hili, watakujibu hapana. Ila sio lazima wakijibu hapana huwa ni kwa sababu hawaoti ndoto za kuona.

No! Wanaweza kusema hapana kwa sababu hawajui picha za kuona zikoje.

Mtu anayeona analitambua papai kwa macho kwa sababu amewahi kuliona papai na kulila katika ulimwengu wa kawaida.

Hivyo, ana uwezo wa kuunganisha picha ya papai na ladha, harufu, umbo na mguso wa papai hata kwenye ulimwengu wa ndoto.

Ikiwa mtu hajawahi kuliona papai kabisa kwenye ulimwengu wa kawaida, ikiwa ataliona kwenye ulimwengu wa ndoto, hata ukimuuliza kama amewahi kuliota papai ndotoni, atasema hapana kwa sababu halijui.

Ila tafiti zinaonesha vipofu wa kuzaliwa hupata ndoto za picha pia, lakini sio mara nyingi kama ndoto za harufu, sauti, ladha na kugusa.

Ova
 
Yupo,

Anaitwa mtu wa ndani. Ndiye ROHO.

Ikiwa una ndugu aliyewahi fanyiwa upasuaji nusu kaputi atakupa experience.

Anaweza kuona Kila kitu madaktari wakifanyacho while mwili haujitambui na anaweza kuona Hadi vyumba vingine nini kinaendelea, hata nyumbani alikotoka bila kizuizi chochote.

Tafiti, yapo mengi usoyajua.
🤣🤣🤣🤣Dogo huu ujinga wa out of body experience ushakuwa debunked ni story tu...ndo maana muislamu ataona mbingu yenye bikra mkristo ataona mansions na streets of gold Mhindi ataona mbingu yenye miungu yake...Sasa wewe niambie Kuna mbingu na hell ngapi kama kila mtu anaona Cha kwake...hizo ni product of mind na washatafiti wakagundua hamna Cha maana hapo
 
Nyie MAKASUKU WA SHULE ZA KATA huwa mnanishangaza sana. Mkikariri jambo kwenye NOTES ZENU basi linakuwa kama ANDIKO LA DINI.

Na bahati mbaya huko kwenye MASHULE YA KATA wanawalisha mayai viza basi mnameza kweli kweli na kuyajambia juu kwa juu.

Ni bora nimsikilize mwendawazimu kuliko KASUKU WA SHULE YA KATA.
🤣🤣🤣So we elimu ya mudi ya kusema Kuna dunia Saba na mbingu Saba zenye majimaji katikati na kiti kwa juu...we unaona ndo elimu ya maana sio
 
Uthibitisho wa vipofu ninao mmoja, japo hauhusiani na ndoto,

Tungepata mchangiaji wa mada aliye kipofu wa Kuzaliwa, maswali yangepungua.
Yah ndio ugumu wa swali unapokuja hapo.
 
Hata kama ukiwauliza vipofu swali hili, watakujibu hapana. Ila sio lazima wakijibu hapana huwa ni kwa sababu hawaoti ndoto za kuona.

No! Wanaweza kusema hapana kwa sababu hawajui picha za kuona zikoje.

Mtu anayeona analitambua papai kwa macho kwa sababu amewahi kuliona papai na kulila katika ulimwengu wa kawaida.

Hivyo, ana uwezo wa kuunganisha picha ya papai na ladha, harufu, umbo na mguso wa papai hata kwenye ulimwengu wa ndoto.

Ikiwa mtu hajawahi kuliona papai kabisa kwenye ulimwengu wa kawaida, ikiwa ataliona kwenye ulimwengu wa ndoto, hata ukimuuliza kama amewahi kuliota papai ndotoni, atasema hapana kwa sababu halijui.

Ila tafiti zinaonesha vipofu wa kuzaliwa hupata ndoto za picha pia, lakini sio mara nyingi kama ndoto za harufu, sauti, ladha na kugusa.

Ova
Hapo kwenye ndoto za picha Kwa kipofu wa Kuzaliwa ndo penye utata.

Tafiti zinasemaje?
 
🤣🤣🤣🤣Dogo huu ujinga wa out of body experience ushakuwa debunked ni story tu...ndo maana muislamu ataona mbingu yenye bikra mkristo ataona mansions na streets of gold Mhindi ataona mbingu yenye miungu yake...Sasa wewe niambie Kuna mbingu na hell ngapi kama kila mtu anaona Cha kwake...hizo ni product of mind na washatafiti wakagundua hamna Cha maana hapo
Tulia WEWE YAI VIZA.

Acha wataalamu wajadili mambo mazito.

Kwani NOTES ZAKO ZA FOM FOO zinasemaje?
 
kwa sababu kipofu baye kazaliwa hivyo maana yake huyo hajawahi kuona chochote tokea anazaliwa.

Hiyo maana yake ni kwamba hana kumbukumbu ya picha yoyote kwemye akili yake kwa sababu hajawahi kuona kitu hicho.

Ni kama ambavyo wewe huwezi kuwa na picha ama kumbukumbu yoyote kuhusu kitu ambacho haujawahi kukiona.

Sula sio kuishi bali suala ni kuona kaka.

Leo nikikaa nikikuambia simba anatisha moja kwa moja kichwani kwako itakuja picha ya simba kwa sababu ulishawahi kumuona na ile picha ikahifadhiwa kwenye akili yake.

Hao walishaona tayari so zile picha pabdo zipo kwenye kumbukumbu.

Kumbuka akili ya binadamu inafanya kazi ya kuhifadhi mambo uliyoyaona nyuma so kama utapofuka baadae bado zile kumbukumbu zitakusaidia kuona picha kwenye ndoto.

Je MTU AMBAYE HAKUONA TOKA KUZALIWA ANAOTAJE NDOTO ZA PICHA WAKATI HAJAWAHI KUONA ?

Mkuu tunapishana kwa sababu tunajadili vitu viwili tofauti

Mimi najadili kuhusu kipofu kuota
Wewe unajadili kuhusu kipofu kuota ANAONA

Ipp hivi
Kipofu anaota kulingana na anavyo experience maisha anayoishi
Mfano, kipofu ataota anazagamua, ataota mtoto wake kapasi mtihani, ataota kazinguana na mkewe nk nk

Zingatia
Kuota ndoto sio lazima uone
Hata ukizaliwa huoni husikii nk as long as brain yako ipo active basi utaota kwa kadiri ya namna unavyoishi
 
Ndugu, Mimi nimeenda kigoma majuzi tu hapa nikaliona Hadi ziwa Tanganyika na mchanga wake ulivyo na nikajua hapa ni kigoma kupitia NDOTO na sijawahi kufika kigoma tangu kuzaliwa.

Hilo unalielezeaje?

How did you know ulichokiota ndio ziwa halisi?
 
Vipofu huota pia mkuu,

Binadamu ni vitu vikuu vitatu yaani spirit soul and body, na kwenye hivi ni spirit pekee ndio hupelekea kiumbe anayeitwa binadamu kuweza kuota ndoto.
 
Hapo kwenye ndoto za picha Kwa kipofu wa Kuzaliwa ndo penye utata.

Tafiti zinasemaje?

Mwaka 1999 Dream researchers wa chuo kikuu cha Hartford walifanya tafiti kwa vipofu

Wale walio wahi kuona kabla huwa bado wanaota waliuoyaona kabla hawajapofuka, na kadiri muda unavyo kwenda nmna ya kuota inabadilika kadiri wanavyoishi

Wale amba hawajaona kabisa wanaota kwa kadiri wanavyoishi..... no visuals dreams
Wana namna yao ya ku genarate uhalisia wa umbo la kitu through touching na hisia
 
Ahsante.
 
Back
Top Bottom